Kuna haja mabenki kuweka ATM mpaka vijijini

Mtafiti77

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,843
2,272
Kodi ya mshikamano italeta mapinduzi makubwa katika sekta ya uchumi. Wakati benki ilikuwa ikionekana kama njia isiyo rafiki miongoni mwa Watanzania wengi, sasa inaonekana kuwa tiba mujarab kwenye miamala ya kifedha hasa kutuma na kupokea.

Miamala ya kawaida ya kuhamisha fedha (ndani kwa ndani, yani , toa akaunti ya benki X kwenda akaunti ya benki X) kwa baadhi ya benki ni bure.

Hivyo, wazee wetu kule vijijini watakatwa pesa ya kutolea tu pale ATM ambayo , kwa kulinganisha, si sawa na tozo za Mzee wa kuhamia Burundi.

Ninatambua umuhimu wa katiba mpya
 
High level of illiteracy
Walio wengi watashindwa kutumia zile kadi, ATM machines zitameza sana kadi
Elimu na mazoea tu. Mbona simu wameweza. Na bado wengi wanasaidiwa na vijana wao hata kwa miamala hii ya simu.
 
Kumbe wakati mwingine unakuwa timamu na kuongea/kuandika vitu vya maana, hongera kwa badiko hili kwani uko sahihi. Sasa acha ujinga wako
 
Mabenk yamelala kampuni za simu zikatumia fursa ya kusambaza huduma zao hadi vijijini, badala ya ushindani wanawahonga wanasiasa kupitisha tozo dhalimu Ili kuuwa ushindani.
 
Kumbe wakati mwingine unakuwa timamu na kuongea/kuandika vitu vya maana, hongera kwa badiko hili kwani uko sahihi. Sasa acha ujinga wako
Asante sana. Lakini zingatia mada husika ili kuwepo na ushikamani(coherence). Kuingiza vitu visivyohusika bila ya kuonesha muunganiko ama mtiririko kutaharibu mjadala. 😂Aidha, ujinga ni dhana pana na tata.

Usikute wewe ndiye mjinga, umekosa tu uwezo wa kutambua hilo mkuu.Kuwa makini, si wakati wote unaweza kuwa sahihi mkuu.😂
 
Mabenk yamelala kampuni za simu zikatumia fursa ya kusambaza huduma zao hadi vijijini, badala ya ushindani wanawahonga wanasiasa kupitisha tozo dhalimu Ili kuuwa ushindani.
Hakika
 
Back
Top Bottom