Kuna aina mpya ya utapeli umeingia Dsm na mikoani chukueni tahadhari

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Kwa mnaofanya biashara iwe za maduka,usambazi, za online na mnaofanya Delivery.
Ipo hivi mtu anakupgia simu anasema ameona umepost bidhaa fulani au anapiga simu anasema anahitaji bidhaa fulani kutoka Dukani kwako

Tena anasisitiza apelekewe na boda na gharama za kudeliva atalipia yeye mwenyewe.

Wewe unaenda kufanya delivery au unamtuma boda njiani anapiga simu anaomba mtu amnunulie umeme aende nao maana alipo yupo mbali na wanapouza umeme then ukifika utampa hizo token na wewe atakupa hela yako

Unaona kwa kua humpi token utaenda kumkabidhi ukifika ngoja ushuke ununue umeme, anakutumia namba ya mita unaenda wanapouza umeme!!Unaambiwa namba ya mita haijatimia

Unampigia anakuambia namba ya mita ni kweli haijatimia hivyo anaomba umuwekee hiyo hela ya umeme tu kwenye simu yake hapo ukijichanganya ukimuwekea imeisha hyo!!

Wengi wamelizwa!!Kuna boda katumwa juzi kamuwekea hela elfu 39...mwingine kaweka elfu 20 mwingine aliweka elfu 45 halafu ukikataa atakubali tu uende ukifika na delivery na mzigo wako atakuambia anakuja utakaa hapo utasubiri hapo ashakublock kitambo
 
Umeme wa dharura atanunuaje wa kuanzia elfu 20?

Nikituma mwingi sana labda wa elfu 3, mbali na hapo bado hajanishawishi..

Kwanza kitendo cha kusema eti amekosea namba ya mita nimtumie kwenye simu hapo hapo nitasitisha na delivery...
 
Boda kaaambiwa apeleke nyama kilo 3 na ndizi bukoba za elfu mbili na nyanya fungu moja
Akaambiwa aweke na elfu 20 kwenye simu.
From there jamaa hakupatikana kabaki na nyama zake sijui alipeleka wapi na elfu 20 ikaenda maskini.
Hii story ni kama nimeisikia pia.....
 
Boda kaaambiwa apeleke nyama kilo 3 na ndizi bukoba za elfu mbili na nyanya fungu moja
Akaambiwa aweke na elfu 20 kwenye simu.
From there jamaa hakupatikana kabaki na nyama zake sijui alipeleka wapi na elfu 20 ikaenda maskini.
Ndo maana boda wengine wanataka umtume sehemu ya lipa namba tu, mambo ya nitakupa hela ukileta hawataki.
 
Back
Top Bottom