Kuna mtu anataka kunitapeli naomba msaada

Mkuu adi debtor aje kuwa bad debtor au deni liwe bad debt kuna conditions lazini zikidhi ndo tutasema deni limekuwa bad debt.....kwa situation ya huyo jamaa bado kuwa bad debt.

Huyo ni debtor sema inabidi apo aweke % za provision for doubtful debts , Mana apo kuna uwezekano asilipwe deni lote coz hiyo amount ya mkopo ni kubwa mno ukilinganisha na situation waliokopesheana.

Mkuu pambana mi naamini ukikaza sura pesa yako utapata japo nahisi kupata zote si rahisi kihvyo.

Ila sku nyengine usifanye huo mchezo (don't put all your eggs in one bucket) na usiwaamini watu ktk biashara...apo ungechukua ata laki 4 ufanye hyo biashara,nyengine (laki 2) ungewekeza Kwenye kuuza ata pipi na karanga... nyengine (laki 2) ungeiweka bank kama akiba itakayo baki ndo pocket money kilinda mfuko na tumbo.
 

Dah pole sana, ila mtu haumjui wala nin unamuachia mzigo wote. Biashara ni kutake risk lakini hii imezid Broo
 
Kusoma kwako kwote mpaka level ya degree hujawahi kusikia kua

"usiweke mayai yako yote kwenye kapu moja"

Mbona hyo ni general rule kila mjasiriamali na mfanya biashara anaijua we ulisahauje ukaenda kununua mzigo wa laki tisa out of milion apo hata hujui mzunguko wa biashara upoje

Pole sana there are more to come, be SMART.
 
Ukiwa na milioni...fanya biashara ya laki...principles of business...sio wewe umekopa 5m bank yote unatumbukiza kwenye biashara....ukikopa benki mill 10 hakikisha wewe na 40mill zako ...principles of business...
 
Chikolombe njo nkupeleke kwa mganga tunamtoa magamba mwili mzima kama hao samaki aliodhulumu.

Mganga achukui pesa mpaka umuhakikishie jamaa katoka magamba mpaka kwenye macho.
 
Dah! pole sana mkuu ila kwa mwenendo huo ni rahisi sana kudhurumiwa kirahisi labda muwe mliandikishana vinginevyo ni maumivu tu.
 
Hivi una miaka mingapi mpendwa maana naona bado akili ya kitoto unakusumbua

Hiyo hela huipati ng'oo 😂
 
Huko chuoni dogo unasome ujinga gani kwanza umenunua samaki pcs 2000 umeshindwa kuzitunza vizuri umefikisha pcs 1300tu na bado hizo samaki umekwenda kumkabidhi tapeli

Ningekuwa Mimi ndio baba yako ungenirudishia pesa za karo sio kwa utopolo wa kiwango hicho
 
Aligundua haujui kuandika hela ndio maana anataka kukutapeli
 
Mshushe busha tu.
Yaani hiyo pesa yako bora unge bet au ungehonga mtoto mzuri umtafune kwa mwaka mzima.
 
Nenda mahakaman kafungue kes ya madai, jamaa anakutingishia kiberiti ukijidai mtu wa kanisa umeumia , dunia hi unatakiwa uwe na roho mbaya kwa mtu anae kufanyia ubaya

Hii dunia haipo kwaajili ya watu wenye mioyo mizuri
 
Vijana wengi siku hizi mnaenda vyuoni kwa sababu vyuo vina nafasi.
 
Umenikumbusha machungu Jamanii, hawa watu wa sokoni sio kabisa. Watu wa sokoni wengi ni matapeli
Na wengi ni Washirikina.

Asilimia kubwa ya walioshika hizi biashara hawana shule wanategemea sana ushirikina.
 
Kuna mtaalam mmoja aliwahi kusema "kasi ya kiongozi wa wahuni ndio kasi ya wahuni wenyewe", dogo next time respect your money! Otherwise utaishia kuwa km huyo mwamba kwenye avatar yako
 

We are twins, ndio maana tulipendana toka mwanzo humu! Hahah nakusalimu kipenzi.

Kiukweli kijana kanisikitisha sana ni vile tu sina chakumsaidia.
 
Vijana wengi siku hizi mnaenda vyuoni kwa sababu vyuo vina nafasi.
Kuna mtaalam mmoja aliwahi kusema "kasi ya kiongozi wa wahuni ndio kasi ya wahuni wenyewe", dogo next time respect your money! Otherwise utaishia kuwa km huyo mwamba kwenye avatar yako
Nyote nyinyi inaonesha hamjawahi kuuza hata pipi kwahiyo nyamazeni kwa sababu hakuna mnachojua!!

Alichofanya dogo kwa kiasi kikubwa ndicho kinachofanyika, kwahiyo acheni kumkejeli wakati hamjui lolote!! BIashara za aina hii zinaenda kwa "mali kauli"!
 
Hao ndio maadui wa maendeleo, hakika umedhulumiwa, hakuna sababu ya kwenda huko , mwombee dua afe tu.

Mloge afie huko

Pole.
Sasa akifa si atakufa na mtaji wake... halafu baada ya hapo arudi kijiweni, au?!

Lakini bora umeona tatizo kuliko wale wanaomkejeli wakati dogo kama huyu alitakiwa kupongezwa! Watu boom wanapigia pombe tu lakini yeye akawa ana-save ili baada ya kumaliza chuo awe na pa kuanzia!!
 
We are twins, ndio maana tulipendana toka mwanzo humu! Hahah nakusalimu kipenzi.

Kiukweli kijana kanisikitisha sana ni vile tu sina chakumsaidia.
Mie niko poa best, ya huyo kijana we acha tu!!

Hawa wanaomkejeli natamani kuwapiga makofi... mbaya zaidi wanamkejeli kwa kitu wasichokijua manake wangekuwa wanafahamu biashara za jumla masokoni zinaendeshwaje wala wasingekuwa wanamkejeli!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…