Kuna haja ya zile Bilioni 30 za ukarabati Uwanja wa Mkapa kufanyiwa Ukaguzi/Uchunguzi

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Nliposikia serikali imetoa kiasi cha Tsh Bilioni 30 kwa ajili ya ukarabati Uwanja wa Hayati Mkapa nlipigwa na Dafrao kwanza nikiamini hizo bilioni 30 zilikua na uwezo wa kujenga kiwanja standard kizuri tu.

Lakini baada ya kueleweshwa nikawa mpole nikisubiri nione mabadiliko chanya tuliyoambiwa yataonekana baada ya ukarabati kukamilika ila kwa kifupi zidi ya kuona yale matangazo ya African cup yamejaza uwanja sikuona jipya lolote la bilioni 30 ni mabadililko madogo sana tena labda kwa ndani ila kwa mazingira ya nje kiwanja kiko vile vile.

Nimejaribu kuangalia running Track bado ni chakavu rangi zake bado hazijakolezwa ni zile zile za zamani, tumeshuhudia wakiweka yale mabango ya electronics sio ajabu wamechukua yale ya Mkwakwani wameyahamishia Lupaso au yale ya Mkwakwani tuliyoyaona wakati wa Mashindano ya Community shield bado yapo mtanisaidia kunijuza kama bado yapo.

Kuna kauli inasema Wacha inyeshe tuone panapovuja yes imenyesha Dar es Salaam tumeona panapovuja pamoja na Uwanja wa Mkapa nimeona video kadhaa pitch limejaa maji kweli nchi kama nchi tumeshindwa kuwa na wataalamu wa kuseti Drainage System pale Lupaso bado tunatumia magodoroo kufyonza maji bado tuna safari ndefu hakika.

Ifike mahali angalau kila Mtanzania awe na uchungu wa hizi fedha ambazo ni kodi za wananchi na Mikopo soon utasikia bilioni 30 zimekata wanaomba kuongezewa bilioni 50 zingine.
 
Back
Top Bottom