Kuna kazi zinaweza kukutenganisha na familia au kutokuweka kwenye maamuzi kama wengine

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,722
Dunia kila mtu kazaliwa kubeba jukumu la mwingine kwenye kazi.

Ila kuna kazi haijalishi zenye pesa au zisizo na pesa ila zinaweza kukufanya hata kutokuwa na familia au kuwa na familia uliyoacha pili kutokufanya maamuzi.

Mfano wa kazi:

* Ubaharia
Hii kazi wanapoteza muda mwingi wa maisha na kuishia wakijisifu sijui nimetembea kote, nimeacha familia huko.

* Polisi, askari magereza, walimu
Nawaonea huruma sana hawa watumishi kwenye hizo idara. Kama ndio sio mjanja unaweza kuishia maishani mwako unachezeshwa vituo vya kazi kama mwanasesele.

*vibarua visiyo na mipaka
Asilimia kubwa ni wale wanatanga tanga leo yupo nchi hii kesho yupo nchi fulani. Muda mwingine wanaishia na story.

* Wachimbaji madini wadogo
katika watu wanaongoza kujipa moyo ni wachimbaji na tena muda mwingi wanakuwa maporini ndani ndani.

Je, wengine wakina nani?
 
marine captain au technicians tu katika meli zinazokwenda mbali siyo siri ni kazi ambayo nilitokea kuikubali mno japo sijafanikiwa kuifanya ila nilikuja kupata nyingine haina utofauti sana, kuna raha yake mzee.
 
Tukiwa hatunakazi mnatunanga mnatuita jobless tumepoteza dira,,,

Tukiwa nazo tena masimango/hazifai ,,,,

Tufanyeje na sisi tuwe walamba asali ?
 
Nyingine ni kazi ya kubeti. Hawa watu kila siku utasikia, isingekuwa timu moja kuchana mkeka muda huu ningekuwa nimeshausahau umasikini.

Uwezekano wa kuwa tajiri ghafla na muda mwingine kukaribia sana kushinda, pamoja na kusikia matangazo ya wenzao walioshinda, wengi hujikuta wanapoteza muda mwingi na pesa mpaka wanazeeka.
 
Hapo kwa walimu toa ....

Mwalimu unakut anafamilia yake kabisa ,anatoka shule mapema saa Tisa jion ,anakutana n familia ,anajumuika na wanajamii Kama Ni kanisani n.k
 
Polisi ,wanajeshii...

Hizi kazi unakuja kuenjoy na familia siku ukistafu ......

Vinginevyo Ni kufuata amri na maelekezo kutoka juu kushinda kwenye malindo na bunduki ,misituni ,mipakani ,kambini ,muda wote huwezi jumuika na wanajamii katika shughuli mbalimbali kabisa huo muda hupati
 
Kazi nyingi bongo ni za namna hiyo bora watu wanakosa mda wa kukaa na ndugu na familia kisa majukumu ila muhimu mkono uende kinywani
 
Back
Top Bottom