Kuna haja ya Afrika kuwa na Chombo Huru cha kusimamia Chaguzi zote na kuwa na Sauti Moja dhidi ya Mataifa Makubwa

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
323
500
Wakuu,

Ni dhahiri kabisa kwa sasa mataifa ya Ulaya na Marekani wamekwisha ona udhaifu wa nchi za kiafrika kutosimamiana yenyewe kwa kuteteana au kuonyana pindi inapotokea chi nyingine nje ya bara Afrika linapoanza ukosoaji kwa kutimia sababu halali lakini malengo ni kinyume chake.

1. Hakuna taifa lolote ndani ya Afrika au Umoja wa nchi za |Afrika unakemea upotofu wa taifa jingine au kutetea udhalilishwaji kutoka wa mataifa makubwa yenye nguvu

2. Kila uchaguzi wa kila nchi unapowadia kila nchi husika, inapaswa pawepo chombo maalumu cha usimamizi wa chaguzi hizo ikishiriana na tume ya nchi hiyo kwa masharti yatakayowekwa kwa mujibu wa sheria

3. Kuhakikisha balozi zinazowakilisha nchi zao haziingilii mambo ya ndani ya nchi husika kinyume na majukumu yao yanayowataka kujadiliana na pande tofauti za kisiasa kabla ya kutoa tamko badala ya wanavyofanya kwa sasa. Ni kweli maeneo ya ofisi na makazi ya balozi au mtumishi yeyote mwandamizi wa uwakilishi huo unasimama kama eneo halali la utawala wa nchi hivyo taratibu za kimataifa zinawajibika kufuatwa ipasavyo

4. Mabalozi wengi kutoa nchi za Ulaya na Marekani kwa sasa wanachochea machafuko ya uasi katika nchi za ukaazi sio kwamba wanazipenda sana nchi za kiafrika, lahasha ila ni kwa maslahi ya kiuchumi ya nchi wanazoziwakilisha au makampuni yenye miradi katika nchi hiyo maaana wanawajibika pia kusimamia;

5. Huko Ivory coast, Nigeria, Uganda nk ambapo ni msimu wa kufanya uchaguzi tayari wanaonesha kupendelea vyama pinzani kwa kutoa matamko bila ya kufanya mawasiliano ya kiitifaki kupata maelezo toka upande wa pili na kushauri badala ya kuonesha kwamba kile walichokipata kutoa upande mmoja uko sahihi kinyume na utaratibu wa haki asili (natural justice whereas nobody should be condemned unheard) This is an obvious breach of diplomatic missions;

5. Nchi za kiafrika hazina umoja la sivyo wangekuwa wametoa tamko kuhusiana na tabia ya mataifa ya Ulaya na Marekani kuingilia mambo ya ndani kwa kisingizio ya kutetea demokrasia na haki za binadamu. Hakuna haki isiyokuwa na wajibu kutoka pande mbili;

Kwanini malalamiko ya kisiasa yanapelekwa kwenye balozi na taasisi za kimataifa wakati tuna sheria zetu kisa ni misaada na mikopo wanayotoa?

Hakuna taifa la Ulaya, Marekani linaloipenda Tanzania au kwamba kuna uvunjifu mkubwa sana wa haki za binadamu kuzidi Marekani ambko hadi sasa wameuwawa watu kadhaa tena weusi lakini hakuna hatua za dhati zinazochukuliwa kudhibiti badala yake wana piga kelele dhidi ya mataifa ya kiafrika kwa tamaa zrasirimali zetu na kuweka watu wao wataofanikisha ukwapuaji.

Waafrika amkeni sasa, kukataa haraka sana vinginevyo itatokea wameshaingia Ikulu wenyewe. Mkifanya hivyo heshima itakuwepo, bila hivyo msahau kuonewa kwa mgongo wa misaada, mikopo kwa kisingizio cha demokrasia na haki za binadamu. Doomsdays are speedily coming to overwhelm african sovereignty.

Nawasilisha
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,286
2,000
Wewe unawatetea genge la wakora wa CCM kwa kuleta porojo ndefu, kwakuwa ww na familia yako ni wafaidika wa hii hujuma. Sisi ni watanzania na tunaona hao wazungu wako sawa,na tutawaunga mjini mkono iwapo kweli watachukua hatua kali dhidi ya kundi la wahuni wanaonajisi chaguzi zetu. Msitumie kichaka cha nchi huru kuendesha chaguzi za kishenzi, zilizojaa ghiliba na uhayawani wa wazi, kwa kisingizio cha nchi huru.

Hujuma za zenu tumeziona toka kuengua wapinzani kwa kutumia sheria zenye nia ovu. Mabox ya kura zilizopigwa tumeziona, tena nyingine zikiwa mikononi mwa vyombo vya dola. Mauaji ya dhahiri ili kuweka madarakani viongozi wasio na ridhaa ya umma, kwa kisingizio cha uzalendo uchwara. Tena ninasikitika sana hao wazungu kutokuwaondoa viongozi wezi wa matakwa ya wananchi ya wananchi kwa kisingizio cha upuuzi uitwao nchi huru. Ule wa juzi haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. 2/3 ya watanzania hawakujitokeza kupiga kura, maana hawaridhiki na mwenendo wa uchaguzi, we unakuja na insha ya nchi huru!

Tunawaomba wazungu waingilie kati huu uhuni, na tutawaunga mkono maana serekali haina ridhaa ya umma, bali nguvu za dola ndio zimeiweka madarakani. Hatuna nafasi ya kufanyiwa ghiliba ya uzalendo uchwara na walevi wa madaraka, kwa kisingizio cha nchi huru. Enyi wazungu tunaomba msikie kilio chetu, hili genge la wahuni waitwao CCM wanatushurutisha kukaa madarakani kwa kumwaga damu za wananchi.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,993
2,000
Kuna mtu kaniambia kukosa ustaarabu ndio ushenzi wenyewe. Kwa hiyo Duniani kuna wastarabu na washenzi. Amua mwenyewe nchi yako iko kundi gani.
 
Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
323
500
Wewe unawatetea genge la wakora wa CCM kwa kuleta porojo ndefu, kwakuwa ww na familia yako ni wafaidika wa hii hujuma. Sisi ni watanzania na tunaona hao wazungu wako sawa,na tutawaunga mjini mkono iwapo kweli watachukua hatua kali dhidi ya kundi la wahuni wanaonajisi chaguzi zetu. Msitumie kichaka cha nchi huru kuendesha chaguzi za kishenzi, zilizojaa ghiliba na uhayawani wa wazi, kwa kisingizio cha nchi huru.

Hujuma za zebnu tumeziona toka kuengua wapinzani kwa kutumia sheria zenye nia ovu. Mabox ya kura zilizopigwa tumeziona, tena nyingine zikiwa mikononi mwa vyombo vya dola. Mauaji ya dhahiri ili kuweka madarakani viongozi wasio na ridhaa ya umma, kwa kisingizio cha uzalendo uchwara. Tena ninasikitika sana hao wazungu kutokuwaondoa viongozi wezi wa matakwa ya wananchi ya wananchi kwa kisingizio cha upuuzi uitwao nchi huru. Ule wa juzi haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. 2/3 ya watanzania hawakujitokeza kupiga kura, maana hawaridhiki na mwenendo wa uchaguzi, we unakuja na insha ya nchi huru!

Tunawaomba wazungu waingilie kati huu muhuni, na tutawaunga mkono maana serekali haina ridhaa ya umma, bali nguvu za dola ndio zimeiweka madarakani. Hatuna nafasi ya kufanyiwa ghiliba ya uzalendo uchwara na walevi wa madaraka, kwa kisingizio cha nchi huru. Enyi wazungu tunaomba msikie kilio chetu, hili genge la wahuni waitwao ccm wanatushurutusha kukaa madarakani kwa kumwaga damu za wananchi.
1. Wazungu hao unaoshobokea hawatafanya chochote, kazi kutoa matamko kupitia tweeter na barua za wazi mtandao. Kama wana guts hizo waambie waitishe 'Press' na kutoa matamko live kwenye runinga

2. Kama unashahidi wa hicho unachokielezea ni bora ukatumia haki yako kudai kupitia mifumo sahihi ya kisherai lakini sio kubwabwaja ukiwa umejificha nyuma ya kibodi ya kinakirishi;

3. Kwenye siasa hakuna kitu kinaitwa haki ambayo inapatikana kwenye vyombo vya kisheria tu. Kwenye siasa kilichop ni uhuru, amani na wajibu basi mengine ni kujidanganya mpaka utakasirika hadi kupata sonono bure pasipo faida yoyote;

4. Hakuna sehemu yoyote natetea kikundi au mtu kwenye siasa zenu za 'lumpen'

5. Kama wewe ni mwanasiasa au mshabiki utapata ugonjwa wa moyo pasipo tija wakati wanao pigania vyeo hivyo ni kwa faida zao na sehemu kidogo kukulaghai kwamba anatetea maslahi yako kwa kukusoma kisaikolojia una taka nini hapo ndio unafikiri kinachosemwa ndio uhalisia kwa ajili yako lakini hakuna kitu;

6. Jenga tabia ya kutoonesha hasira zako kwa wengine utafanikiwa sana kufiklia malengo yako tofauti na hapo, yule unayemshawishi akuunge mkono akigundua huna uvumilivu kwenye mchezo wa kuchezean rafu huo atakuadhibu kimyakimya.

7. Bahati mbaya popote duniani hakuna uchaguzi usio wa siri na 'Universal Declaration' inataka chaguzi zote ziwe za siri kuzuia mtu unayedhani atakuunga mkno waziwazi wakati kimoyomoyo hakutaki kugundulika hivyo kutengeza uadui, maana ninyi wanasiasa mna nongwa sana

NB: I am not a politician as you do rather I contribute my opinion based on constructive perspective to pool in the best practice on core values, cultural cycles and diversity civilization.
 
Mkuu hongera kwa kujiunga hapa jukwaani wiki iliyopita, hata kama maoni yako ni Makande yaliyochacha.
 
Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,235
2,000
Demokrasia ni utamaduni wao, tumeiga tu.

Nakitu cha kuiga hakiwezi kuwa perfect.

Tunahangaika kulalamika Demokrasia na uhuru ndani ya taifa hili.Kwenye familia zetu tu tumeliweza??

Wake zetu,watoto wetu tumewapa uhuru na kuna Demokrasia kwenye maaumizi.
 
Ti Go

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
578
500
Wewe unawatetea genge la wakora wa CCM kwa kuleta porojo ndefu, kwakuwa ww na familia yako ni wafaidika wa hii hujuma. Sisi ni watanzania na tunaona hao wazungu wako sawa,na tutawaunga mjini mkono iwapo kweli watachukua hatua kali dhidi ya kundi la wahuni wanaonajisi chaguzi zetu. Msitumie kichaka cha nchi huru kuendesha chaguzi za kishenzi, zilizojaa ghiliba na uhayawani wa wazi, kwa kisingizio cha nchi huru.

Hujuma za zebnu tumeziona toka kuengua wapinzani kwa kutumia sheria zenye nia ovu. Mabox ya kura zilizopigwa tumeziona, tena nyingine zikiwa mikononi mwa vyombo vya dola. Mauaji ya dhahiri ili kuweka madarakani viongozi wasio na ridhaa ya umma, kwa kisingizio cha uzalendo uchwara. Tena ninasikitika sana hao wazungu kutokuwaondoa viongozi wezi wa matakwa ya wananchi ya wananchi kwa kisingizio cha upuuzi uitwao nchi huru. Ule wa juzi haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. 2/3 ya watanzania hawakujitokeza kupiga kura, maana hawaridhiki na mwenendo wa uchaguzi, we unakuja na insha ya nchi huru!

Tunawaomba wazungu waingilie kati huu muhuni, na tutawaunga mkono maana serekali haina ridhaa ya umma, bali nguvu za dola ndio zimeiweka madarakani. Hatuna nafasi ya kufanyiwa ghiliba ya uzalendo uchwara na walevi wa madaraka, kwa kisingizio cha nchi huru. Enyi wazungu tunaomba msikie kilio chetu, hili genge la wahuni waitwao ccm wanatushurutusha kukaa madarakani kwa kumwaga damu za wananchi.
Umemjibu vizuri. Shida Ni pale serikali inapoweka mazingira ya utata. Hivi hujui kuwa hatuna tume huru? Hujui kuwa wagombea Wa upinzani wameondolewa kwa hira? Hujui kuwa uchaguzi Wa serikali za mitaa ziligubikwa Na hilà za kijinga? Hujui kuwa hatuna mahakama huru? Hujui kuwa rais aliwambia wakurugenzi kuwa amewateua Na anawalipa mishahara hawapashwi kutangaza wapinzani wameshindwa? Ndugu yangu hata kama siyo mwanasiasa hili liko wazi, unaliona ila unajifanya huoni!
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
15,869
2,000
Wakuu,

Ni dhahiri kabisa kwa sasa mataifa ya Ulaya na Marekani wamekwisha ona udhaifu wa nchi za kiafrika kutosimamiana yenyewe kwa kuteteana au kuonyana pindi inapotokea chi nyingine nje ya bara Afrika linapoanza ukosoaji kwa kutimia sababu halali lakini malengo ni kinyume chake...
Mkuu Afrika haihitaji chombo chochote hiyo OAU wamekuwepo na hakuna lolote linaloendelea. Waafrika ni lazima wabadilike sisi Tanzania ndio tuwaonyeshe Waafrika wenzetu kwamba uwezo tunao nguvu tunazo na rasilimali tunazo. Simple as that. Unaweza kuona kwamba UK wanapenda kile kinachotokea Kenya kwa sababu Kenyans wanawasujudia na kila kitu wanachowaambia wanatekeleza. Same goes to USA, lakini ukiangalia kiundani kwa nini Kenya wanafanya hivyo ni kwa sababu ya kufikiri kwamba matatizo ya Kenyans yatatatuliwa na Europeans.

Haiwezekani generation after generation tuendelee kuwa watumwa wa wazungu kwenye nchi zetu. Enough is enough hawa walafi wachache wasitucheleweshe kwenye agenda zetu za kulikomboa hili taifa kutoka kwenye makucha ya wakoloni. Ushahidi upo pale JPM alipokataa pesa za IMF/WB wakati Kenya walipewa ili waendelee kujifungia ndani (Covid-19) kufikiri wana mjomba huko nje.
 
Kingkinya

Member
Oct 31, 2020
26
75
Mkuu Afrika haihitaji chombo chochote hiyo OAU wamekuwepo na hakuna lolote linaloendelea. Waafrika ni lazima wabadilike sisi Tanzania ndio tuwaonyeshe Waafrika wenzetu kwamba uwezo tunao nguvu tunazo na rasilimali tunazo. Simple as that. Unaweza kuona kwamba UK wanapenda kile kinachotokea Kenya kwa sababu Kenyans wanawasujudia na kila kitu wanachowaambia wanatekeleza. Same goes to USA, lakini ukiangalia kiundani kwa nini Kenya wanafanya hivyo ni kwa sababu ya kufikiri kwamba matatizo ya Kenyans yatatatuliwa na Europeans...

Tuwe wakweli waafrika hatupendani pia tuna unafiki na wivu mnoo na uroho wa madaraka.Afrika bado inatakiwa kutawaliwa kwa mtazamo wangu.
 
victor siriamaka

Senior Member
Jul 19, 2016
161
250
Mkuu Afrika haihitaji chombo chochote hiyo OAU wamekuwepo na hakuna lolote linaloendelea. Waafrika ni lazima wabadilike sisi Tanzania ndio tuwaonyeshe Waafrika wenzetu kwamba uwezo tunao nguvu tunazo na rasilimali tunazo. Simple as that. Unaweza kuona kwamba UK wanapenda kile kinachotokea Kenya kwa sababu Kenyans wanawasujudia na kila kitu wanachowaambia wanatekeleza. Same goes to USA, lakini ukiangalia kiundani kwa nini Kenya wanafanya hivyo ni kwa sababu ya kufikiri kwamba matatizo ya Kenyans yatatatuliwa na Europeans...
Mbona sijaelewa
 
VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,640
2,000
Wazo jema,waanze na jumuia za kikanda,ila utaona baadhi nchi wakijitoa mfano Tz.Maskini Jaji Kaijage kajipinda kusoma alioandaliwa kusoma.
 
Bajeti ya kunguru

JF-Expert Member
Sep 21, 2014
1,276
2,000
Kwanza haya mambo ya vyama vingi yafe tu haya mambo ya chagua chagua kuna siku azima ya mabeberu itatimia tutabaki tunagombana halafu wao wanachota mali bila hata malipo yoyote.
Magufuli4life
 
JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,143
1,500
Wakuu,

Ni dhahiri kabisa kwa sasa mataifa ya Ulaya na Marekani wamekwisha ona udhaifu wa nchi za kiafrika kutosimamiana yenyewe kwa kuteteana au kuonyana pindi inapotokea chi nyingine nje ya bara Afrika linapoanza ukosoaji kwa kutimia sababu halali lakini malengo ni kinyume chake.

1. Hakuna taifa lolote ndani ya Afrika au Umoja wa nchi za |Afrika unakemea upotofu wa taifa jingine au kutetea udhalilishwaji kutoka wa mataifa makubwa yenye nguvu

2. Kila uchaguzi wa kila nchi unapowadia kila nchi husika, inapaswa pawepo chombo maalumu cha usimamizi wa chaguzi hizo ikishiriana na tume ya nchi hiyo kwa masharti yatakayowekwa kwa mujibu wa sheria

3. Kuhakikisha balozi zinazowakilisha nchi zao haziingilii mambo ya ndani ya nchi husika kinyume na majukumu yao yanayowataka kujadiliana na pande tofauti za kisiasa kabla ya kutoa tamko badala ya wanavyofanya kwa sasa. Ni kweli maeneo ya ofisi na makazi ya balozi au mtumishi yeyote mwandamizi wa uwakilishi huo unasimama kama eneo halali la utawala wa nchi hivyo taratibu za kimataifa zinawajibika kufuatwa ipasavyo

4. Mabalozi wengi kutoa nchi za Ulaya na Marekani kwa sasa wanachochea machafuko ya uasi katika nchi za ukaazi sio kwamba wanazipenda sana nchi za kiafrika, lahasha ila ni kwa maslahi ya kiuchumi ya nchi wanazoziwakilisha au makampuni yenye miradi katika nchi hiyo maaana wanawajibika pia kusimamia;

5. Huko Ivory coast, Nigeria, Uganda nk ambapo ni msimu wa kufanya uchaguzi tayari wanaonesha kupendelea vyama pinzani kwa kutoa matamko bila ya kufanya mawasiliano ya kiitifaki kupata maelezo toka upande wa pili na kushauri badala ya kuonesha kwamba kile walichokipata kutoa upande mmoja uko sahihi kinyume na utaratibu wa haki asili (natural justice whereas nobody should be condemned unheard) This is an obvious breach of diplomatic missions;

5. Nchi za kiafrika hazina umoja la sivyo wangekuwa wametoa tamko kuhusiana na tabia ya mataifa ya Ulaya na Marekani kuingilia mambo ya ndani kwa kisingizio ya kutetea demokrasia na haki za binadamu. Hakuna haki isiyokuwa na wajibu kutoka pande mbili;

Kwanini malalamiko ya kisiasa yanapelekwa kwenye balozi na taasisi za kimataifa wakati tuna sheria zetu kisa ni misaada na mikopo wanayotoa?

Hakuna taifa la Ulaya, Marekani linaloipenda Tanzania au kwamba kuna uvunjifu mkubwa sana wa haki za binadamu kuzidi Marekani ambko hadi sasa wameuwawa watu kadhaa tena weusi lakini hakuna hatua za dhati zinazochukuliwa kudhibiti badala yake wana piga kelele dhidi ya mataifa ya kiafrika kwa tamaa zrasirimali zetu na kuweka watu wao wataofanikisha ukwapuaji.

Waafrika amkeni sasa, kukataa haraka sana vinginevyo itatokea wameshaingia Ikulu wenyewe. Mkifanya hivyo heshima itakuwepo, bila hivyo msahau kuonewa kwa mgongo wa misaada, mikopo kwa kisingizio cha demokrasia na haki za binadamu. Doomsdays are speedily coming to overwhelm african sovereignty.

Nwasilisha
Ww bado ni mtoto na hujui ulimwengu ulikotoka ndio maana maandiko yako hayausiani na ustaarabu wa kilimwengu ndio hujui unaandika nn.Si lazima kuandika hata Kama huna cha kuandika.
 
JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,143
1,500
Halafu unaitwa intelligence justice hebu tendea Haki jina lako hilo.
Ww bado ni mtoto na hujui ulimwengu ulikotoka ndio maana maandiko yako hayausiani na ustaarabu wa kilimwengu ndio hujui unaandika nn.Si lazima kuandika hata Kama huna cha kuandika.
 
JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,143
1,500
Umoja wako wa Africa ulishashindwa kila kitu tatizo letu Africa ni unafiki na ulafi wa madaraka na owongo. umoja ulioshindwa kutatua hata mgogoro mmoja wa Congo jirani zetu hapa ndio unataka kuwavika jukumu ambalo halilingani na umri wao.Vijitu vinatumwa kuja kula posho tu na kulishwa maneno ya kusema.Waafrica wenzetu hata wakinyanyaswa umoja wa Africa hausemi chochote.Baba wa Taifa alisema tabia za kutojali na kuonea onea watu zimebaki Africa na madikteta wamebaki Africa haya ni maneno ya baba wa Taifa letu Mwl.Nyerere.
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
49,613
2,000
Hilo linawezekana...

Lakini hicho chombo kitakua hakina meno wala makali, kama vyombo vya umoja vilivyopo...Cc: mahondaw
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom