Kuna baba mwenye nyumba...hakuna baba mwenye gari....!!

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
Maisha yanaenda yakibadilika, huko nyuma tuliowahi kuzaliwa, M/MUNGU akikujaalia kupata kibarua, jambo la kwanza utatafuta kiwanja, kumezuka mtindo miongoni mwa vijana wengi wa sasa kuanza na kununua gari huku anakaa nyumba ya kupanga, gari anailaza CCM, akija mjini kuna parking za kulipia........!! gari ni mzigo. kupanga ni kuchagua bali chagua mzigo mwepesi ili safari iwe rahisi kwako.
 
we leo umeamka vibaya nini?au kuna jamaa kakupita bila kukupa lift ndo umeamua kumdiss hapa jf!kununua gari au kuwa na nyumba ni uamuzi wa mtu binafsi!
 
Ni kweli mkuu ndivyo ilivyo kuwa. Those days kupata gari ilikuwa very expensive,Leo ukiwa na milion 4, unapata gari. na pesa zilikuwa ngumu kuliko ilivyo leo. Ujenzi ni long term investment inayohitaji pesa nyingi na usimamizi wa hali ya juu. sasa usipo kuwa na uwezo wa kufika site on time huwezi kujenga ktk ufanisi ule. Hivyo usafiri unakuwezesha kufanya yote. Kwa sasa gari ni kitu cha lazima ili uweze kufanya mengine kwa haraka na ufanisi. Nadhani swala labda iwe ni aina gani ya gari.
 
we leo umeamka vibaya nini?au kuna jamaa kakupita bila kukupa lift ndo umeamua kumdiss hapa jf!kununua gari au kuwa na nyumba ni uamuzi wa mtu binafsi!

Mkuu, ni kweli kununua gari au kuwa na nyumba ni uamzi wa mtu binafsi, hata kujiua ni uamzi wa mtu binafsi; lakini unauonaje uamzi huo? Mzuri au mbaya? Tafakari kwanza kabla hujaamua, na ninafikiri mtoa hoja ndicho alichokuwa ana maanisha.
 
Yeyekama hana gari ni shauri yake, aacha kumwaga mapovu hapa. Swala la uamuzi kuwa mzuri au mbaya, ni la mtu binafsi na utashi wake.
 
kuwa na gari ni muhimu ila inategemea aina ya gari na gharama zake, mfano utakuwa huna akili timamu kama utanunu gari ya ml 40 na unaishi nyumba ya kupanga, kama ni ya ml 4 its ok,
 
Nyumba ni ghari kuliko gari,ingawa inategemea na unajenga wapi! Mtaani mwenye gari anajulikana kuliko mwenye nyumba..kama ulivyosema awali kupanga ni kuchagua..unaweza ukawa na gari la milioni saba..ambayo ni gharama ya kiwanja sehemu fulani,tafakari!
 
Yeyekama hana gari ni shauri yake, aacha kumwaga mapovu hapa. Swala la uamuzi kuwa mzuri au mbaya, ni la mtu binafsi na utashi wake.

Nafikiri, hoja imekugusa. Yamwagike mapovu au maji ukweli unabaki pale pale na kizazi kinachoamua mambo kijinga jinga kitatengeneza historia yake na mwisho kitaishia kusema tulisikia wakisema kuna baba mwenye nyumba na si baba mwenye gari.
 
Nyumba ni ghari kuliko gari,ingawa inategemea na unajenga wapi! Mtaani mwenye gari anajulikana kuliko mwenye nyumba..kama ulivyosema awali kupanga ni kuchagua..unaweza ukawa na gari la milioni saba..ambayo ni gharama ya kiwanja sehemu fulani,tafakari!

Ukijulikana una gari na unaishi kama ndege leo hapa kesho pale kwasababu tu mazingira hayajaku-favour, itakusaidia nini? Bila shaka mwisho hata wale wasiokuwa wanakujua kuwa una gari wanaweza kukucheka!

Pale Dodoma nikiwa katika shughuli zangu za utafiti nilishuhudia mzee mmoja anatolewa vyombo katika nyumba ya kupanga ingawa alikuwa na gari vile vyombo akaviweka ofisi ya kitongoji, na ikamchukuwa siku tatu kupata nyumba nyingine. Si aibu hiyo? Tubadilike tuwe kama enzi za mtoa hoja.
 
Nafikiri, hoja imekugusa. Yamwagike mapovu au maji ukweli unabaki pale pale na kizazi kinachoamua mambo kijinga jinga kitatengeneza historia yake na mwisho kitaishia kusema tulisikia wakisema kuna baba mwenye nyumba na si baba mwenye gari.

Wewe jipange nunua gari na wewe. Hayo mengine ni yako na wajukuu zako. Unataka kulazimisha uonavyo wewe kuwa ndo Sheria??

Watanzania tuna tabia ya kupenda kuangalia maisha ya watu wengine na kuanza kukosoa, badala ya kuangalia maisha yetu binafsi na kusonga mbele. hapa duniani kila mtu ana maisha na maamuzi yake mradi havunji sheria, kuna dada anamlaumu kaka yake kwa nini aliamua kuacha chuo mjinga sana yule wakati yeye mwenyewe hata form four hakumaliza, huyu mwingine analaumu watu kununua gari badala ya kujenga utakuta yeye hana hata kimoja na hata kama anavyo vyote ishi maisha yako achana na ya wengine hayakuhusu.
 
kila mtu na maisha yake.......

Mambo yanabadilika tofauti na zamani.......

Zamani nyumba ya nhc upanga ulikuwa unapata, siku hizi zimekuwa za wahindi...... Vijana inawalazimu waishi kibamba riziki wanaipatia posta mpya, gari siku hizi lina umuhimu wake.... Na nyumba pia muhimu hivyo mtu anajipanga kadri awezavyo......
 
Kikubwa ni kitu gani kinaweza kupatikana kwanza kirahisi na kulingana na hitaji lako.
Kwa mfano nimepewa nyumba na shirika ila sijapewa gari na ninauwezo wa kununua kwa nini nisinunue gari?
Au natumia gari ya kazini na nimepanga kwa nini nisianze kaujenzi mdogo mdogo?
Haya yote hutegemea hitaji la mhusika kwa muda muafaka.
 
jina la mleta uzi ni sinafungu sasa mnapoteza muda wa nini jamani?

hahahaha, kwa hiyo ni fungu la kukosa ama hata hapo hayupo?

But nikiwa na gari naweza kwenda nitakapo pasi shida,
madem nakamua kila kituo toka mbez hadi posta,
sijui mvua wala jua wala vumbi.
Nguo hazipauki na uso haupauki kwa jua
sina karaha za kuganda na bomba wala kunukiwa vikwapa na vijambo
na baba mwenye nyumba ana niita baba kisa lift.
Kama ishu ni mjengo hata ule wa tani saba(kaburi) nao ni mjengo.
Halafu mtu anakwambia kuna uzee kweli lol.
 
Gari lina heshima yake hapa mjini!

Kwahiyo lengo ni kutafuta heshima? Ama kweli!! Tafuta uone kama kuna mtu anaitwa kwa heshima baba mwenye gari.

OK, labda niseme unamtazamo mdogo sana ikiwa ndivyo haswa unakimbilia heshima za muda na kijinga kwa vitu vya mpito. Kuna tofauti gani kati yako na mlevi anayeuza nyumba na nusu au pesa zote anatumia kunywea pombe ili apate heshima baa?
 
Back
Top Bottom