Msichana anayemkataa mwanaume kwa vile ana kiwango chini yake cha elimu, anakuwa anajitambua. Huyo mwanamke ni wife material haswa! Uzoefu unaonesha kuwa miaka 5 ya kwanza kila kitu kitakuwa sawa ila mbele ya safari hasa baby na darling vikitoweka kinywani hapo inferiority complex ya mume ikikutana na superiority complex ya bibie huleta shida. Kawivu kanakuwepo hasa bibie akikutana na wasomi wenzie au kukumbushana ya mabibo hostel, hall 3 etc. Kwani jiulize, Kwanini ndoa za viongozi hazikawii kuvunjika hasa mama akiwa ni kiongozi. Halafu piga ua akinamama hupenda kutoa introduction kuwa huyu mume wangu ni mtendaji wa kijiji (wakati yeye mama akiwa mkulima) siyo awe afisa tarafa na aseme mume wangu ni dereva bajaji.