Kumuona nabii milioni 1.5 nimechoka

Kumuona nabii milioni 1.5 nimechoka

Kuna ndugu yangu anaumwa hoi bin taaban kawekewa mavitu huko kazini na yeye sio muumini wa waganga akaona aende Direct kuonana na baba yake wa kiroho kuhani amsaidie maeneo ya temboni kuelekea kwa msuguri , kaambiwa na wasaidizi wa Nabii atoe milioni 1.5 amuone nabii.

Baada ya kulipa hiyo hela chawa wa Kuhani wanamzungusha na kumpa kalenda kuwa angoje siku aliyopangiwa nabii yupo bize

Na risiti ya m 1.5 imetolewa nimechoka

Kiboko ya wachawi hakuwa peke yake.
Ameitwa?
 
😂😂🙌🤣🤣 Watu wanataka kudanlodi TU bila kufanya kazi

MWISHO WA SIKU HATA SHETANI ANAWACHEKA. ANAWAULIZA MLIKUWA MNAMFUKUZAJE MNASEMA shabarababara🤣🤣🤣🤣🤣👇👇👇
 
Bwana yesu ilikuwa bure
2 Timotheo 3:1-2,5-6
[1]Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.

[2]Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,

[5]wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.

[6]Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;


Kipofu tu ndie anaeweza kwenda uki
 
Wakristo tunapigwa vibaya vibaya😃, Mungu tunayemuamini Amekua na madalali? Kwa io ili Mungu akusaidie lazima utoe pesa?
Hakuna Mkristo anayepigwa. Kuwa ndani ya Yesu ni kuwa nuruni. Penye nuru Giza halikai. Tafakari Ukristo wako mkuu
 
Mwambie aende kwa prophet James Nyakia mwenge mpakani huyu ni nabii wa watu. Mwambie asikose nimeona watu wakifunguliwa
 
Hawa viongozi wa dini wa miongo yetu hii hawatofautian na zile kamali za barabarani unajikuta tu umeenda na hata wapo wanaoenda na hiyo mil 15 wakaiona ni sh. Kumi baadae sasa😭😭😭
 
Matapeli tu
20241114_162018.jpg
 
Du jambazi limekwapua 1.5 kiurahisi kabisa kama kunywa togwa
 
Nimekuja kubain dini yetu hii ndio Ina malofa wengi sana kuliko hata upande wa pili.
 
Kuna ndugu yangu anaumwa hoi bin taaban kawekewa mavitu huko kazini na yeye sio muumini wa waganga akaona aende Direct kuonana na baba yake wa kiroho kuhani amsaidie maeneo ya temboni kuelekea kwa msuguri , kaambiwa na wasaidizi wa kuhani atoe milioni 1.5 amuone kuhani.

Baada ya kulipa hiyo hela chawa wa Kuhani wanamzungusha na kumpa kalenda kuwa angoje siku aliyopangiwa nabii yupo bize

Na risiti ya m 1.5 imetolewa nimechoka

Kiboko ya wachawi hakuwa peke yake.
Usitulaumu manabii jilaumu wewe na shida zako. Kwanini umeshindwa kutatua shida zako mwenyewe.
 
Kuna ndugu yangu anaumwa hoi bin taaban kawekewa mavitu huko kazini na yeye sio muumini wa waganga akaona aende Direct kuonana na baba yake wa kiroho kuhani amsaidie maeneo ya temboni kuelekea kwa msuguri , kaambiwa na wasaidizi wa kuhani atoe milioni 1.5 amuone kuhani.

Baada ya kulipa hiyo hela chawa wa Kuhani wanamzungusha na kumpa kalenda kuwa angoje siku aliyopangiwa nabii yupo bize

Na risiti ya m 1.5 imetolewa nimechoka

Kiboko ya wachawi hakuwa peke yake.
inasikitisha sana.Sema vyovyote vile wekeza kwenye afya yako, kama unajiweza beba bima ya kueleweka na usiache kufuata ushauri wa madaktari.
 
Back
Top Bottom