Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 88,843
- 156,276
Hujaelewa. Hujui kusoma kwa ufahamu.Kama unaamini kuna ushirikina that goes against everything you believe in, an atheist does not believe in miracles or supernatural powers.
Wewe ni mnafiki.
Kwanza, kuamini kuna ushirikina maana yake nini? Nikisema najua kuna watu wanakwenda kwa wachawi kufanya ushirikina, ushirikina ambao mimi siuamini lakini wao wanauamini, hapo naamini kuna ushirikina?
Ni hivi, imani za ushirikina zipo. Mimi kusema kuna imani za ushirikina haimaanishi mimi naamini ushirikina.
Hivi, nikisema watu wanaenda kanisani kila Jumapili kumuabudu Mungu, wao wanaenda kanisani kumuabudu Mungu kika Jumapiki, hapo maana yake mimi naamini Mungu yupo?
Unajua kusoma kwa ufahamu wewe?
Mimi siamini kwenye miracles wala supernatural powers, ila kuna watu wanaamini miracles na supernatural powers, sasa mimi kusema kuna watu wanaamini katika miracles na supernatural powers kunanifanyaje mimi kuamini katika miracles na supernatural powers?
Zaidi, hujui hata atheism ni nini. Kuwa atheist ni kutoamini uwepo wa Mungu. Mtu asipoamini uwepo wa Mungu tu, tayari ni atheists.
Hizo habari za supernatural powers ni kitu tofauti. Hivyo, inawezekana kukawepo na atheist ambaye anaamini kwenye supernatural powers, ambazo hazitokani na Mungu, ila haamini kuwepo kwa Mungu.
Inaonekana unarukiarukia mambo tu bila kuyaelewa.