Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,217
- 1,706
Yer 2:28 SUV
[28] Lakini wako wapi miungu yako ulioifanya? Na wasimame hao, kama wakiweza kukuokoa wakati wa taabu yako; kwa maana hesabu ya miungu yako ni sawasawa na hesabu ya miji yako, Ee Yuda.
Ulizo hili la Mungu ni la kejeli kwa Yuda, kwa sababu walimwacha Mungu na kugeukia miungu mingine, jambo ambalo lilikuwa chukizo kwa Mungu wao.
Mungu kuwauliza "Wako wapi miungu yako uliyoifanya? " Inaonyesha miungu yao haikuwasaidia katika mapito yao, walifikiri miungu waliyoitengeneza itakuwa msaada wao, ila haikuwa hivyo ndio maana Mungu anawauliza swali hili la kejeli.
Tunaweza kufika mahali tukaacha kumtegemea Mungu na kugeukia miungu mingine, miungu ambayo ni kazi ya mikono ya mwanadamu, yaani unajitengenezea sanamu au mnatengeneza sanamu alafu mnaanza kuiabudu.
Tunashindwa kuelewa miungu hiyo haiwezi kujibu mahitaji yetu, haiwezi kuokoa, na haiwezi kusaidia shida ngumu zinazotukabili katika maisha yetu.
Tuelewe hakuna mungu mwingine kama Yehova, na wokovu wetu haukuletwa na miungu ya kuchongwa au ya mababu zetu, wokovu ulipatikana kwa Yesu Kristo peke yake.
Kugeukia miungu mingine ni kujiletea laana pasipo sababu, tunapaswa kujiweka mbali na ibada za sanamu, au kutegemea miungu mingine huku tunasema tumeokoka.
Ukimwamini Yesu sawasawa, umejihakikishia usalama wa maisha yako, muhimu kwako ni kuendelea kukua kiroho, kuhakikisha neno la Mungu linajaa moyoni mwako na kujua haki zako, na yale Mungu hataki ufanye.
Ukishamwelewa Mungu kupitia neno lake, hautakuwa na tamaa ya kugeukia miungu mingine kutafuta msaada, unajua unaye Mungu mwenye uwezo wa kufanya chochote kwa wakati wowote.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana