Kuna baba mwenye nyumba...hakuna baba mwenye gari....!!

Watanzania tuna tabia ya kupenda kuangalia maisha ya watu wengine na kuanza kukosoa, badala ya kuangalia maisha yetu binafsi na kusonga mbele. hapa duniani kila mtu ana maisha na maamuzi yake mradi havunji sheria, kuna dada anamlaumu kaka yake kwa nini aliamua kuacha chuo mjinga sana yule wakati yeye mwenyewe hata form four hakumaliza, huyu mwingine analaumu watu kununua gari badala ya kujenga utakuta yeye hana hata kimoja na hata kama anavyo vyote ishi maisha yako achana na ya wengine hayakuhusu.

Hapo kwenye bold kunanifanye nikuone wewe kuwa ***** mtoozeni. Kwahiyo ulitaka afurahie? Hujagundua kuwa huyo dada amejifunza kwa vitendo hasara ya kutomaliza form four sasa hafikirii na hapendi mtu katika familia yao kufanya kosa kama lake ktk familia kulifanya. Halafu unayejiita GT, unaunga mkono kuacha chuo, zuzu kweli.
 
Gari waeza nunua kwa muda mfupi na kuanza litumia, nyumba kama ni ya kujenga mpaka kuishi utachukua muda mrefu na waweza maliza pesa kabla ya nyumba yenyewe kumalizika. Ni vema kama una "cash" nunua nyumba iliyojengwa tayari.
 
Hivi ni kweli chi zilizoendelea,kwa % kubwa watu nyumba nyingi (ambao wanazo)ziko kwenye mikopo na wanaweza kumaliza mikopo either wanakaribia kufa au katika miaka ya 60's au 70's?wa Tz wengi wanajenga kwa cash ambayo ukiichunguza loooooh!:amen:
 
Gari waeza nunua kwa muda mfupi na kuanza litumia, nyumba kama ni ya kujenga mpaka kuishi utachukua muda mrefu na waweza maliza pesa kabla ya nyumba yenyewe kumalizika. Ni vema kama una "cash" nunua nyumba iliyojengwa tayari.

............kujenga ni mateso, haswa kwa kutumia mshahara ! miaka10 au 15 wewe na ujenzi tuu ! huna muda wa kuenjoy maisha. Labda uwe Mhasibu wa Halmashauri au wa Tanesco ndo utaenjoy !
 
Wote tukijenga nani atapanga? Sio lazima wote tuwe baba wenye nyumba, acha wengine tubaki wapangaji,, muhudumu leta ndovu baridiiii.... Wambie na jikon walete mchemsho
 
Kwani mtu kuitwa baba mwenye nyumba kunamsaidia nini mwenye nyumba? Anafaidika nini kuitwa baba mwenye nyumba? Sio kila mwenye nyumba anaitwa baba mwenye nyumba maana sio wote wazipangisha nyumba zao. Mleta maana inaonekana unapenda ujiko toka kwa wapangaji wa nyumba na sio wewe kufaidi kuwa kwenye nyumba yako. Kuna watu wanaitwa baba mwenye nyumba lakini wanaishi nyumba za kupanga. Hii inaama naye huko anakoishi kuna boss mwenye nyumba. Kuwa nyumba, kutokuwa nayo, kuwa na gari, kutokuwa nayo ni life style tu.
Kuna nchi hasa zilizo endelea hakuna mtu anaruhusiwa kujenga nyumba, nyumba zote zinamilikiwa na serikali (mashirika ya nyumba) na raia wote ni wapangaji.


Hii maada inanikumbusha ujinga fulani eti ili uoe mke lazima uwe umejenga nyumba. Watu wanaoa kwanza halafu wanasaidiana kujenga. Hakuna shida mambo yanakwenda
 
Maisha yanaenda yakibadilika, huko nyuma tuliowahi kuzaliwa, M/MUNGU akikujaalia kupata kibarua, jambo la kwanza utatafuta kiwanja, kumezuka mtindo miongoni mwa vijana wengi wa sasa kuanza na kununua gari huku anakaa nyumba ya kupanga, gari anailaza CCM, akija mjini kuna parking za kulipia........!! gari ni mzigo. kupanga ni kuchagua bali chagua mzigo mwepesi ili safari iwe rahisi kwako.
Papaa Sinafungu,
Huu ni mwaka 2012 mambo na maisha kwa ujumla yamebadilika sana. Na uhakika enzi za ujana wako soda ilikuwa inauzwa shilingi 5(tano) na leo ni sh 600-700. Kuna watu Kama wewe mnaotegemea watu wengine waishi kutokana na jinsi ulivyoishi. Kumpangia mtu afanye nini na kipato chake sio Jambo la busara. Kununua gari huku ukiwa unakaa nyumba ya kupanga ni uamuzi binafsi. Siku hizi kuna mpaka baba bajaj na baba bodaboda. Usiumie roho Kama mtoto wa dada yako kanunua gari huku mjomba bado unagombania mabasi kwa kupandia dirishani.

Then again hilo Jina lako "Sinafungu" explains it all.
Kila la heri mkuu.
 
Back
Top Bottom