kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,428
- 13,936
Sipendi kuoa kwakuwa sipendi kutoa mahari, maana sioni kwanini nitoe mahari wakati mimi, mke wangu na wakwe zangu wote tutakwenda kutegemeana kwa hali na mali. kwanini nipeleke ng'ombe zangu kwa wakwe zangu kama mahari badala ya kuziacha ili zije ziwasaidie wajukuu zao watakaozaliwa? mke, watoto, wazazi na wakwe nitawahudumia vipi?
Jana siku ya wanawake nilisubiria nisikie wanawake wenyewe wakitoa tamko la kuikataa mahari ambayo ndiyo miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia unyanyaswaji wa wanawake majumbani, lakini sikusikia chochote. Bado natafuta mwanamke na wakwe ambao hawataki mahari kabisa.
Je, ni hasara gani nitaipata kama nitaoa mke bila kutoa mahari?