Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Hapo kwenye bold ni kweli kabisa. Ukisubiri maish aboa yakukute kitandani wakati umelala basi utasubiri sana.Serikali yeyote hata bila Kikwete kuahidi maisha bora inachofanya ni kuweka mazingira wezeshaji ( sijui kana ni kiswahili sanifu kwa enabling environment) ili mtu anaye jibidiisha aweze kufanikiwa. Cha kujiuliza ni kuwa je Kikwete aliweka mazingira wezeshaji kipindi chake tofauti na vipindi livilivyopita?
Huwezi kuendelea kama mazingira yanayokuzunguka hayakuwezeshi kujiendeleza. Huwezi kujiendeleza kama u mgonjwa na hupati dawa, huwezi kujiendeleza kama hupati elimu nzuri, hata kama una akili vipi. Mazingira mazuri ya kujiendeleza lazima yawepo, na hilo ni jukumu la serikali iliyopewa dhamana na wananchi. Hebu tujiulize, kazi ya serikali ni nini?