Kuna haja ya kupunguza umri wa kustaafu kwa watumishi kutoka miaka 60 ya sasa hadi 50

KUSYAMA

Member
Jan 27, 2011
6
0
Facts:
1) Kwanza umri wa kuishi kwa Watanzania umeshuka mpaka miaka 45, kwa maana hiyo watumishi wetu walio wengi hawataweza kustaafu wakiwa hai. ni vizuri tupunguze umri wa kustaafu uendane na umri wa kuishi kwa Watanzania kama zinavyoonyesha tafiti nyingi juu ya umri wa mtanzania kuishi duniani.

2) Watumishi waliowengi wanabweteka na urefu wa umri wa kustaafu na kuwafanya wasijiandae kwa maisha ya baadae, badala yake wanaponda mali wakiamini muda wa kustaafu bado mwingi so watajiandaa tu.

3) Serikali itakuwa imetoa fulsa kwa vijana wengi kuingia kazini na pia kuwafanya watumishi wa serikali kwenda kujiajili wakiwa bado wana nguvu na weledi mkubwa wa kuendesha miladi mbalimbali baada ya uzoefu na mtaji watakao kuwa wameupata kupitia uwekezaji wao ktk mifuko ya jamii.
Tofauti na tunavyowaimiza vijana kujiajili bila wao kuwa na mitaji wala uzoefu wowote wa kimaisha, biashara na utumishi.

4) Kuwaondolea watumishi wetu utegemezi wa ajira kwa muda mrefu, jambo linalowafanya kuwa tegemezi wa ajira na ata pindi wanapostaafu kuomba mikataba au kupita pita maofisini waonekane bado ni watumishi.

5) Kuleta rotation ya utumishi wa umma katika kipindi kifupi, ili kuwezesha mpishano kwa wakati muafaka kati ya vijana wasaka ajira na watumishi wanaostaafu.

6) Mtumishi aliyefanya kazi kwa miaka 50 serikalini au sekita binafsi anayo fulsa kubwa kujiajiri mwenyewe kuliko kijana anayehitimu chuo bila mtaji wala uzoefu wowote wa maisha au utendaji.
Mtumishi huyu anazo fulsa nyingi kama ifuatavyo:
1. Ana uzoefu wa kujisimamia kuliko kijana aliyehitimu soon
2. Ana mafao ambayo anaweza kuyatumia kama mtaji mkubwa kibiashara
3. Anakopesheka rahisi zaidi kuliko kijana huyu aliyehitimu chuo juzi tu
4. Ana partiners wengi kuliko kijana huyu aliyehitimu chuo juzi
5. Huyu mtumishi tayali ana experience ya mafanikio

Angalizo:
A) Huu ni mtazamo wangu na si mapendekezo, serikali ambayo ni wananchi inaweza kubolesha wazo hii na likaleta tija kwa vijana na wastaafu wetu Tanzania.

B) Serikali iwaamasishe watumishi kuwekeza ili waamie kwenye ujasiliamali na kuwapisha vijana waliohitimu vyuo kuingia serikalini wapate uzoefu wa maisha ya kazi, kujisimamia, maisha na ujasiliamali mdogo wakiwa kazini kisha na wao wajiandae kung'atuka kuwapisha wanao kuja.

TANZANIA BILA UMASIKI INAWEZEKANA

Ni mtazamo tu.............................., unaweza pia toa hojaaaaaaa

mi binafsi nina miaka 45 now
 
Aya ya kwanza si kweli. Unaweza kutuambia takwimu zinasemaje kwa sasa 2016 kuhusu life expectancy ya Watanzania? Maana nahisi mwaka jana kwenye world Bank indicators database (2015) ilikuwa around 60. Hebu tupe source ya aya ya kwanza kwamba life expectancy ni Miaka 45
 
Pili tupe link ya baadhi ya hizo tafiti zinazosema umri wa mtanzania wa kuishi ni miaka 45. Tafiti hizo ni za zamani sana itakuwa. Jaribu kusoma recent literature mkuu kabla hujaweka threads yako hapa.
 
Aya ya kwanza si kweli. Unaweza kutuambia takwimu zinasemaje kwa sasa 2016 kuhusu life expectancy ya Watanzania? Maana nahisi mwaka jana kwenye world Bank indicators database (2015) ilikuwa around 60. Hebu tupe source ya aya ya kwanza kwamba life expectancy ni Miaka 45


The 2012 Census preliminary results show that the life expectancy at birth for Tanzanians has increased from 50 years in 1988 to 61 years in 2012. The results further show that female life expectancy at birth is higher (63 years) than that of males (60 years). The increase in life expectancy over a decade is attributed to increased economic growth and reduced income poverty (basic needs).

Source: 2014 Basic Demographic and Socio-Economic Profiles report, 2012 Population and Housing Census
 
Idea yako nzuri but umebwabwaja Sana ,ungetulia ingekua thread ya kueleweka Sana ,jipange then urudi watu wachangie.
 
Kiukweli kuna haja ya serikali kuliona hili nakupunguza ,umri wa kustaafu angalau kua miaka 50 kwa lazima na 45 kwa hiyari


Sent from mTalk
 
Picture_297.png
 
Back
Top Bottom