Kuna mtu anamjua huyu mama?

Kuna mtu anamjua huyu mama?

Baada ya kumuona kwa muda mrefu, sikumoja nilimshukia kuzungumza nae just for curiosity. Siku hiyo alikuwa ametinga nguo mpya ya kitenge cha wax huku ameoverduu wanja na lipstick.

Watoto wake anawanyoa vizuri mitindo mitindo na wana afya njema.

Anaongea very comfidently kuwa yeye ni Mtanzania wa Kigoma alikuwa mfanya biashara mkubwa akipeleke vitenge vya Zaire Nairobi na Kampala. Akapata bwana Mkenya wakaoana na kuzaa nae watoto hao wanne. Kumetokea kutoelewana hivyo bwana amemtelekeza hali iliyopelekea yeye kuchukua kilicho chake na kurejea kwao nyumbani Kigoma.

Alipofika Dar, ameibiwa kila kitu, hivyo anatafuta nauli ya kurudi kwao Kigoma.
Kwa vile hana ndugu ameamua kujihifadhi kando ya bahari ya Hindi akisubiri misaada ya wafadhili huku akidunduliza nauli, ikitikia ataendelea na safari yake.

Nlimdadisi zaidi anaishije nja nauli ni kiasi gani, akaniambia 100,000 inamtosha, akasema ameshawahi kuhojiwa Cliods Redio, na kuomba msaada lakini hajafanikiwa. Nlimuuliza kuhusu kujiremba, akasema yeye ni mwanamke, lazima ajijali, akaniambia tena nguo zake kama hilo tenge jipya, ameshona mwenyewe kwa sindano ya mkono na kunionyesha ni kweli.

Nikamuuliza anasurvive vipi na chakula anapata wapi, ajibu wasamaria tuu wengine wanampa pesa na wengine wanamletea chakula na hadi nguo za watoto.

My Obsevation: Ukimsikia anavyoongea, she is perfectly normal, ila the way anavyoongea akiwa relaxed huku anasmile na kurembua macho, utajua tuu she is not ok upstairs ila sio kichaa wa level ya kuokota makopo.

Lafudhi ya Kiswahili chake pia imelalia zaidi Zaire kuliko Kigoma. Kwa jinsi anavyojimake up, na umbo lake linalipa, naamini kabisa usiku, walinzi walinzi wanajisevia na kuachia japo jelo jelo, hivyo kutokana na mental case yake, sidhani kama ni kweli nauli ndio tatizo, bali Mama hapo amefika.

Huyu mama anahitaji msaada wa kisaikolojia kabla hajawaharibu hao malaika, sijui hii idara yetu ya Ustawi wa Jamii inafanya nini, maana hiyo ndio njia ya Ikulu, wakubwa wote wanampita hapo na wanamuona, but nobody bothers.

Nilimalizia kwa kumuachia chochote kitu, kwa imani hata ningetoa hiyo laki, issue sio nauli, there is more to it that what is visibly seen.

Thanks for concern.
 
.......Yule mama ubongo wake haupo sawa, ni msafi kweli yeye na watoto but has something wrong with her brain.
Kuna organization fulani ina deal na watoto wa mitaani, hiyo organization ilitaka kuwachukua wale watoto cha ajabu hakukubali watoto wachukuliwe, alikataa kata kata.
 
.......Yule mama ubongo wake haupo sawa, ni msafi kweli yeye na watoto but has something wrong with her brain.
Kuna organization fulani ina deal na watoto wa mitaani, hiyo organization ilitaka kuwachukua wale watoto cha ajabu hakukubali watoto wachukuliwe, alikataa kata kata.
Watoto anawafanya mtaji wa symphathy.
 
Back
Top Bottom