Kuna aliyeamini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna aliyeamini?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyani Ngabu, Sep 4, 2010.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Sep 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Hivi mwaka 2005 Kikwete alipoahidi maisha bora kwa kila Mtanzania, kati yetu humu kuna aliyemwamini kweli au niko peke yangu tu ambaye sikuamini hayo?
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nilidhani walau angefanya kitu cha kuridhisha. Lakini baadaye nilipoona mbwembwe nyingi, hasa alipoanza kuchota hela za hazina nilikosa matumaini. Mabilioni aliyoyachota hazina eti kusingizia kupeleka maendeleo mikoani hadi leo ni siri wanaoijua wenyewe. Kwani baadaye zilifuata hadhi ndefu hadi walengwa walikosa matumaini. Nahisi kwa asilimia kubwa zilirudi mikononi mwa mafisadi.

  Ndiyo maana katika kampeni zake kote alikopita hakutaja kuhusu hiyo hela aliyoitoa hazina kwa mbwembwe kubwa.

  Angekuwa na nia njema na kuisimamia nia yake hiyo ile hela aliyodai ni ya kutoa ajira kwa vijana ingetosha kumrudisha madarakani, bila kuhitaji kampeni kubwa wakati huu kwani yote yangekuwa dhahiri. Wengi wangeona ni rais wa Maendeleo.

  Lakini ni bahati mbaya tumeambulia usanii mtupu.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Maisha bora unajiwekea mwenyewe, Chama/serikali vipo kukuwezesha kufikia hayo maisha. Binafsi niliamini hivyo na nina uhakika wale waliotaka maisha bora wameyapata.
   
 4. B

  BRIA Senior Member

  #4
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Ndo watu wanahoji huo uwezeshaji wa kikwete na serikali yake ama kweli..Ndo mana amewawezesha Mwarabu wa Igunga na nduguze Jeetu Patel,Chavda na wewe fisadi by the way HAKUNA UWEZESHAJI BALI UWEWESESHWAJI
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Sep 4, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nilipata bahati ya kumfahamu Kikwete kabla hajaingia madarakani. Sifa mojawapo kubwa sana kwake ni ujuzi wa kushawishi, na moja ya weaknesses zake kubwa ni ile tabia ya kushawishi kwa kuahidi jambo lolote analodhani litasikilizwa hata hana kama uhakika nalo. Tabia zote hizo mbili alikuwa anazitumia sana hasa kwa akina dada waliokuwa majirani zangu kule Sinza.

  Mwaka 1995 alipogombea nilikuwa ninaamini kuwa hangefika popote kwa sababu nilidhani kuwa NEC ya CCM ina watu wenye busara ambao wangeweza kuona weakness zake mapema, ila nilishangaa kusoma kuwa jamaa alishinda ila akaenguliwa na watu wachache sana wenye busara zaidi. Sasa alipogombea tena mwaka 2005, niliunganisha tena tabia hizo zote mbili halafu na ile irresponsibility aliyokuwa akionyesha kwa wale akina dada majirani zangu wa zamani pale Sinza, na kuangalia tena rekodi yake ya miaka 10 aliyokuwa Mambo ya Nje, nikasema wazi kabisa pale Business Times Forum kuwa hapa tunanunua kofia ya polisi. Ninafurahi kuwa nilikuwa ni mmoja kati ya wachache waliotambua mapema sana janga la kumpangisha jamaa huyu kwenye kasri letu la Magogoni kabla hata hajasaini mkataba.
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nilimwamini kwa asilimia 60%, nikitumaini ataweza kubadilika na kuwa mzalendo wa kweli kwa raslimali za Taifa. Lakini wengi walimwamini kwa asilimia 100% kutokana na hulka yake ya ushawishi mkubwa.

  Ni vyema kuangalia nyuma na kupima mafanikio, lakini kwa vile tuko kwenye mchakato mwingine, swali kwa sasa ni:

  Je, kuna watakao mwamini?! Nini kifanyike kuwajuza Watanzania kutokuwa na imani naye kama mimi na wewe, ilivyo 2005 hata 2010?!
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mkuu unaelekea sipo
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Tafadhali usifanye kufuru na kutukana Watanzania wengi ambao wanaishi maisha duni siku hadi siku! Wale ambao wamepata maisha bora wapo katika kundi la kufisadi mali za Tanzania, na ni hao hao wanaojitahidi kuitetea ccm ili wazidi kudhulumu wananchi. Siku za kufisadi zimekwisha, na hakika Tanzania haitakua ile ile baada ya October 31 2010.
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Maisha bora unaletewa nyumbani kwako, au ni baada ya mtu binafsi kujishughilisha?

  Kinachotakiwa ni kwa watanzania wote kwa ujumla kuamka na kutafuta hayo maisha bora. Haiingii akilini kusubiri maisha bora kwenye kibanda chako kama hutaki uwe na maisha bora!
   
 10. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  No mimi sikumuamini tangu nateuliwa na ccm. Kwani hakuna nilichokiona alichofanya wakati akiwa na nyadhifa mbalimbali.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Sep 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  So are you saying that today we are better off than we were five years ago?
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Sep 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Hata mimi sikumwamini na wala sikuona potential yoyote.....kwa hiyo nilimpinga kwa asilimia 100.
   
 13. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  ======

  Kumbe kulikuwa na sababu gani ya yeye kusema ataleta maisha bora kwa kila Mtanzania ikiwa kila mtu ni kujishughulisha?

  Ninafurahi sikuwa mmoja wa waliomwamini. Nilikutana naye Morogoro akitafuta kura za kishindo nikamweleza, ya kwangu haimo katika hizo, akaniuliza kwa nini? Nikamjibu, wagombea ni wengi, afadhali wagawane kuliko mmoja kuchukua zote. Kama kawaida yake akacheka, nikaondoka.
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Much better, na hii inawahusu wale ambao wameamua kuwa na maisha bora.

  Mkuu NN, kumbuka kuwa JK aliwezesha asasi zote zenye kushughulika maisha bora kufanya hivyo. Hivyo jukumu liliobaki ni kwa wananchi kupata maisha hayo kupitia asasi hizo, na sio kukaa majumbani mwao kusubiri kuletewa maisha bora.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Sep 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Duh!! hii kali sasa.....Sikonge, Mwafrika, na Rev. Masanilo hebu tuwekeeni zile picha za maisha bora kwa kila Mtanzania....e.g. zile za wale madogo waliokaa chini darasani au zile za akina mama wajawazito na wale walijifungua kulala sakafuni.....
   
 16. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Huwezi kuzungumzia maisha bora wakati inflation imepanda mpaka kufikia double digit. huwezi kzungumzia maisha bora wakati utekelezaji wa utawala bora uko low. Huwezi kuzungumzia maisha bora wakati kiongozi mkuu anasema waziwazi nimewasamahe wezi wa mali za umma. Naweza kukubalina an wewe kuwa mafisadi ndio wameweza kuwa na maisha bora kwa kipindi hiki kwa kuwa wao ndio wameweza kuchota mapesa na wanaweza kutamba na kutumia without feeling the pinch of inflation or even without fear of being arrested for crimes they committed and which they are still committing.
  Unatakiwa uwe na matatizo mkaubwa sana akilini mwako kuamini kuwa katika miaka mitano tumekuwa na miasha bora.
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kwa ufahamu wangu, asilimia kubwa ya watz wanaishi vijijini, ambako shughuli nyingi za maendeleo yao zinapita kwenye kamati za maendeleo za maeneo hawa angefuta utaratibu wasingekumbana na kadhia hizo.

  Picha za kinamama waliolundikana kwenye wodi za uzazi, zimetoka DSM, ambako wengi amehamia jijini humo pasipo sababu za msingi. Hii haijalishi usalama wao wa kujifungua katika mazingira muafaka. Tatizo hapa ni kuzidiwa kwa vituo vya afya kutokana na uhamiaji wa watu hao.

  Nchi yetu inajengwa na kata, tarafa, wilaya na mkoa. Iwapo wilaya ama kata inakuwa na tatizo fulani, mwenye jukumu la kuondoa tatizo hilo ni wale ambao wanaishi kwenye eneo hilo. Iwapo wao binafsi kulundikana kwenye hospitali sio tatizo kwao, hata ije serikali yoyote ile tabia ya kulundikana haitoweza kubadilika.

  Maendeleo ya wananchi yatatokana na kero ambazo wanaziona, kupita kamati zao wanauwezo mkubwa wa kuondoa kero hizo. Matatizo makubwa miongioni mwa wananchi ni ujenzi holela(hii ni kutokana na uhamiaji holela), taka ngumu na taka maji, shule, zahanati, n.k

  Iwapo katika level ya kata wataweza kujua kero zao, hapana shaka kutakuwepo na unafuu mkubwa katika ngazi ya wilaya na mkoa vilevile.

  Wakati wa kusubiri kupangiwa kila kitu na serikali kuu umepita, ni jukumu la wananchi kujipangia vitu wanavyotaka katika maeneo yao, ili kuboresha maisha yao ya kila siku.
   
 18. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Na nyinyi hamuchoki na Kikwete! Kikwete! Slaa! Slaa!

  Hakuna jipya kati ya hayo munayoyaleta kwa headings nyingi nyingi tafauti. Hebu wapumzisheni kidogo na sisi tupumzike na topics hizo.
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye bold ni kweli kabisa. Ukisubiri maish aboa yakukute kitandani wakati umelala basi utasubiri sana.Serikali yeyote hata bila Kikwete kuahidi maisha bora inachofanya ni kuweka mazingira wezeshaji ( sijui kana ni kiswahili sanifu kwa enabling environment) ili mtu anaye jibidiisha aweze kufanikiwa. Cha kujiuliza ni kuwa je Kikwete aliweka mazingira wezeshaji kipindi chake tofauti na vipindi livilivyopita?
   
 20. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hivi kweli ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania iliahidiwa kwa condition ya kujibidisha kila mtu binafsi? au ilikuwa open promise kwa maana kwamba resources zetu zitaelekezwa kuleta hayo maisha bora, shule nzuri zitajengwa na walimu bora wataandaliwa? Hospitali kila kijiji zitajengwa na dawa zitapatikana? Umeme utafika kwa kila kijiji ili kila mtu aunganishe akipenda? barabara zitajengwa, mazao ya wakulima yatapata soko zuri bila kukopwa malipo? Sasa tujadiliane katika muktadha wa ahadi yenyewe na siyo maneno matupe yaliyobeba ushabiki na ujanjaujanja tu. Kikwete alidanganya watu na hana kipya atakachoweza kuahidi sasa na mimi nikamwamini tena. Hongera wewe bado una imani kubwa naye!1 Sijui inatokana na nini..wewe unajua zaidi kuliko mimi.
   
Loading...