Kubemenda mtoto kuna madhara gani? Mbona kunaogopwa sana?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,200
12,691
Katika tafakari yangu nimegundua kuwa kubemenda mtoto hakuna madhara yoyote. Kubemenda ikiwa ni kuzaa watoto karibukaribu kupita kiasi, huyu hajamaliza kunyonya tayari mwingine kazaliwa. Zamani jambo hili liliweza kusababisha kwashiarkor kwa watoto.

Hata Kwashiarkor maana yake ugonjwa unaompata mtoto baada ya mtoto mwingine kuzaliwa, lakini watu wa zamani hawakujua kuwa kwashiarkor ni tatizo la lishe. Sasa, mbali na hiyo shida, kubemenda kuna madhara gani mengine hadi kuogopwe sana? Maana Huko Mtwara kuna kijana juzi kati alimuua mzee wake baada ya kuzuia asije kubemenda.
 
Back
Top Bottom