Kavimbe jr
Member
- May 9, 2023
- 63
- 94
Miaka 7 iliyopita nilinunua kiwanja cha SQm 400 hivi maeneo ya Sahwa.
Kutokana na uwezo wangu mdogo tukashauriana na wife tujenge nyumba ndogo kwanza ya vyumba viwili na sebule baadaye tukitulia ndio tujenge nyumba ya nafasi.
Kweli nilifanikiwa kujenga nyumba ndogo na nikaunga umeme pia na maji.
Kodi ya majengo ilikuwa tayari imo katika mfumo wa umeme. Kama kawaida ninalipa kodi kupitia manunuzi ya umeme.
Baada ya miaka nikafanikiwa kujenga nyumba kubwa ya familia iliyoshikana na ile nyumba ndogo.
Sasa nikawa napokea meseji za TAMISEMI zenye control namba kunitaka nilipie kodi ya jengo.. nikawa ninashangaa kwa sababu tayari ninalipa katika umeme.
Siku hiyo nitakutumiwa control namba na mtendaji kata kunitaka nilipie jengo langu. Nikampigia na kumwambia mimi ninalipa kodi ya jengo kupitia umeme. Mtendaji akanijibu hapo kwako una nyumba mbili unayolipia ni moja katika umeme na moja nyengine haina mita ya umeme, kwa hiyo unatakiwa kulipia kupitia control namba.
Kwa kweli sikumuelewa.. nikamwambia mimi mwenyewe ninajua nina nyumba moja siwezi kujitapa nina nyumba mbili hapa.
Akaniambia wao wanahesabu majengo, kama katika kiwanja chako kuna majengo manne basi ni nyumba nne hizo na unatakiwa zote uzilipie kodi ingawa zipo katika kiwanja kimoja.