Kuna haja gani bomba la gesi kujegwa kutoka mtwara kuja dar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna haja gani bomba la gesi kujegwa kutoka mtwara kuja dar?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ELIESKIA, Jun 21, 2012.

 1. E

  ELIESKIA Senior Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  huwa najiuliza sana kuna haja gani bomba la kusafirisha gesi kutoka mtwara lijengwe mpaka dar na kutumia gharama kubwa na kutengeneza hatar nyingi. kwann kinachokuja kufanyika dar kisifanyikie huku huko mtwara na hvy kuijenga mtwara na kuokoa fedha nying za kusambaza pipe za kusafishia.tumezoea kurundika kila kitu dar
   
 2. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya ndiyo matatizo tuliyonayo tumeshindwa kuipangilia Dar es Salaam vizuri na kutokana na vitu vya hovyo tulivyovifanya bado tunataka kuongeza matatizo mengine,kwa mfano miundombinu ya maji katika jiji la Dar ni hovyo,barabara nazo ziko hovyo msongamano wa magari usiokwisha kila siku,umeme nao ni usumbufu mtupu.Mimi naungana na mtoa mada kuwa hamna haja ya kulet bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar,kama itakumbukwa vizuri hata watu wa Songosongo walilalamika sana katika mpango wa kuweka bomba la gesi kutoka Songosongo kuja Dar lakini Serikali iliamua kwa makusudi kulileta bomba lile mpaka Dar hivyo kuwanyima fursa kadhaa za kimaendeleo kwa watu wa Songosongo. Mapendekezo yangu ni haya tuache tabia ya kuithamini Dar pekee hata siye watu wa mikoani tunatamani kupata maendeleo kwa rasilimali zinazotoka katika mikoa yetu.
   
 3. B

  Bob G JF Bronze Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wakiamka wananchi wa Mtwara Gesi imekwisa watabaki na historia tu, tulikua na Gesi huku wanapiga miayo
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  ukinijibu kwanini alaska pipeline ilijengwa kuja to the US main nitaona una akili la sivyo naona unatumia siasa zaidi ya theories za uchumi kwako wewe unaona kila bidhaa ya gesi inaweza kutengenezwa huko kwa kuwa mtwara kuna soko! Ninachoweza kukushauri ni ulilie mapato ya gesi hiyo yanufaishe Mtwara na si kwanini bomba linajengwa
   
 5. M

  Makupa JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Fikiri kwanza kabla ya kuropoka, hivi huku mtwara ukiondoa matumizi ya umeme soko la gesi ni sifuri
   
 6. W

  WaMzizima Senior Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni wazi tukufungue macho kidogo hivi sasa mtwara na lindi tayari wana umeme wa kuwatosha unaozalishwa na songas sina hakika ila najua wao wala huwa hawana mgao maana hata huwo umeme hawaumalizi tofauti na sehemu nyingine nchi especially Dar.

  Vilevile viwanda vingi na matumizi yanayohitajika hivi sasa ya gesi yapo Dar ndio maana bomba linajengwa, pindi kusini viwanda vikiongezeka gesi yao itatumika hukohuko kwa sasa waje ije bongo labda mgao utapungua makali kwa kiasi na hio ndio sababu, pure economics, demand and supply.
   
 7. t

  tarizle Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ukweli mtupu...Siasa imewateka zaidi baadhi ya watu mpaka mambo ya kitaalamu wanaona yanakosewa..
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Geza Ulole pipe haijajengwa ila inategemewa kujengwa na sababu zake ni matumizi ya watu ktk miji ya USA wanatumia gas kwa matumizi mbali mbali ya nyumbani, hivyo soko la gas nchini kwao lipo na inahitajika. Ukipiga hesabu usafirishaji na usambazaji wa gas kwa Treni, meli au magari kwa maili 3500 toka Alaska (sijui kwa Afrika ni toka wapi hadi wapi) itakuwa gharama kubwa zaidi ya kuwepo bomba linalosafirisha gas hiyo kukidhi mahitaji kwa miaka 100 ijayo bila wasiwasi.

  Pia kuisafirisha gas kwenda kwa wateja ni rahisi zaidi kupitia bomba kubwa kulingana na mahitaji ya leo na kesho tofauti na sisi tunataka kujenga bomba la gas kutoka Mtwara wakati soko lake ni dogo pia nyumba zenyewe zetu hazijaandaliwa kutumia gas wala hakuna sababu kubwa zaidi ya kuzalisha nguvu za umeme ambazo mitambo hiyo iinaweza kuwekwa Mtwara na zikaunganishwa ktk grid ya taifa. Ujenzi wa bomba la gas kwao ni sawa na kuwepo sewerage system ktk miji yao, tofauti na sisi tunaochimba septic tank au vyoo vya shimo nyuma ya nyumba tukitegemea vijijaa utaita gari la kunyonya..

  Tuna matatizo sana ya utalaam hasa pale logic tu inapotakiwa..na maana husema kwa nini tunajenga barabara pasipo kuweka kwanza mitaro ya majitaka? (sewerage system) kulinda mazingira kiasi kwamba mvua zikinyesha basi barabara hizo huharibika baada ya miaka 5 tu ya ujenzi. Kwa nini tunajenga nyumba zetu bila kwanza kuweka nguzo za umeme, mabomba ya maji na kadhalika isipokuwa vitu hivi hufanyika mwishoni baada ya ujenzi yaani inaonyesha hatuna sababu wala umuhimu wa kuwa na umeme wala maji iwe huduma ama kibiashara.
   
 9. w

  wikolo JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wanafanya hivyo kwa sababu ya ubinafsi tu. Wakubwa wote wanakaa huko DSM na laiti kama wangekuwa wameshahamia dodoma nadhani wangelipeleka huko kwa sababu hizo hizo zinazowafanya walipeleke Dar sasa! Kwani ni kwa nini serikali haijahamia dodoma hadi leo? Ni kwa nini wanajenga daraja la kigamboni kwa mabilioni wakati reli yetu ya kati ni mahututi? Nina kwa nini nyingi sana ila ngoja tu niishie hapo manake nahisi hasira.
   
 10. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  Alaska's oil pipeline marks 35-year milestone


  Posted: June 21, 2012 - 12:04am

  [​IMG]
  FILE - In this 2007 file photo, a new oil transit pipeline runs across the tundra to flow station at the Prudhoe Bay oil field on Alaska's North Slope. The oil pipeline that stretches 800 miles across the Alaska landscape is celebrating a milestone. The trans-Alaska oil pipeline on Wednesday marked 35 years in production with more than 16.5 billion barrels of oil loaded into the pipeline at Prudhoe Bay for delivery to Valdez, where it is loaded intotankers destined for the West Coast. (AP Photo/Al Grillo, File)
  By Mary Pemberton
  THE ASSOCIATED PRESS
  ANCHORAGE - The engineering feat that is the trans-Alaska pipeline is celebrating a milestone.
  On Wednesday, the 800-mile pipeline marked 35 years of production with more than 16.5 billion barrels of oil loaded at the North Slope's Prudhoe Bay oil field for delivery to Valdez at the line's southern end. There, tankers leave Prince William Sound and head for West Coast refineries.
  It was June 20, 1977, when oil was loaded for the first time into the pipeline, also known as TAPS. It arrived in Valdez - the country's northernmost ice-free port - 38 days later.
  "The pipeline is an engineering marvel, but it's the TAPS workforce who has kept oil moving for 35 years," Alyeska Pipeline Service Co. President Tom Barrett said in a statement.
  The pipeline now accounts for 11 percent of U.S. domestic oil supply.
  The company has more than 2,000 employees and contractors whose job is to keep the oil safely flowing through the pipeline. Twenty-nine employees have been on the job since the start, Barrett said.
  Two oil companies, Atlantic Richfield Co. and Humble Oil and Refining Co., announced oil in a discovery well at Prudhoe Bay on March 13, 1968. Almost a decade later, after building a pipeline that crosses three mountain ranges, 34 major rivers and numerous earthquake fault lines - and spending $8 billion in what was the world's largest privately funded construction project - the oil began flowing and kept flowing with the discovery of more oil in more fields on Alaska's North Slope.
  Engineering work and construction of the pipeline moved at an astonishing pace. The pipeline was finished in just three years and two months. It began in April 1974 and finished in June 1977, with more than 70,000 people working on it. Thirty-two people died during construction.
  About 75 percent of the pipeline passes through permafrost, land that is perpetually frozen. That posed engineering challenges for the designers of the pipeline. While permafrost in some areas was just a few inches deep, it was more than 2,000 feet in another.
  The 800-mile pipeline route required that the pipeline be placed above ground on an elevated support system to avoid melting the permafrost. In areas where the land was unfrozen, the pipeline was buried. Some permafrost areas required the construction of special below-ground sites for highway, animal crossings, or to avoid rockslides and avalanches.
  When the oil flowed, so did the money, creating heady times for many Alaskans. Some were new arrivals, lured by the promise of good-paying jobs.
  Alyeska Pipeline Service Co. employee Mel Jessee was 20 when he began working for the company. He remembers piles of pipe stored in a large yard in Fairbanks in 1974 and hotels being built as fast as crews could put them up.
  Fairbanks was just a small frontier town then, but it quickly filled with people there to build the pipeline. Welders came from Louisiana and oilmen from Texas, Jessee said.
  "It was hard enough to understand them but they were folks who knew what they were doing," he said.
  Jessee still marvels at the engineering solutions for complex problems, such as using a zigzag design to allow the pipeline to expand in the summer and contract in the winter.
  "It didn't seem possible, but somehow they got it done," he said.
  Alaska remains heavily dependent on the pipeline and the money it generates from transporting North Slope oil. It has no state income tax.
  The pipeline is owned by a consortium of companies. It was designed to withstand powerful earthquakes, and did just that on Nov. 3, 2002, when a 7.9-magnitude earthquake centered about 50 miles west of the pipeline shook near Denali National Park.
  The ground along the fault moved an estimated 18 feet horizontally and nearly 2.5 feet vertically. The quake was so strong that it opened cracks 6 feet wide in roads and rocked boats on lakes as far away as Louisiana.
  Yet, the 48-inch diameter pipe did not rupture.
  There have been hundreds of oil spills since the pipeline started up in 1977, especially in the first two decades of operation. The number of gallons spilled since the mid-1990s has been greatly reduced, with no spills recorded in 2004 and 2005.
  The worst year was in 1989, when the Exxon Valdez oil tanker ran aground on Bligh Reef in Prince William Sound and spilled nearly 11 million gallons of crude. It was the nation's worst offshore oil spill until the 2010 blowout of a BP well in the Gulf of Mexico.
  Another bad spill year for the Alaska pipeline was in 2001, when a man shot the pipeline, spilling 258,000 gallons of oil onto the tundra.
  The pipeline is aging, along with the Prudhoe Bay oil fields. That means the amount of oil flowing through the pipeline is declining as oil reserves on the North Slope are drawn down. Oil through-put peaked at 2.1 million barrels a day in 1988. It averaged about 590,000 barrels a day last year.
  Alaska's oil pipeline marks 35-year milestone | Juneau Empire - Alaska's Capital City Online Newspaper
   
 11. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Mbona kinachozungumziwa hapa ni mafuta badala ya gesi ambayo ni mada kuu!
   
 12. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Jibu hoja na si kuleta maswali ya ajabu, yaani kila kitu ni kufyonza tu
  kwa mirija na kunufaisha mikoa mingine huku ile inayoitwa ya pembezoni
  ikiendelea kuchekwa. Jibu hoja na si kuleta maswali yenye muelekeo wa
  Chuki!
   
 13. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  mafuta na gesi yana tofauti gani katika matumizi? Khaaa watu wengine bwana? wewe katika mabwege ni wa kwanza nathani..! sorry lakini i did not mean to insult u! kwa uelewa wako, hivi unadhani hilo bomba likijengwa na mafuta yakagundulika litashindwa kupitisha mafuta hayo pia? na unapoongelea kwanini linapelekwa dar jaribu kufikiri hata kwa sekunde kwamba ni matumizi yake ndiyo yanaongelewa hapa!
   
 14. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Nakuomba utukane sana kwasababu ni hulka yako! Kwanini unatoa matusi wakati mimi sikukutukana? Tabia ya mtu inaonekana kwa matendo yake na jinsi asivyofunzwa vizuri na wazazi wake. Jirekebishe, unawaaimbisha wazazi wako na huenda wanajilaumu kwanini walikuleta duniani kwa tabia yako hiyo ya kibwege!
   
 15. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  jifunze kwanza kwanini umeme ule mdogo wa Songas umeshindwa kutumika huko Mtwara! na kwanini kuna watu wachache zaidi ya Dar! Na kama Marekani tajiri kuliko nchi nyingine yoyote walijenga trans Atlantic pipeline na si kulazimisha matumizi ya mafuta huko, Tanzania ndo itaweza? Ninachoweza kukuambia opportunity haisubiri! Mtwara inahitaji revenues za gesi kujiendeleza na si kusema gasi isisafirishwe kwenda kwingine! Nadiriki kusema uelewa wako ni mdogo sana kwa haya maswala!
   
 16. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Unaweza kuwa uko sahihi lakini ninachozungumza hapa
  ni majibu ya Hoja. Mtu badala ya kujibu anaanza kuponda
  na kulaumu mtu aliyeleta Mada kwa mfumo wa swali. Jibu ni
  kwanini imetokea hivyo?
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo unazungumzia OIL pipeline na sio Gas pipeline!
   
 18. unju bin unuki

  unju bin unuki Member

  #18
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Achenui mambo zenu inaweza kuzalishwa huko huko,hata umeme unaweza zalishwa huko na ukaingizwa ktk hiyo mnayoita gridi ya taifa,viwanda vya cement vinajengwa huko kama hauna habari its just the begining.
   
 19. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2012
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tuacheni akili za kizamani. Kila kitu lazima kije
  Dar.kama shida ni soko, Oryx wanabomba wapi Dar?na kila siku wanaleta mitungi ilojazwa gesi toka nje.kama ni viwanda vingapi vina mfumo wa kutumia hiyo gesi?
   
 20. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  tofauti nayojua mimi kati ya gas na oil ni combustion efficiency na physical form (one liquid while another gas) itokanayo na CH ratio! Lakini on economic sense pipeline ya oil inaweza kutumika kupitishia gas ndo maana nimetumia mfano huo! na pia on compression gas inaweza kuwa liquefied! Mjaribu kujiuliza kwanini mtu anafananisha the two jibu ni kwa vile logistics zake zinafanana
   
Loading...