Kuna Mlipuko wa Homa na Mafua makali jijini Dar

Kuna Mlipuko wa Homa na Mafua makali jijini Dar

Ndugu zangu Watanzania,

Mimi nipo kwenye sekta ya afya.

Kwa wiki tatu sasa kuanzia katikati ya November 2020 kumekuwa na mlipuko wa homa kali na mafua makali ambayo huambatana na kikohozi.

Kwa takwimu ndogo niliyochukua kutoka vituo mbalimbali vya afya ni kuwa kuna ongezeko la wagonjwa wa

1. Homa kali
2. Maumivu ya kichwa
3. Mafua makali
4. Mafindofindo

Ni wazi kuwa tunapitia katika kipindi kigumu cha magonjwa haya.

Wengi wa wagonjwa hupona katika kipindi cha siku nne mpaka 7.

Mmejiuliza pia sababu ya mlipuko huu?

Wagonjwa wengi wamepimwa malaria lakini hawana malaria.

Hivyo madaktari wengi wamewapa dawa za homa na kikohozi.

Hali ikoje huko kwenu?
Nilidhani ni bia yangu ya baridi kumbe ni kweli maana hizo dalili zote ninazo na mpaka sasa siko poa
 
Hata kama ni uzi wa mwaka jana nataka kuamini hali hiyo ipo! Hata mimi kwa muda wa siku nne hivi zilizopita nimekumbana na hali hiyo. Lakini hali hiyo ina dissolve taratibu and I am Ok.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi nipo kwenye sekta ya afya.

Kwa wiki tatu sasa kuanzia katikati ya November 2020 kumekuwa na mlipuko wa homa kali na mafua makali ambayo huambatana na kikohozi.

Kwa takwimu ndogo niliyochukua kutoka vituo mbalimbali vya afya ni kuwa kuna ongezeko la wagonjwa wa

1. Homa kali
2. Maumivu ya kichwa
3. Mafua makali
4. Mafindofindo

Ni wazi kuwa tunapitia katika kipindi kigumu cha magonjwa haya.

Wengi wa wagonjwa hupona katika kipindi cha siku nne mpaka 7.

Mmejiuliza pia sababu ya mlipuko huu?

Wagonjwa wengi wamepimwa malaria lakini hawana malaria.

Hivyo madaktari wengi wamewapa dawa za homa na kikohozi.

Hali ikoje huko kwenu?
Ni kweli Mkuu ,Ndugu zangu wanne wanaumwa mafua,homa kali,mimi tu ni mbishi kwasababu huwa nafanya mazoezi na kutafuna tangawizi kwa sana ndio maana hayajanikumba,yalianza nikaweza kuyacontrol.

Jana nimepanda na mtu kwenye daladala yaani ni kupiga michafya,mafua kama yote!! Ni kweli Mkuu usemayo.
 
Lini katika nchi hii mafua na kikohozo vilisumbua wachache? Tuwe objective

Mie naongea kwa hali ilivyo sasa hivi, unapoambiwa wimbi ni idadi kubwa ya watu kuwa na homa, mafua na kikohozi.

Hauoni ushuhuda wa raia wanaokwambia wanapitia hiyo hali sasa hivi?

Kwangu ukiachilia mimi, familia nzima wanamafua na kikohozi.
 
Binafsi huwa siugui mafua hivyo ila yamenipata kiasi kwamba najisikia mgonjwa kama malaria.

Nimekunywa dawa na si kawaida yangu,sasa najisikia nafuu.
 
Back
Top Bottom