Kuna madhara gani kumpeleka mtoto kusoma Uganda?

MfalmewaKiha

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
1,191
1,233
Habari zenu watu wa Mungu,
Poleni Kwa majukum ya kila siku

Leo ninahitaji msaada wenu wana Ndugu, jamaa, na marafiki

Nina rafiki yangu wa karibu anataka ananiomba ushauri kuhusu kumpeleka mtoto wake kwenda kusomea Kampala Uganda, Kwa sasa mtoto wake yuko darasa la pili St Kayumba hapa Tanzania,
Ila kaniomba ushauri hasa anataka kujua madhara ya mtoto wa kitanzania kwenda kusomea nchi jirani (English Medium)
Je Kwa baadae kibongo bongo haina madhara?
Hayo Ndio maswali yake,

Nimeamua niwashilikishe maana hata Mimi sina uzoefu wa jambo km hilo.

Nb:sio lazima utumie maneno ya kebehi, ninacho omba ni ushauri tu.
received_911694485652677.jpeg
received_911694295652696.jpeg
 
Kama ana ndugu Kampala sio mbaya ila kama hana ndugu huyo bado mtoto sana subiri angalau afike darasa la tano ndio umpeleke all in all shule zao ni nzuri lakini care ya mwanafunzi hapo tunawazidi.
 
Kama ana ndugu Kampala sio mbaya ila kama hana ndugu huyo bado mtoto sana subiri angalau afike darasa la tano ndio umpeleke all in all shule zao ni nzuri lakini care ya mwanafunzi hapo tunawazidi.
Huyo mwenye mtoto, Ana mtu huko wanae fahamiana.
 
Huyo mwenye mtoto, Ana mtu huko wanae fahamiana.
Kama ni hivyo hamna shida ampeleke tu sizijui sana shule zao za primary nafahamu za sekondari maana nilisoma huko anyway elimu ya kule ni nzuri Hasa kwenye maswala ya lugha Kingereza wapo vizuri sana akitoka huko anakua very competent na kwa kuwa ni mdogo bora awe anatumia fast jet kwenda nae mpaka Entebbe halafu anaingia Kampala.
 
Mtoto wa darasa la pili... Umpeleke boarding nje ya nchi? Hivi hawa Watoto mnawatafutaga kwa kujipinda kweli au mnasingiziwa?
Lengo la uzi ni kuomba ushauri,
Hebu sema bording inatakiwa mtoto wa Darasa la ngapi?
 
by experience yakuishi na kusoma Kampala c nzuri kwa hawa watoto wasiojielewa kiukweli na trust me wana shule nyingi nzuri za boarding but hazina quality na wale wakina ssengaa(matron) wanalemewaga kuna zile very expensive kama st marys ndo nzuri otherwise ajikaze fees ampeleke Nairobi kama zakwetu hazitaki kabisa au ampeleke secondary
 
Nyinyi ndio mnaotutengenezea kizazi kilichoshindikana!

Mtoto wa darasa la pili hatakiwi hata kuishi kwa ndugu (kama wazazi wapo). Anatakiwa awe chini ya uangalizi wa wazazi ili kuhakikisha anakulia kwenye maadili.

Kuna athari kubwa sana kumuacha mwanao mdogo wa umri huo alelewe na kukulia kwenye uangalizi wa watu wengine!

By the way, huyo jamaa anaishi wapi hapa Tanzania ambapo hakuna shule za English medium?

Mbona anahangaika na vitu visivyokua na umuhimu wala ulazima?

Mwambie amtafutie shule hapa hapa Tanzania, tena asimuweke boarding. Ni hatari sana kwa umri huo!
 
Elimu bora iko ndani ya nchi yetu..wengi ya wazaz wanazan kupeleka mtoto nje ni bora zaid..wangap washasoma nje ya nchi na wamebaki kuwa mbulula hadi leo?

Nimesoma shule zetu za kawaida tu leo hii niko nakula bata out of the country na kizungu nakipolomosha kama kijaluo

.....
 
Nyinyi ndio mnaotutengenezea kizazi kilichoshindikana!

Mtoto wa darasa la pili hatakiwi hata kuishi kwa ndugu (kama wazazi wapo). Anatakiwa awe chini ya uangalizi wa wazazi ili kuhakikisha anakulia kwenye maadili.

Kuna athari kubwa sana kumuacha mwanao mdogo wa umri huo alelewe na kukulia kwenye uangalizi wa watu wengine!

By the way, huyo jamaa anaishi wapi hapa Tanzania ambapo hakuna shule za English medium?

Mbona anahangaika na vitu visivyokua na umuhimu wala ulazima?

Mwambie amtafutie shule hapa hapa Tanzania, tena asimuweke boarding. Ni hatari sana kwa umri huo!
Umesema vyema kabisa. Naongezea hivi: Wazazi waache ulimbukeni ama kutafuta sifa za kijinga Mwanangu anasoma Uganda , kwa umri huo mtoto anapaswa asome shule ya kutwa tena hapa hapa nyumbani. Boarding aende atleast akiwa form one/two.
 
They amount to nothing nawajua wengi, wanarudi na maadili mabovu kuna shule nzuri tu hapa tz
 
Sina ushauri, ila nakupa pole wewe Mzazi/Mlezi na huyo mwanafunzi (mtoto wa std 2)

Naona wazi unapingana na ushauri unaopewa na Wadau (japo ni wewe uliye omba ushauri)

Mtoto ni wenu na maamuzi yako mikononi mwenu.

Nawasilisha..
 
Tanzania kuna shule nzuri nyingi sana za English medium, unaweza hata kuchek kwenye matokeo yao yao ya darasa la 7 kwenye mtandao wa NECTA hapo utachagua best school unayoihitaji kwa wilaya , mkoa husika au kitaifa.
 
Ni hatari, watoto waliosoma huko ninaowafamu wameribika kimaadili kabisa.
Yeah! Hata mimi wapo watoto wa ndugu yangu waliharibikia huko. Wa kike aligeuka malaya hatari, na wakiume bangi. Nilipofuatilia nikagundua ni asilimia chache wanapona kupata madhara hayo. Lakini walio wengi wanaharibika.
 
Back
Top Bottom