Kuna mjane ateseka, naomba ushauri wa namna ya kumsaidia

drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
4,664
4,764
Kuna mama mmoja anaitwa Aisha aliolewa na Mtanzania mwenye asili ya Kioman mwaka 1979 huyu Aisha aliwakuta watoto 4 kwa huyu mumewewakiwa na umri miaka 6 wengine miaka 5 yaani bado wadogo waliozaliwa kwa wanawake wengine walioachwa.

Huyu Aisha alipoolewa aliwalea watoto hao kama watoto wake na yeye aisha alibahatika kupata watoto 6 aisha aliwalea watoto vizri sana kwa miaka mingi akiwa na mumewe wakaweza kujenga nyumba nyingi mwaka 1990 mzee akawapeleka watoto wake Oman kusomea huko.

Yeye akabaki mwanza kuishi na mkewe Aisha. Mwaka jana 2020 mzee akaugua ugonjwa ikabidi waenda yeye na mkewe Oman akatibiwe bahati mbaya mzee akafariki wakamzika Oman baada ya kuzika wale watoto wa kambo walishakuwa wakubwa na wanafanya kazi walipanda ndege na kuja kuiba hati zote za nyumba kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Aisha na mumewe.

Watoto wa Aisha waliposikia hivyo na wao wakapanda ndege wakarudi kutoka Oman kuwafuata ndugu zao wa kambo walioiba hizo hati wakashtakiana polisi wakapelekana mahakamani kugawiwa urithi. Tatizo mahakamani watoto wa kambo wana pesa wanahonga huyu mama anasumbuliwa sana na mara nyingine watoto wa kambo wanakwenda kumfanyia fujo nyumbani kwa aisha halafu wakiisha mfanyia fujo wanaenda polisi wanamfungulia mashtaka Aisha.

Hela zao ndio zinazomtesa Aisha maana wanahonga sana: sasa naomba mwenye kujua namna ya kumsaidia huyu mama asisumbuliwe na watoto wa kambo na apewe haki zake naomba anieeleza hapa afanye nini. Najua kuna waungwana watachangia vizuri na kuna watu watatoa maneno ya ovyo hao mungu atawalipa.
 
Tusubirie wajuzi watakuja kutoa msaada ila daah kuna watu wanateseka
 
mimi nimeeleza kwa ufupi sana ila huyu mama ni mpole sana na atakuja kufa kwa mawazo na hakutegemea watoto aliowalea kama wanae watakuja mgeuka hivi kesho 23/6 atakuwa yupo kituoni wale vijana wanamshitaki
 
mimi nimeeleza kwa ufupi sana ila huyu mama ni mpole sana na atakuja kufa kwa mawazo na hakutegemea watoto aliowalea kama wanae watakuja mgeuka hivi kesho 23/6 atakuwa yupo kituoni wale vijana wanamshitaki
Hao watoto kama walilelewa vizuri halafu wanalipa mabaya , dunia duara lazima yatawarudia muda ni mfupi tu!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Kwa vile nadhani hii ni ndoa ya kiislamu, pia utafute ushauri kwa masheikh maana sharia

Na huko mama ajipange na kukubali matokeo.

Sharia....
 
Back
Top Bottom