Kuna haja ya kuangalia mavazi ya mtu kwenye usaili wa kazi?

Vijana!
Interview ni mambo mengi sana yanaangaliwa. Kumbuka watu 1000 mnapambania nafasi 10. what do you expect? Kama ni vyeti wote 1000 wanavyo. kama ni maswali wote wamejibu vizuri kabisa. kwa ufupi wote wanalingana katika kila nyanja.
hapo tutaanza kuangalia nani ana cha zaidi. Kwenye mavazi hatuangalii ya utajiri na umaskini. Tunaangalia unavaaje na unaonekanaje. Hata kama shati lako la kitenge limepauka lakini liko smart, na umelivaa vizuri utaweza kuwazidi waliovaa za mlimani city zenye vilaka. Umenyoaje? Unaongeaje? Makucha yako?.. na mengine mengi. So be prepared kwa kila kitu. Hata mpangilio tu wa Document zako unaweza kuonyesha uko smart kiasi gani.
 
USMART WA MTU KICHWANI UNAPIMWAJE NA MAVAZI?

JAMAA MMOJA HAPO JUU AMESHARE NAMNA GANI NCHI ZILIZOENDELEA KUWA MKIFANANA KILA KITU HUWA WANA MASWALI YA KIDUNIA KUONA UNA UELEWA KIASI GANI NA MASUALA MBALIMBALI YA KIDUNI.

NGUO HAINA UHUSIANO WOWOTE NA USMART WA KICHWA CHA MTU.

NATAKA UNAIMBIA HAPA NGUO ZINAAKISI VIPI AKILI YA MTU?
 
Mavazi na huna kazi? Umewaza kwa upana wake kweli? Mavazi yana impact gani kwenye kazi zako? Let say umepigilia T-shirt na Jeans itaathiri uwezo wako wa kufikiri au ufanisi?
Yaani jibu hapo kwanza.
First impression matters. Kama alivyosema mdau hapo juu kuna kazi zinakuhitaji na kuna kazi unaihitaji. Sasa kama upo kundi la kuhitaji kazi lazima ufuate protocol zote za usaili.
 
TRA dodoma,wewe ukienda kufata huduma umevaa kaptula,suruali imekubana sijui crazy jeans we ujue huingii Sasa ndo interview yao wasimamie wao unatarajia nin hapo
 
Hata muuza vyombo akiamka asubuhi lazima afute vyombo vumbi kuviweka smart! Mbona mkitongoza first date mnakuwa smart. Vijana vaeni smart kwenye interview acheni usasa utawaponza .
 
  • Thanks
Reactions: apk
First impression matters. Kama alivyosema mdau hapo juu kuna kazi zinakuhitaji na kuna kazi unaihitaji. Sasa kama upo kundi la kuhitaji kazi lazima ufuate protocol zote za usaili.
Unakwepa swali la msingi sasa, MAVAZI yana uhusiano gani na IQ ya mtu?
 
Hata muuza vyombo akiamka asubuhi lazima afute vyombo vumbi kuviweka smart! Mbona mkitongoza first date mnakuwa smart. Vijana vaeni smart kwenye interview acheni usasa utawaponza .
Mavazi yana impact gani kwenye usaili? Yaani jibu hili swali, kuwa smart no vile mtu anavyoona yeye, mwingine anatafsiri kuvaa Tshirt na Jeans, mwingine Suruali ya kitambaa + Shati, mwingine full suti nk.

Swali la msingi MAVAZI yana ATHIRI VIPI AKILI YA MTU kiasi kwanza kumkosesha kazi?
 
First impression matters. Hayo ya IQ kubwa yatakuja baadae. Yani uende interview ya bank au law firm umevaa tshirt na jeans halafu usingizie una iq kubwa
 
  • Thanks
Reactions: apk
Unakwepa swali la msingi sasa, MAVAZI yana uhusiano gani na IQ ya mtu?
Hakuna uhusiano ila mavazi kiujumla ni utaratibu wa uvaaji uliokubalika katika maeneo fulani.

Tambua jinsi ya kuheshimu sehemu husika ndo maana hata shule waliamua kuwa na uniform haijalishi mwanafunzi ni kilaza au kipanga wote wanvaa...zipo professional zinaheshimika kama urubani, macaptains wa meli hata majeshi na polisi wanvaa uniform kabisa.

Kama una shida ya kazi basi fuata taratibu ndo maana unatakiwa kujua taasisi husika kabla ya kuenda kama hutaki mavazi yao basi usi-apply.
 
First impression matters. Hayo ya IQ kubwa yatakuja baadae. Yani uende interview ya bank au law firm umevaa tshirt na jeans halafu usingizie una iq kubwa
Hujajibu swali la msingi. Na nikwambie ukweli 90% ya wenye mawazo ya First Impression matters ni watu wasiotumia akili zao kwa ufasaha.

Usiweke hoja za huko mnakotongozana ukataka kuiweka kwenye usaili wa kazi.

Tunaajiri weledi na ujuzi wa mtu na sio mavazi yako. What we need ni uwezo wako wa kuelewa na kuchambua mambo, ili tupate ideal candidate lazima tuangalie namna gani anaweza kujibu maswali kwa uelewa mpana.

Unakomaa na First Impression matters we unadhani watu wanataka papuchi yako?
 
Hakuna uhusiano ila mavazi kiujumla ni utaratibu wa uvaaji uliokubalika katika maeneo fulani.

Tambua jinsi ya kuheshimu sehemu husika ndo maana hata shule waliamua kuwa na uniform haijalishi mwanafunzi ni kilaza au kipanga wote wanvaa...zipo professional zinaheshimika kama urubani, macaptains wa meli hata majeshi na polisi wanvaa uniform kabisa.

Kama una shida ya kazi basi fuata taratibu ndo maana unatakiwa kujua taasisi husika kabla ya kuenda kama hutaki mavazi yao basi usi-apply.
Taratibu za kuomba kazi ni tofauti na za kuajiriwa. Mtu anapoomba kazi maana yaka hana hiyo kazi.
Mtu akiajiriwa anapewa pesa ya kujikimu ambayo inajumuisha na aina ya mavazi ambayo atatakiwa kuwa nayo, unapewa pesa ya maandalizi kwa maana wanajua hauna.

Utahitaji vipi mtu awe amevaa kama mfanyakazi wakati sio mfanyakazi?

Kwanini wasishoneshe sare za usaili sasa?
 
Hujajibu swali la msingi. Na nikwambie ukweli 90% ya wenye mawazo ya First Impression matters ni watu wasiotumia akili zao kwa ufasaha.

Usiweke hoja za huko mnakotongozana ukataka kuiweka kwenye usaili wa kazi.

Tunaajiri weledi na ujuzi wa mtu na sio mavazi yako. What we need ni uwezo wako wa kuelewa na kuchambua mambo, ili tupate ideal candidate lazima tuangalie namna gani anaweza kujibu maswali kwa uelewa mpana.

Unakomaa na First Impression matters we unadhani watu wanataka papuchi yako?
Unachekesha kweli wewe. Kwangu mimi first impression matters na usinichukulie poa. Mengine uliyosema ni bullshit tu
 
Nachoona wenye hoja ya kwamba mavazi hayawezi kutumika kwenye usaili ni kama wanapoint hivi. Walioteta mavazi hawana hoja za msingi kuhusiana na uhitaji wa ajira yenyewe. Wengi tupo kinadharia zaidi.
 
Taratibu za kuomba kazi ni tofauti na za kuajiriwa. Mtu anapoomba kazi maana yaka hana hiyo kazi.
Mtu akiajiriwa anapewa pesa ya kujikimu ambayo inajumuisha na aina ya mavazi ambayo atatakiwa kuwa nayo, unapewa pesa ya maandalizi kwa maana wanajua hauna.

Utahitaji vipi mtu awe amevaa kama mfanyakazi wakati sio mfanyakazi?

Kwanini wasishoneshe sare za usaili sasa?
Upo sahihi kwa kiasi fulani ila tambua lazima ujue utaratibu wa kampuni husika kwanza kabla ya interview.

Ukiachana na mambo ya mavazi inabidi utambue hata moja mbili tatu ya hyo kampuni...Hii inapima katika interview kwa muombaji kwa ujumla anaweza vip kufit katika nafasi hyo.

Taratibu za mavazi zinajulikana kama TRA anaweza kuenda pale hata mimi naenda ila naona sana sana wanavaa mashati meupe au blue bahari na koti kwa mbali hata ukienda Banks utakuta huu utaratibu.

Interview ni kumshawishi muajiri wewe unaweza kufit vip pale ka written ushapiga fresh sasa hapa umshawishi tena upya...

Kama unabisha nenda na modo na mashati haya ya kuwaka waka, mara yana maandishi.

Kufauta utaratibu ni simple nunua shati lako la rangi moja safi then litumie kwa ajili ya interview .
 
  • Thanks
Reactions: apk
Unachekesha kweli wewe. Kwangu mimi first impression matters na usinichukulie poa. Mengine uliyosema ni bullshit tu
Duh, impression lkn si inategemea na shepu ya mtu pia? Kwa mfano mtu mfupi mwenye kitambi na Mrefu aliyejazia balanced huoni watakuwa tofauti hata kama watavaa same code?

Kigezo cha mwonekano ni kigezo biasness zaidi. Maana itategemea na mtu anavyoonekana na namna nguo zilivyomkaa kisawasawa.

Hiki kigezo unakitumia kwa kutumia Knowledgeable mind kweli?
 
Upo sahihi kwa kiasi fulani ila tambua lazima ujue utaratibu wa kampuni husika kwanza kabla ya interview.

Ukiachana na mambo ya mavazi inabidi utambue hata moja mbili tatu ya hyo kampuni...Hii inapima katika interview kwa muombaji kwa ujumla anaweza vip kufit katika nafasi hyo.

Taratibu za mavazi zinajulikana kama TRA anaweza kuenda pale hata mimi naenda ila naona sana sana wanavaa mashati meupe au blue bahari na koti kwa mbali hata ukienda Banks utakuta huu utaratibu.

Interview ni kumshawishi muajiri wewe unaweza kufit vip pale ka written ushapiga fresh sasa hapa umshawishi tena upya...

Kama unabisha nenda na modo na mashati haya ya kuwaka waka, mara yana maandishi.

Kufauta utaratibu ni simple nunua shati lako la rangi moja safi then litumie kwa ajili ya interview .
Lakini kuijua kampuni sio kujua mavazi, bali huduma zake. Unapoambiwa unapaswa kuijua kampuni basi unatakiwa kuijua kampuni au taasisi juu ya shughuli zake. Mavazi haimo kwenye hayo ya kujua juu ya kampuni.

Website ya TRA inaeleza juu ya mavazi? Ila ukiajiriwa utaambiwa sasa sisi utaratibu wetu ni hivi na hivi.

Hii sasa ya kuangalia huyu amevaa hivi ukampa kazi ndio shida ilipo.
 
Back
Top Bottom