wakati niko kidato cha tatu mwalimu wangu wa somo la hisabati aliondokea kunipenda sana sababu nlifanya vyema katika somo lile..akawa wakati mwingi ananiita pale ofisini na kunipa kazi kidogo kidogo kama vile kusahihisha homework za wanafunzi wa vidato vya chini huku tukipiga stori za kawaida..kama kawaida,wanaume wengi tunapopata mapendeleo kutoka kwa mwanamke cha kwanza kuja akilini ni kuwa lazima huyu mwanamke anakuelewa ila hataki kukueleza moja kwa moja..ikawa ndo mawazo yangu kwa muda...ipo siku nikaamua kumtongoza ila hapo ndo nikaharibu..yaani iweje mtoto rika na wanangu kufikia kiwango hata ukanitongoza..je huoni mimi mamako wewe mvulana?..yani nilijaribu kuomba msamaha ila wapi..nikatumwa kwa mkuu wa shule nikasususia..akaenda mwenyewe kushtaki..yaani nlitimuliwa bila hata ya kupewa barua..ikawa nikionekana tena huko itakuwa balaa...nlijutia sana kuzoeana kwangu na huyu mwalimu...ila alikuwa mrembo kupindukia...kama angenikubali hakika singesita kuchukua fursa...utundu wangu uliniponza..