Kuna anayeelewa kibonzo hiki kinamaanisha nini?

Boniphace Bembele Ng'wita

JF-Expert Member
Dec 25, 2013
3,437
1,786
Edfisadi(2).jpg


Huyu mwandishi wa Nipashe kaweka kibonzo hiki, je kunaanae muelewa? Ana maana ipi?
 
Maana yake watakaomizwa na utumbuaji majipu ni mabosi wa kati lakini wale mafisadi wanaowatuma na kuwatumia sms wataendelea kupeta. Mfano wale walioambiwa wasafishe hospitali.
 
Je! Vipi kuhusu kifaa anachotumia kukata huo mnyororo? Msumeno ni valid kwa kazi hiyo kweli?
 
Kwa jinsi nilivyokielewa hiko kibonzo

Kwanza JPM hajakaa mkao sahihi wa kukata huo mnyororo,alitakiwa ashuke chini[atoke kwenye huo mlingoti] na kusimama,lakini hajafanya hivyo

Hii inatuonyesha kuwa,JPM anahubiri mabadiliko wakati bado yupo kwenye chama kilichokataa mabadiliko

Pia msumeni alioushika ni butu,hii inamaanisha kuwa watendaji kazi wake[Baadhi ya mawaziri mfano nape] hawafai


Pia ameshika msumeno kwa mkono wa kushoto,huku mkono wake wa kulia uking'ang'ania kwenye nguzo

Kwa jinsi alivyoushika,hatoweza kuukata,bali anachofanya ni kuuvuta kwake huo mnyororo

Wakati huohuo,mtanzania anajitahidi kutoka pale alipofungwa
So anakuwa kama anamkaba fulani

Huo mnyororo=umaskini
 
Anakata mnyororo kwa msaada wa nguzo ambayo imesimikwa na mfumo wa kifisadi.
The way anakata hatafanikiwa kwa sababu hana balance.Hiyo miguu ikichoka kila mtu anajua kitakachofuata.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom