Kuna mambo watu hawayaelewi kuhusu Mungu

Kuna mambo watu hawayaelewi kuhusu Mungu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,401
Reaction score
80,089
Kwema Wakuu!

Mods naomba Uzi huu msiupeleke jukwaa la dini, huu ni mjadala mfupi kuhusu MUNGU.

Kwanza kabisa neno "Mungu" ni Cheo na wala sio personal Name Kama wengi wadhaniavyo. Ni Kama vile useme, Rais, Mama, Baba, Mfalme N.k. hivyo watu wanapotaja Mungu wasidhani wamemtaja mhusika Fulani external labda internally wawe wamedhamiria jina la Mungu huyo au sifa zake, mfano mtu anaweza kumtaja Mungu akidhamiria Mungu Aitwaye Yahwe, au aitwaye Allah, au aitwaye Baal, au aitwaye Buddha n.k.
Kutukana Kwa kutumia jina Mungu kimsingi kisheria za kimwili physically mahakamani unaweza usitiliwe hatiani kwani utakuwa na utetezi wa kusema hujataja Jina la Mungu yeyote, labda utaje Mungu na uorodheshe na sifa zake ambazo zinagusa miungu wengine. Hata hivyo pia utaweza kujitetea.

Ingawaje kwenye dhamiri ya ndani utajishtaki mwenyewe na kujihukumu mwenyewe. Ndio maana niliwahi andika hapa kumtetea Afande Selle alivyomtukana Mungu bila kumtaja ni Mungu yupo labda alimzungumzia Jah Nani ajuaye, soma hapa 👉👉https://www.jamiiforums.com/threads/miungu-wapo-wengi-afande-sele-hajataja-mungu-yupi.1850936/

Leo nataka tuzungumze Mungu kama Cheo na jina hilohilo tulitumie Kama Personal name, kumrejelea Mungu Mkuu, muweza wa yote, muumba wa vilivyomo na visivyokuwemo.

Wale wanaosema Mungu hayupo wanaweza kuwa sahihi Kwa sababu uwezo wao wa kufikiri hauna uwezo wa kuona uwepo wa Mungu wa Aina yeyote.

Katika mamlaka na utawala kuna muundo kutoka juu mpaka chini Kabisa, hivyo hivyo katika Mungu,
Mungu aligawanya uungu kuanzia Wakuu kabisa ambaye ni yeye mpaka chini Kabisa ambaye hana uungu(yaani mwenye nguvu ya uungu hafifu).

Mwanadamu ni sehemu tuu ya uungu wa Mungu ingawaje wapo viumbe wengine wenye uungu wa Mungu kama Malaika, Majini, maserafi, makerubi na viumbe wengine ambao wanasifa za kiungu.

Sifa za kiungu ni Kama ifuatavyo;
1. Utawala na mamlaka ambao lazima uwe na nguvu na uwezo(uweza hi wa Mungu Mkuu)

2. Kuunda na kutengeneza, ( Kwa Mungu ni kuumba, yaani kufanya Jambo jipya pasipo kutumia kilichopo)
Mungu Mkuu huwapa viumbe uwezo wa kubuni na kuunda vitu ili viwasaidie na kuwarahisishia maisha, wanatumia vitu vilivyopo,

Kuwa na sifa hizo haIkufanyi kuwa Mungu Mkuu isipokuwa mungu kiumbe ambaye utaitwa upo kundi la miungu, na hapo ndipo unapopewa Jina Kama vile miungu iliyopo tunayoiabudu.

Mungu MUWEZA anasifa zifuatazo;
1. Hana mwanzo wala mwisho kumaanisha hakuzaa wala hakuzaliwa
2. Hana jina isipokuwa Cheo chake ni Mungu.
Hujipatia majina yake kupitia miungu wadogo aliowapa uwezo, na hilo sio kosa isipokuwa kuwaabudu miungu hiyo.
3. Hakosei wala hapatii, yaani hayuko sahihi wala hana makosa.
Ila hupata usahihi Kwa miungu aliyoiweka na hupata makosa Kwa miungu aliyoiweka.
Makosa hayo ipo Kwa miungu ya uharibifu ambayo wengi huiita mashetani. Zingatia Shetani naye ni mungu kwani anasifa za miungu.

4. Hafurahi wala hachukii na huwezi kumfurahisha wala kumchukiza Kwa sababu wewe ni kiumbe tuu, isipokuwa atafurahi kupitia miungu aliyoiweka na atachukia kupitia miungu aliyoiweka.

Zingatia, kila mwanadamu na kiumbe kina mwanzo huo mwanzo ndio mungu wako ingawaje sio MUNGU Mkuu!
Mfano, Baba yako na Mama yako ni mungu wako ingawaje sio MUNGU Muweza,
Mama na Baba yako huchukia na kufurahi ukifanya mazuri au mabaya,
Lakini hiyo haimaanishi Mungu MUWEZA atachukia au atafurahi unapofanya lolote kwa wazazi wako(miungu yako ya kimwili).

Katika Falme za kiroho wako Wazazi au miungu iliyowekwa ajili yako, hiyo wengi ndio hudhani ni MUNGU MKUU muumba wa mbingu na Nchi, mfano Yahweh! Ni mungu wa Wayahudi hivyo anasifa nyingi za kibinadamu Kama kuchukia, kufurahi, Kupenda na kupendelea n.k. ilhali Mungu Mkuu hawezi kuwa na sifa hizo.

Yaani Mungu MUWEZA Hana uhitaji wa lolote toka Kwa viumbe wake, hafanyi Kwa maslahi ya yeyote Yule.

Hauwi wala hatoi uzima, Ila aliweka Uhai na kifo Kwa viumbe wake.
Wapo viumbe wenye uwezo wa kutoa Uhai na wapo wenye uwezo wa kutoa mauti.

Huwezi kumuomba Mungu Mkuu kwani utakuwa umevunja Itifaki ya muundo wa kiungu
Mtoto mdogo hawezi kuacha kumuomba Mama Kipande cha andazi akamuomba Mungu kipande cha andazi, hiyo haipo.

Mungu MUWEZA aliweka mamlaka yake Kwa viumbe wake kulingana na sifa zao. Mwanadamu alikabidhiwa Dunia awe ndiye mungu wa dunia, aitawale na kuitunza, katika mfumo unaofuata huyo aliyemkabidhi mwanadamu naye amekabidhiwa eneo Fulani la kimamlaka labda Nyota ya Jua na Sayari zake ndio awe mungu kwazo, ambao Wakristo huamini ni Yesu ambaye ndiye wanamuomba, Yesu Naye anawajuu yake ambaye alimkabidhi, sio ajabu Galaxy yetu ambayo ni kundi la Nyota zipatazo mamilioni zina mungu wake aliyepewa atawale hivyohivyo mpaka Afikiwe Mungu MUWEZA sio leo wala sio kesho.
Kama nilivyoeleza huwezi kumuomba Mungu Mkuu MUWEZA WA yote ukavunja itifaki yote mpaka juu.
Ingawaje unatakiwa kumuabudu,

Ni Kama uwe unamwomba mzazi wako pesa hiyo haimaanishi Ndio umuabudu.

mungu wa kwenye Biblia aitwaye Yahweh, alivyomuumba Adamu Kama mungu mdogo WA kumsaidia kuitawala Dunia na kuitunza kisha akamuumba mungu mke Msaidizi wa Adamu alimpa masharti ambayo adamu aliyatengua, kutengua masharti ya mungu ni kujitoa kwenye mfumo, ndio maana mungu alipofika Edeni akawa hamuoni Adamu sio kwamba hajui yupo wapi Ila hamuoni kwenye mfumo wake wa kiungu.

Ni Sawa na Mwanafunzi aliyefukuzwa Chuo au mtumishi aliyefukuzwa utumishi, mfumo haumtambui.

Huwezi muelewa MUNGU MKUU muumba wa mbingu na Nchi Kama hujui Itifaki ya utawala na mamlaka.

Watu wengi wanalumbana Sana Kuhusu Mungu Kwa sababu wanamiungu tofauti wanayotaka ifanye kazi Sawa zinazofanana, ni Sawa na wazazi wetu ni tofauti alafu mtu aseme ni mmoja.

Yaani Baba yangu mzazi alafu mtu mwingine amlinganishe na Baba yake mzazi Jambo ambalo hata kama wote ni Baba lakini lazima yapo mambo watatofautiana.

miungu tunayoiabudu inamapungufu Yao katika level za miungu na ndio maana wengi wanamjaji Mungu Mkuu Kwa kuwatumia miungu wanayoiabudu wakiona Mungu anaupendeleo wakati kimsingi MUNGU MKUU muumba wa mbingu na Nchi Hana upendeleo.

Upendeleo utapewa na miungu yako, Inategemea na ushapu WA miungu unayoiabudu.
Ni Kama vile wazazi wetu, wapo walioshapu kuwatafutia fursa watoto wao na kuwaachia Urithi na wapo wazazi waluozubaa zubaa na wanaoendekeza tamaa zao wenyewe.
Wazazi wako ndio watakupendelea lakini sio Mungu.

Nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon Master
Arusha
 
Hizi ni sifa mpya nazisikia za Mungu ambazo sijawahi kuzisikia popote pale

"Mungu ambaye hapatii" hii ni sifa ambayo naiweka juu ya hizo zingine

Mungu haitaji lolote kutoka kwa watu lakini bado anasisitiza umuabudu

Hafurahi wala hachukii lakini kupitia hiyo story ya eden tunaona hasira yake kwa kuwatimua kina adam

Akaleta na gharika kuua kila mtu na kubakisha familia ya watu 8 tu, lakini bado haikutosha kukata hasira zake mpaka alipoamua kuja na comeback ya kuangamiza watu kwa moto

Hii hukumu ya moto aliyoitoa hata yeye alijilaumu na kujiapiza hatakuja kufanya maamuzi kama hayo tena. Lakini alivyo mnafki bado anaendelea kuset moto huko wa jehanam
 
Scars huwa unamchukulia Mungu kama ni jamaa fulani hivi anayepangiwa cha kufanya.

Yeye kaumba kila kitu na anao uhuru wa kuamua atakavyo.
 
MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU.
 
Hizi ni sifa mpya nazisikia za Mungu ambazo sijawahi kuzisikia popote pale

"Mungu ambaye hapatii" hii ni sifa ambayo naiweka juu ya hizo zingine

Mungu haitaji lolote kutoka kwa watu lakini bado anasisitiza umuabudu

Hafurahi wala hachukii lakini kupitia hiyo story ya eden tunaona hasira yake kwa kuwatimua kina adam

Akaleta na gharika kuua kila mtu na kubakisha familia ya watu 8 tu, lakini bado haikutosha kukata hasira zake mpaka alipoamua kuja na comeback ya kuangamiza watu kwa moto

Hii hukumu ya moto aliyoitoa hata yeye alijilaumu na kujiapiza hatakuja kufanya maamuzi kama hayo tena. Lakini alivyo mnafki bado anaendelea kuset moto huko wa jehanam

Soma Uelewa Mada, huyo aliyetoa mambo ya Moto ni Yahweh na sio Mungu Mkuu MUWEZA WA yote.
Kila mungu anaadhabu zakw Kutokana na utashi wake na hasira zake.

Nishakuambia Mungu MUWEZA WA yote Hana anachohitaji kutoka Kwa viumbe wake.

Ukitenda kosa Kwa mzazi wako mfano kudokoa mboga labda ni nyama na Mimi nikafanya vivyohivyo Kwa mzazi wangu wote ni wazazi lakini adhabu zitakuwa tofauti.
 
Ni kweli kabisa,shida yetu tunamwabudu Mungu ambae hatuhusu sisi .Kila jamii na Kila kabila Lina Mungu wake upo sahihi
 
Soma Uelewa Mada, huyo aliyetoa mambo ya Moto ni Yahweh na sio Mungu Mkuu MUWEZA WA yote.
Kila mungu anaadhabu zakw Kutokana na utashi wake na hasira zake.

Nishakuambia Mungu MUWEZA WA yote Hana anachohitaji kutoka Kwa viumbe wake.

Ukitenda kosa Kwa mzazi wako mfano kudokoa mboga labda ni nyama na Mimi nikafanya vivyohivyo Kwa mzazi wangu wote ni wazazi lakini adhabu zitakuwa tofauti.
Kwa hiyo huyu Mungu muweza wa yote yeye anaitwa nani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom