Kongosho
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 35,987
- 24,234
Samson alikutana na Delila chuoni, akampenda na kumweleza, lakini Delila akawa hajatoa maamuzi yeyote.
Wakati huo huo, Delila akakutana na Ibra, wakaelewana na wakaendelea na mapenzi yao.
Delila akamweleza Samson kuwa keshampata mwingine kwa hiyo aendelee na maisha yake.
Kila mtu akaendelea na maisha yake, lakini Samson kila mara akikutana na Delila humlaumu sana kwa nini alimkataa. Na anaonesha chuki kubwa kwa Ibra kuwa ndio sababu ya yeye kumkosa Delila.
Samson keshaoa na ana watoto kadhaa, lakini kila mara lawama haziishi kwa Delila.
Sasa, kuna haja ya Sam na Delila kuendelea kulaumiana bado? Wakati imepita miaka zaidi ya kumi na tano?
Wakati kila mtu ana familia yake na maisha yake?
Samson sana mke halali wa ndoa, nini tatizo?