Habari zenu wakuu, natumaini Pasaka kwenu imekuwa vyema, kuna mdada mmoja tulikuwa tukiishi nae mtaa mmoja alikuwa mzuri shombe shombe nilitokea kumpenda sana lakini alikuwa ananiheshimu sana na binti mwenye maadili sana, nilitafuta kila mbinu ya kumuingia lakini nashindwa na sijawahi muona akizungumzia maswala ya mapenzi na sijawahi muona na mwanaume yeyote zaidi ya marafiki wa kike nao wote walikuwa ni mabinti wenye maadili sana ,kwahiyo niliangaika sana mpaka akasafiri lakini leo nimekutana nae ni mwaka wa tatu toka tupotezane Nimemuona ana mtoto mchanga katika kumuuliza maswali akadai amezalishwa na kuachwa huko alikokuwa roho imeniuma sana lakini Sina jinsi nilimpenda sana lakini udomo zege uliniponza sana ,vijana fungukeni msije mkaumia kama mimi .nawatakia sikukuu njema na Pasaka njema
anamaanisha AMESHINDWA KABISA KUSEMA KILE ANACHO MOYONI MWAKE...!Udomo zege ndo u nini poyee pasaka njema na kwako piyaa.
Wewe ni great thinker kweli.....katika kumuuliza maswali akadai amezalishwa na kuachwa huko alikokuwa.... Hapo alimaanisha ameshakufungulia mLaNgO! Ulichukua namba yake ya simu?
Huyu anaamini haraka haraka haina baraka!Mkuu ngoja ngoja yaumiza matumbo, imekula kwako sasa pole sana.
Hahahaha, saa hizi itakuwa kazi rahis kwake amfungukie tu ataeleweka.Huyu anaamini haraka haraka haina baraka!
Tena simple kabisa mkuu, karahisishiwa kazi kama kweli anampenda bado basi kazi Ni rahisi tu kwakeKwa gear ya kuwa nae na kumlelea mtoto wake pindi ukimfungukia kwa sasa Utampata.
Wengi wana allergy na single mothers.....katika kumuuliza maswali akadai amezalishwa na kuachwa huko alikokuwa.... Hapo alimaanisha ameshakufungulia mLaNgO! Ulichukua namba yake ya simu?
daah... Mkuu hiyo avata Mkuu...!Mfungukie..mlee mtoto
kwani ye anamtaka mtoto au mamaake, afu huyu anaonekana ataka piga na asepe tuMfungukie..mlee mtoto