Kuna ishara kabla ya kufikwa na mauti

Kuna ishara kabla ya kufikwa na mauti

Ramea

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
2,146
Reaction score
4,090
Katika kipindi hiki ambacho kuna vifo vingi, nime experience baadhi ya matukio ambayo huwa ni nadra kutokea ila huashiria jambo ambalo si la kheri

1. Kuna siku jirani yangu nilimkuta anamwaga takataka za vyombo vilivyovunjika nikamwuliza ilikuwaje vyombo vyote hivi vivunjike kwa wakati mmoja? Akajibu ni kabati limeanguka bila kusukumwa wala uwepo wa upepo likiwa lenyewe tu. Hata sisi tukio hili limetustaajabisha sana. Haikupita wiki yule jirani yangu alipata ajali ya kugongwa na gari akiwa anaendesha pikipiki akafariki papo hapo. R.I.P Mpambanaji.

2. Rafiki angu ambaye alikuwa mtaalam wa ultrasound hospitali x, wiki kadhaa kabla hajafariki alikuwa anazungumzia sana kifo. Yaani ukikaa naye Hadi anaudhi stori zake za kifo tena akijizungumzia yeye mwenyewe ataiachaje familia yake kana kwamba alikuwa anajua. Cha kushangaza alikuwa na afya njema tu nilishtuka napigiwa simu nikiwa safarini kuwa rafiki yangu amefariki alikimbizwa hosp usiku alikosa pumzi na hakuwahi kupatiwa matibabu. R.I.P Comrade.

3. Brother wangu wa tumbo moja, alikuja nyumbani kwangu ingawa huwa anakuja mara kwa mara, ila hii ya mwisho alikuwa wa tofauti kidogo. Aliomba achukue vitu vyake(huwa anaacha mabegi au mabox ) mara zote tunamletea begi au box analotaka akiwa sebuleni, lakini awamu hii aliingia mwenyewe chumbani, chumba ninachokitumia kama store. Kumbe ndo ilikuwa last visit. Ameondoka kwa changamoto ya upumuaji, kukohoa na kukosa hamu ya kula. R.I.P Brother
Msg zako za mwisho WhatsApp bado nazisoma kila muda. Naona kama bado upo nasi.
 
KILA NAFSI ITAONJA MAUTI NA HAKUNA AJUAYE SIKU WALA SAA.KIFO JI FUMBO KUBWA SANA MKUU
 
Kifo kina husisha roho na nafsi kuucha mwili. Roho huwa na information zote, hata umauti unapokuwa umekaribia roho hujua ( mambo huanzia katika ulimwengu wa roho ), mwili jambo huonekana baada ya rohoni kukamilika. Na ndio kuna ule msemo kuna watu wanatembea ila walishakufa ( wamekufa rohoni tayari ). Nini kinafanya wasijue ? Ni ile kutokuwa na uwezo wa kutafsiri lugha ya rohoni
 
Ishara hujitokeza kabla ya kifo, sema wengi hupuuzia
 
Mi mzee wangu aliniambia nataka uniletee kitu flan na nataka nisafiri nikapumzike. Haikupita wiki mbili.
Nina rafiki yangu wa karibu yeye aliniambia hivyo hivyo nataka nisafir nikapumzike kesho yake nae akafa.
 
Mgonjwa kugeukia ukutani kukataa kuonana na watu n dalili mojawapo

Mtu akiwa anaumwa akaanza ita watu kwa wingi wamuone na hata kugawa baadhi ya nguo na hii n dalili

Mgonjwa kupona ghafla na kudai aina fulani ya chakula na kupiga stry nyingi sana na hii n dalili
 
Kaka yangu aliugua akawa yupo
ICU lakini siku moja kabla ya kufa alichangamka sana ilikuwa jioni, nilipoenda kesho yake kwenda kumuona asubuhi alikuwa tayari amefariki,

Mama yangu mzazi wakati anafariki alihitaji wanae wote tuwepo, ila mimi nilikawia kufika nilipofika tu haikupita mufa akafariki.
 
Back
Top Bottom