Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Tangu Dodoma itangazwe kuwa jiji, bei za viwanja katika manispaa hii zimekuwa juu mno kiasi cha mita moja ya mraba kufikia kuuzwa kwa bei ya shilingi 8000 kwa maeneo ya Michese na hata Nzuguni bei inatarajiwa kuwa ni hiyo.
Bei zingine kwa mita moja ya mraba ni kati ya shilingi 5000/= mpaka kufikia shilingi 7500/= kutegemeana na location na aina ya matumizi ya kiwanja ambapo viwanja vya makazi na biashara ndio bei yake huwa ipo juu zaidi kulinganisha na vya makazi tu ila vyote viko katika hiyo range.
Maeneo haya mengi ni mapori kwa maana hata miundombinu kama maji na umema bado ila bei ndio hizo.
Sasa najiuliza,katika nchi hii,kuna Halmashauri yoyote imewahi kuuza viwanja ambavyo ni mapori na vilivyo mbali na katikati ya mji kwa bei za aina hii huku wakitoa muda wa kulipa wa ndani ya miezi mitatu?
Hivi hata Manispaa za Dar-es-Salaama,na wao leo hii wanaweza kuuza viwanja kwa bei hizo?
Tunawashukuru kitu kimoja kwamba ukilipia kiasi fulani au ukionyesha unajitahidi kulipa,basi wanaweza kukuvumilia na kukuongeza muda ingawa kulipia huku bado hakukupi guarantee
Hata hivyo,bei hizi na muda huo ni realistic kwa watanzania wengi?
Na kingine ni Manispaa hii kuuza viwanja kupitia ramani (mtu unachagua kiwanja kwenye ramani tu) bila kwenda sight na ili ukaone kiwanja husika ulichochagua, ni mpaka uwe umekamilisha malipo.
Waziri Lukuvi tunaomba utazame jambo hili hasa huu muda wanaoutoa kwani ni mfupi mno na unawafanya watu wengine hata kusita kununua kwa hofu ya kunyang'anywa muda uliopangwa kulipia ukiishi bia ya kukamilisha malipo.
Mipango na mikakati ya kuendeleza mji huu ni mizuri kwa mfano ujenzi wa hili jengo lnaloonekana katika picha hapo chini litakolejengwa katika Mji wa Serikali maeneo ya Mtumba, ila hizi bei za viwanja pamoja na muda mnaoutoa, kwakweli haviendani kabisa na maisha ya watanzania walio wengi.