GE2025 Kuna hatihati hazina kukauka uchaguzi ukikamilika na maisha yakawa magumu zaidi kuliko kawaida

GE2025 Kuna hatihati hazina kukauka uchaguzi ukikamilika na maisha yakawa magumu zaidi kuliko kawaida

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
23,877
Reaction score
31,632
Mara nyingi kipindi cha uchaguzi pesa nyingi mno hutumika kwenye kampeni na mbilinge mbilinge za hapa na pale kuhakikisha chama tawala kinabaki madarakani kwa namna yoyote ile mwisho wa siku uchaguzi ukitamatika hazina inabaki nyeupe na watanzania huwa wanakuwa kwenye kipindi kigumu mno cha maisha na huwa wanakamuliwa kweli kweli kurudisha pesa kwenye hazina.

Kipindi hiki naona matumizi ni makubwa mno kuanzia kununua vyama pinzani , kuzima watu / ubambikiwaji wa kesi kwa watu wanaonekana watakwamisha ushindi kwa chama tawala, hivyo pesa nyingi inatumika hapo.

Pesa nyingi ya tanganyika kuelekezewa Zanzibar hili nalo ni pigo kubwa mno.

Pesa za kulipa vilabu vya mipira kuongeza hamasa kwa chama tawala .

Pesa kwa viongozi wa juu wa ngazi za usalama kuhakikisha chama tawala kinaendelea kubakia madarakani nk.

Sasa haya yote maumivu yatazidi kuonekana baada ya uchaguzi.

Na hata wale chawa waliokuwa wanapewa elfu 10, 10 kukipigia promo chama tawala watajuta haswa hawa ndugu zetu wa bodaboda.

Bado hatuja chelewa sana.

No reform no election

CCM must go.
 
Kukauka kushakauka kitambo kama huamini tazama wazabuni na wakandarasi wanataabika kupata malipo yao licha ya kukamilisha kazi/mikataba yao Tanroads na Tarura kuko hoi miaka 3 wakandarasi hawajalipwa wengi wao washaacha kabisa kuomba kazi za serikali mpaka taasisi za fedha zinagoma kuwapa pesa watu wenye miradi ya serikali.
 
Kukauka kushakauka kitambo kama huamini tazama wazabuni na wakandarasi wanataabika kupata malipo yao licha ya kukamilisha kazi/mikataba yao Tanroads na Tarura kuko hoi miaka 3 wakandarasi hawajalipwa wengi wao washaacha kabisa kuomba kazi za serikali mpaka taasisi za fedha zinagoma kuwapa pesa watu wenye miradi ya serikali.
True uko sehemu nyeti sana kwenye hiyo sekta kiufupi unaijua nje ndani unachosema ni sahihi kabisa
 
True uko sehemu nyeti sana kwenye hiyo sekta kiufupi unaijua nje ndani unachosema ni sahihi kabisa
Ukizingatia Road Fund imeuwawa chini ya ushauri wa Mwigulu & co mafungu yote lazima yapite hazina ndo yagawiwe kidogo kidogo kwa matakwa ya Mwigulu kama unasafiri mikoani mara kwa mara barabara zetu kuu zote zimeharibika zina hali mbaya sana ukielekea Iringa, Mbeya mpaka Songwe kutoka Moro njia mbovu ukielekea Dom kutokea Moro barabara ina mashimo kama hupiti mara kwa mara unaweza pata ajali nenda mpka Singida, Nzega, Shinyanga mpaka Mwanza toka hapo elekea Mara mpaka Tarime na Silali bila kusahau njia ya Kaskazini nayo hoi ipo pia ukipita Dom/Iringa au Iringa/Dom nako taabani Matengenezo hakuna watu walioko juu hata hawana abc za miundombinu kama barabara
 
Division 0 ambayo ilipatikana licha ya mtu kusoma kidato cha 4 pekee miaka 3 hamkuona ni dosari kubwa?
 
Umesahau na pesa zilizonunua baiskeli na bodaboda na ile mikopo ya halmashauri.

Kwa akili za watanzania hakuna atakayerejesha, wanajua wamepewa sababu ya uchaguzi ili kusema mitano tena..!!
😂😂😂😂😂
 
Ila kweli pesa zinachezewa jamani, kwenye mkutano wa kampeni hapa Songea, wanafunzi wa shule mbali mbali wakiongozwa na na songea Boys, wamepewa ma tisheti ya chama, haya wananchi wamepewa khanga, tisheti, vifungashio, vibendera.

Hadi unajiuliza hizi pesa si zingepelekwa kwa miradi mingine muhimu ya nchi. Kampeni ya nn ikiwa uhakika wa kutikiwa upo?

Inasikitisha na kuumiza sana. 😢😢😭😭
 
Nilidhani uchaguzi wa 2020 ndo ungekuwa uchaguzi wa mwisho wa hovyo ila huu wa 2025 umekuwa wa hovyo mno. Demokrasia imebakwa na kulawitiwa kwa pamoja.
 
Sikuona umuhimu wa kutumia gharama zote hizi kufanya Uchaguzi ambao unayeshindana naye anazungumzia Sera ya Kula Ubwabwa 🙌

Hizi fedha zingetumika kufanya miradi ya maendeleo tu, na kuongeza mzunguko wa fedha Mtaani
Machawa wamekaa chini toka january wansuka namna ya kupiga pesa ya kampeni alafu zisipigwee haiwezekani.
 
Back
Top Bottom