Umri wa kustaafu ukipunguzwa, vijana hawawezi kuajiriwa?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Sheria ya kustaafu kwa sasa ni mpaka miaka 60 lakini ukosefu wa ajira nchini ni mkubwa mno. Ninavyoongea kuna vijana tangia 2015 bado wanahangaikia ajira. Unakuta kuna wazee zaidi ya miaka 55 bado wako kazini na utendaji kazi wao umepungua kwa kiasi kikubwa.

Je, tukipunguza umri wa kustaafu hatuewezi kuongeza upatikanaji wa ajira kwa vijana?
 
Kwani ajira maana yake kuajiriwa serikalini?. Yaani kila kijana aajiriwe na serikali?
 
Kwani kwenye sekta binafsi umri ni huo huo..labda upate huruma ya boss..ila kuna point kubwa kwenye hii mada..
Maana watu wanakufa mapema sana hasa hawa wa 50-60
 
Sekta Binafsi uamue mwenyewe kuacha kazi nimewah kukuta Mzee anafanya kazi sehemu miaka yake inacheza kwenye 80 mpaka nikashangaa anakwambia amestaafu miaka 25 ilopita
 
Na hao vijana watakuja kulalamikia huo umri uliopunguzwa wakishafika kwenye kustaafu.

Mm nashauri, kazi za serikalini ziwe za mikataba kulingana na ufanisi na fainali unayoleta kwa kampuni, yani ukionekana huna ufanisi hvy huleti faida kwa kampuni wakutoe.
 
Mawazo duni haya Kwa kuamini kuwa ili wewe upate kazi lazima watu wawe redundant (kustaafishwa) kupunguzwa kazi.
 
Miaka 55 amekua mzee😂.

Shida ni kwamba watu wote wanategemea ajira za serikali.

Tutengeneze mazingira ya watu kujiajiri, watu wengi wawe na ajira binafsi hiyo miaka 60 haitatosha ndio maana huko ulaya wanaipeleka 65 hadi 80.

Sasa sababu ya watu wote kuangalia sehemu moja ndio tunaanza kuleteana uchawi mtu wa miaka 40 pia ataitwa mzee
 
sheria ya kustafu kwa sasa ni mpaka miaka 60 lakini ukosefu wa ajira nchini ni mkubwa mno. Ninavyoongea kuna vijana tangia 2015 bado wanahangaikia ajira. Unakuta kuna wazee zaidi ya miaka 55 bado wako kazini na utendaji kazi wao umepungua kwa kiasi kikubwa.

Je, tukipunguza umri wa kustaafu hatuewezi kuongeza upatikanaji wa ajira kwa vijana?
Hiyo ni kuongeza mzigo wa gharama zaidi za matumizi ya umma yasiyo ya Lazima 🐒

R I P Laigwanan comrade ENL
 
sheria ya kustafu kwa sasa ni mpaka miaka 60 lakini ukosefu wa ajira nchini ni mkubwa mno. Ninavyoongea kuna vijana tangia 2015 bado wanahangaikia ajira. Unakuta kuna wazee zaidi ya miaka 55 bado wako kazini na utendaji kazi wao umepungua kwa kiasi kikubwa.

Je, tukipunguza umri wa kustaafu hatuewezi kuongeza upatikanaji wa ajira kwa vijana?
Try thinking out of the box, hao viongozi wazee wako wangapi?
Na hao vijana wa kujaza nafasi wako wangapi?
 
Hao wastaafu wanaitaji pension Kila mwisho wa mwezi...hapo itakuwa unatwanga maji kwenye kinu
Umri WA kustaafu ulitakiwa uwe 70 years. Ukitokea hapo unasubiri Nchi nzuri ya kumetameta. Pensheni zingebaki nyingi na Serikali ikafaidi
 
sheria ya kustafu kwa sasa ni mpaka miaka 60 lakini ukosefu wa ajira nchini ni mkubwa mno. Ninavyoongea kuna vijana tangia 2015 bado wanahangaikia ajira. Unakuta kuna wazee zaidi ya miaka 55 bado wako kazini na utendaji kazi wao umepungua kwa kiasi kikubwa.

Je, tukipunguza umri wa kustaafu hatuewezi kuongeza upatikanaji wa ajira kwa vijana?
Hiyo ni vicious circle, hakuna ajira inayoongezeka wala kupungua dawa ni kubadilisha mfumo wa elimu na kujikita katika ujenzi wa viwanda na teknolojia!
 
sheria ya kustafu kwa sasa ni mpaka miaka 60 lakini ukosefu wa ajira nchini ni mkubwa mno. Ninavyoongea kuna vijana tangia 2015 bado wanahangaikia ajira. Unakuta kuna wazee zaidi ya miaka 55 bado wako kazini na utendaji kazi wao umepungua kwa kiasi kikubwa.

Je, tukipunguza umri wa kustaafu hatuewezi kuongeza upatikanaji wa ajira kwa vijana?
Nchi zote Duniani zinaongeza umri wa kustaafu unaelewa Kwa nini?

Jobless ana Nguvu za kutafuta au hata kupewa pesa ya kujikimu ila mzigo wa mstaafu ni mkubwa zaidi so hakuna Nchi itapunguza huo umri.

Juzi hapo Kuna Nchi imeongeza umri wa kustaafu kuwa miaka 70 sema nimesahau.

Unadhani Kwa nini Jiwe aliamua kuja na sheria Mpya ya kikokotoo?
 
Back
Top Bottom