Kuna kila dalili za Prof. Lipumba kuwa Waziri wa Magufuli

Ubunge wa kuteuliwa anaweza kuupata ila uwaziri asahau kwan katiba hairuhusu labda awe mwanachama wa ccm
 
magufuli weka siasa pembeni tumia majembe kama lipumba,mimi ni mpinzani ila kwa magufuli SHIKAMOO,nilikunyima kura yangu mpaka sasa nahisi niliipoteza.muhimu mukulu tupa mbali dogo jembe na prince kwenye baraza lako,tunasubiri suprise kama ya waziri mkuu
 
Ili uwe waziri unapaswa kuwa mbunge...akiteuliwa hawezi kuwa mbunge mpaka akiapishwa bungeni mkutano ujao unless wafanye uvunjaji wa sheria kama alivyofanya JK...kuwaapisha uwaziri kina Mkuya kabla ya kuapa ubunge

Kumbe unawezekana? Sasa unapinga nini?
 
Ndugu wana JF
Prof. Lipumba ni mmoja wa wamchumi nguli waliowahi kutokea nchini. Huyu bwana mbali tuu na kujivua uenyekiti wa chama chake cha CUF katika kipindi ambacho walikuwa wanamhitaji sana, lakini yeye amemkubali Rais JPM kuwa rais halali tofauti na msimamo wa chama chake ambacho kinaunda UKAWA.

Lakini hivi juzi alienda mbali mpaka kwenda Ikulu kumpongeza rais JPM. Kana kwamba haitoshi, mahakama imemfutia kesi yake na wafuasi wote alioshitakiwa nao kisa eti DPP kaamua kutoendelea na hiyo kesi. Hapo kuna maswali mengi ya kujiuliza???

Lakini vilevile Lipumba mara nyingi amekuwa na maoni chanya Kwa rais na CCM hali yeye mpinzani. Na yeye anajinasibu kuwa anapinga ufisadi na kitendo cha lowasa kwenda ukawa ni sawa na kumkaribisha fisadi.

Na JPM anasema hana ubia na mtu yeyote kwenye urais wake na kuna kila dalili za mawaziri kibao wa serikali iliyopita kupigwa chini kutokana na sifa ya utendaji mbaya. JPM haishiwi surprise na kutekeleza kile anachokiamini. Sasa je hizi si dalili za Prof Lipumba kuukwaa ubunge wa kuteuliwa na baadaye uwaziri wa serikali ya JPM???

Ni mtizamo wangu tuu
Mkuu,
1.IN RED
-Sio kweli kwamba mara nyingi amekuwa na maoni chanya juu ya CCM Mkuu usipotoshe umma,Lipumba has spent years criticising CCM
-Hakukuwa na Ubaya kujiuzulu kwa kukataa kuwa pamoja na Lowasa koz aliamini ni Fisadi na ametumia muda mwingi kuwaaminisha watu hivo
2.Weka Taifa mbele angalau kwa maramoja tu,kuna Ubaya gani kwa Lipumba kuwa waziri kama JPM atamuona He is the most qualified kwa ile chansi anayotaka kumpa?
 
Hapo ndipo atapokula malipo ya "kujivua uenyekiti wa CUF"
kwani alifanya maamuzi magumu na makini sana.
 
Mtazamo Wangu,
1.Ukiweka ushabiki wa kivyama pembeni Prof.Lipumba ni Hazina kwa taifa hili.
2.Kwa muda mfupi nimegundua JPM sio mwanasiasa hana Blah Blah na inaonekana ana nia ya dhati ya kutupeleka in a Promised Land,hivo akimteua Lipumba naamini kuna kitu amekiona anataka kishughulikiwe
 
Naomba sana amuweke kwenye a more technical position kuliko uwazir ugavana hv au hata akampa shirika moja kati ya haya ambayo yanalegalega
 
Lipumba huyu huyu aliyekua anahamasisha waislamu misikitini!!
Lipumba ni mchumia tumbo hafai kabisaaaaaa
Hana uzalendo wowote kwa taifa, yuko radhi kuhamasisha machafuko kwa tamaa yake ya madaraka, Lipumba hafai hata kwa kulumangia
 
Lipumba huyu huyu aliyekua anahamasisha waislamu misikitini!!
Lipumba ni mchumia tumbo hafai kabisaaaaaa
Hana uzalendo wowote kwa taifa, yuko radhi kuhamasisha machafuko kwa tamaa yake ya madaraka, Lipumba hafai hata kwa kulumangia

Hata Lukuvi naye alihamasisha watu makanisani! Lakini aliendelea kufaa kuwapo kwenye baraza la mawaziri lililopita!

Achaguliwe Sheikh au Mchungaji katika serikali ya Magufuli, watanzania tunachokitaka ni maendeleo ya nchi yetu, kwa maana kwamba hachaguliwi mtu au haachi kuchaguliwa mtu kwa ajili ya dini yake as long as anaweza!

Kuwa upinzani, siyo kukosa uzalendo au kuwa muhaini bali ni mawazo mbadala wa kinachoendelea serikalini. Na upinzani ukiwa dhaifu, lazima chama tawala kijisahau....hata Joti anaweza agombee urais na akapewa! Upinzani upo pia kwa mjibu wa sharia!

Chochote alichokuwa akikifanya Lipumba, ilikuwa ni kutokana na maamuzi au makubaliano ya alipokuwapo!
 
kuna kila dalili za Prof Lipumba kupata nafasi ya kumsaidia Mhe Rais katika awamu hii serikali ya awamu ya tano katika nafasi ambayo Rais ataona inamfaa.kwanini natabiri hilo sababu
1.Prof kaenda kuongea na Mhe Rais.
2.Prof kafutiwa kesi ambayo ilipaswa kutajwa 15/01/2016
3.Prof alikuwa anazungumza kwenye kituo cha TV TBC1 "live" 03/12/2015.
Sii kawaida mambo haya kufanywa kwa mtu ambaye si mwanachama wa chama tawala.
 
Nakubaliana na hoja.Hata mimi nina amini kuwa Lipumba atapewa kazi hata kama siyo hiyo ya Ubunge na hatimaye Uwaziri.Ukiacha tofauti zetu za kichama Lipumba ni mbobezi wa Uchumi.Nawasilisha.

Dr Slaa sio kamawanavyomfikiria team lowasa yule ni msomi pia amekuwa mshauri wa uchumi katika mataifa mbalimbali apa Africa na ulaya msimfananishe kabisa na we ye digrii za kibongo
 
Wala hatuhitaji wasomi wa design ya Prof nchi hii. Hao wasomi ndio waliopo TRA, MNH, TRL, TPA nk... Ndio wanaotupiga dili kila siku.

Prof alipokuwa Mkiti CUF haikuwahi kupata wabunge wengi Bara mpaka alivyoondoka mwaka huu ndio angalau CUF wameng'ara. Sasa kuendelea kumuamini Huyu msomi ni sawa na kusubiria muujiza.

prof. Ndo aliefanya watu wasilinde kura? Wasiuze ushindi?
 
Back
Top Bottom