Kuna Jambo Pesa haiwezi kununua

Munyaluganda

Member
Jul 13, 2022
7
21

Wanadamu wengi tumerithi kwa walezi wetu fikra isemayo kwamba ukiwa na pesa unaweza kununua chochote ukipendacho kwa sababu tulishuhudia kumuona tajiri wa mtaa akisumbua atakavyo wakati tulipokuwa wadogo ila wengi hatukufundishwa kutambua kuwa ndoa ni ya mtu bali msiba ni wa watu.

Ndoa ni taasisi ya Amani inayofanya kazi kama taasisi zingine ila utofauti wake ni kwamba. Taasisi zingine husajiliwa na BRELA ila taasisi ya ndoa huitaji mashahidi, wadhamini na kupewa cheti tu.

Taasisi hii hailipi posho kabisa ndio maana mamluki wengi hushindwa kuvumilia.

Kati ya ndoa zilizowahi kufungwa kwa maneno mengi tena ya kebehi ni hii kati ya Nandy na Billnass. Watu wengi walimuhukumu Nandy kutokana na maisha yake ya kisanii ila Billnass ametuachia ujumbe mzito hapo. Vijana wengi hutafuta kuoa wanawake wenye hofu ya Mungu wakati wao wenyewe mambo mengi.

Ndege wanaofanana ndio huruka pamoja. Rafiki yangu chukua hii, hivi unafikiri ni kwanini mapepo hulipuka kwenye nyumba za ibada. Ni salamu tosha kwamba hata makanisani shetani ni wengi huko.

Billnas na Nandy walikutana majukwaani katika kazi yao ya mziki na ndio maana wanapendana sana kwa sababu tabia zao zinafanana. Katika maisha pesa imeshindwa kununua mambo mawili tu; upendo na kurudishia uhai wa mtu tu na huo ndio ukuu wake Mungu. Tatizo Afrika tunawalazimisha watoto wetu kwenda katika nyumba za ibada hata kama mzazi anaona kabisa mtoto ana dalili zote za uwakili na ndio maana tumewatengeneza vibaka wengi huko.

Wanawake zaidi ya 87,000 huuliwa na wanaume zao na wanaume zaidi ya 3,200 huuliwa na wake zao kila mwaka duniani. Hiyo ni dalili kwamba wanandoa wengi huushi kwenye ndoa zisizowahusu. Rafiki dada yangu chukua hii, usikubali kuufata upepo wa pesa katika mahusiano ila ukiwa mkaidi kwa haya maneno yangu ukiliwa kichwa mimi nimesema.

Yule msanii aliyeimba wimbo wake akisema “Utazunguka huku na kule kumbe chaka lako ni hapa” alipaswa kujengewa sanamu tena pale posta ila tabia ya Wabongo huwa tunamtambua mtu akishakufa. Kama ipo ipo tu hata kama itachelewa, hivi unajua Nandy ametembea na wangapi tena wenye pesa zao. Maisha ya mahusiano ni sawa na gari la abilia lenye kufanya safari za mikoani, unaweza ukapanda na mtu tena mkakaa siti moja kumbe yeye anashuka njiani hafiki unakokwenda wewe.

294400299_163388872869135_4338290854797459025_n.jpg


 
Kwa mtazamo wangu, ni uhai pekee ndiyo hauwezi kununulika. Ila upendo kwa hii dunia ya leo, unanunulika kabisa.

Na ndiyo maana hata kwenye lile jukwaa letu pendwa la kutafuta wachumba, moja ya kigezo cha mwanaume anayetakiwa, ni yule mwenye kazi/shughuli ya uhakika ya kumuingizia kipato! Na siyo upendo wa dhati.
 
Pesa ni sabuni ya roho wahenga walisema,
"Ama kweli maradhi yote ugua lakini kuchacha usiombee"
ni uhai na kifo tu ndiyo havinunuliki vingine vina price tags
 
Imebidi niweke kibao cha twanga pepeta MTU PESA, utunzi bora kabisa, moja kti ya kazi nyiingi nzuri za marehemu Ramadhani masanja, BANZA STONE, mwalimu wa walimu
R.I.P legend.

ukiwa na pesa jiandae kupata marafiki wengi wa uongo, kupata mapenzi ya uongo(japo hili si lazima, ila nafasi yake ni kubwa mnoo)
Pesa hainunui furaha ila dada mmoja wa mjini aliniambia bora ulie kwenye range kuliko kulia unaswampa kwa mguu.

PPESA NI MAPITO lakini zinanoga zaidi zikipitia na kwako 😂🤣
 
Kwa mtazamo wangu, ni uhai pekee ndiyo hauwezi kununulika. Ila upendo kwa hii dunia ya leo, unanunulika kabisa.

Na ndiyo maana hata kwenye lile jukwaa letu pendwa la kutafuta wachumba, moja ya kigezo cha mwanaume anayetakiwa, ni yule mwenye kazi/shughuli ya uhakika ya kumuingizia kipato! Na siyo upendo wa dhati.
Naomba jibu lako muungwana.Kati ya kumpa pesa mwanamke ila usioneshe upendo kwake na kuonesha upendo wa dhati kwa mwanamke lakini usimpe pesa ni sababu gani kati ya hizo mbili inaweza kumfanya mwanamke kurudi nyumbani kwao.
 
Naomba jibu lako muungwana.Kati ya kumpa pesa mwanamke ila usioneshe upendo kwake na kuonesha upendo wa dhati kwa mwanamke lakini usimpe pesa ni sababu gani kati ya hizo mbili inaweza kumfanya mwanamke kurudi nyumbani kwao.
Ingekuwa miaka ya zamani, hiyo sababu ya kwanza ingemrudishwa kwao.

Ila dunia ya sasa, nadhani hiyo ya pili kama haitamrudisha kwao, basi itasababisha udharauliwe sana hapo nyumbani kiasi cha kufikia hatua hata ya kumdhuru iwapo utakuwa huna uvumilivu.
 
Back
Top Bottom