TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,514
- 11,277
Kutokana na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa Urais wake, nadiriki kusema kuwa Bwana Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni mwa watanzania wachache sana waliofanikiwa kutimiza ndoto zao. Ni watu wachache sana ambao katika kuishi kwao huweza kutimiza ndoto zao walizojiwekea, huyu Bwana amefanikiwa kwa hilo na tumpe pongezi zake. Kikwete alikuwa na ndoto ya kuwa Rais tu, na si zaidi wala pungufu ya hilo. Na ni Rais wa Tanzania sasa!
Kutokana na aina ya uongozi wake pamoja na kauli zake za mara kwa mara utagundua kwamba Ndugu Kikwete hakuwahi kufikiria kuhusu kuikomboa au kuwakomboa watanzania dhidi ya Umasikini. Hivyo tunaolalamika kila kukicha kwamba ameshindwa kuongoza nchi basi kuna jambo hatuelewi. Kitendo cha Baba wa Taifa kumuwekea kauzibe mwaka 1995 asigombee naweza kusema ilikuwa ni kumcheleweshea tu Ndugu yetu muda wa kutimiza ndoto zake. Na muda mwingi aliutumia kujijengea mazingira ya kuingia Ikulu mara baada ya Mkapa.
Utaweza kuona ni jinsi gani mbio za Urais 2005 ziligubikwa na kuchafuana pamoja na kashfa ambazo hapo awali hatukuwahi kuzisikia na ziliisha mara tu baada ya Ndugu yetu huyu kupitishwa na chama chake "Tukufu" kuugombea Urais (kutimiza ndoto zake). Baada ya kufanikiwa kutimiza ndoto zake, huyu Ndugu yetu akapumzika (wengine watasema akajisahau) na kupelekea waliomsaidia kwenye harakati kuanza kuchafuka na kutotamanika tena katika jamii. Wao watamlaum (Ila yeye hatajali kwa kuwa alishatimiza ndoto zake, shauri yao).
Katika mahojiano yake akawahi kuulizwa eti kwa nini Tanzania ni masikini, naye kwa mshangao akajibu kwamba hajui. Kimsingi hakuwahi kufikiria kuhusu Tanzania na umasikini wake. Bali aliwahi kufikiria Tanzania chini ya Uongozi wake kama Rais. Kwenye Kampeni akasisitiza watu wampe kura ili ajitahidi kutembeza bakuli zaidi tusije tukafa njaa!! (Haamini kabisa kwamba watanzania tunaweza kuishi bila kuomba misaada) Hakujali ni ahadi zipi atatimiza bali alikuwa tayari kuahidi hata kama ni kununulia kila kijiji ndege yake alimradi ndoto zake zitimie.
Ni mambo mengi sana amekuwa akitenda na yakasemwa juu yake, ila kimantiki tunaomsema tunakosea kwa kuwa yeye anaishi ndoto zake. Alitamani kusafiri kwenda nchi mbali mbali, alitamani sana awe anapigiwa mizinga pamoja na kukwagua magwaride, apigiwe saluti kila anapopita na aitwe Mheshimiwa na watu wote. Hizo zilikuwa ndoto zake na amezitimiza. Sisi tunaolalamika anatushangaa na huenda kimoyomoyo anatuuliza: Hivi ninyi ni ndoto ipi katika maisha yenu mliwahi kutimiza?
Kauli ya Baba wa Taifa kuwa "Tukiona mtu anang'ang'ani kwenda Ikulu, basi tumuogope kama Ukoma" ilikuwa na maana kubwa sana.
Cha msingi tuwe makini huko tuendako tusijikute tunaingia tena huu mkenge wa kuwapa Uongozi mkuu wa nchi watu ambao wanautaka ili tu watimize ndoto zao. Wapo watu ambao ndoto zao kuu ni kuikomboa nchi dhidi ya Umasikini. Hao ndiyo wanaotufaa. Na kubwa zaidi kila mmoja wetu, kwa nafasi yake ashiriki kuikomboa kifikra Jamii yake dhidi ya hawa akina Karunguyeye wanaotumia Nyumba za Ibada pamoja na vyombo vya habari kuhubiri sera zao ili waje kutimiza ndoto zao.
Mapendo.