Kumtoa mtoto!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumtoa mtoto!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mvaa Tai, Oct 29, 2012.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,175
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Wana Jamvi weekend hii nimepata kadi ya mchango ambayo sijawahi kuchangia mchango wa aina hiyo, kadi yenyewe ina heading isemayo "Mchango wa Maulidi" inaendelea kusema Bwana na Bi xxx wanaratajia kumtoa mtoto wao kipenzi mwanzoni mwa mwezi December, hivyo mimi kama rafiki, Ndugu au jamaa wa karibu wananiomba mchango wa hali na mali ili kufanikisha jambo hilo muhimu.

  Kwasababu ni watu wa imani tofauti na mimi na nilifahamiana nao nikiwa nanunua Shamba huko bagamoyo, nimehisi pengine kumtoa mtoto si kitu kigeni ila ni mimi tu sifahamu na nikiwauliza wao wanaweza kuhisi nina dharau ilihali wao wameniheshimu kwa kunishirikisha jambo(Hivyo nimekubali kushiriki bila kujua 'kumtoa mtoto' ni nini). Sijajua wanamaanisha nini je wanataka kumfanyia mtoto Sendoff au Harusi? Naombeni anayefahamu mchango wa maulidi ni nini, na kumtoa mtoto ni nini anisaidie kabla sijachangia ili nifahamu uzito wa jambo lenyewe maana naamini humu wanapitia watu wa aina mbalimbali na exposure tofauti tofauti.
   
 2. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hakuna kitu kinanibo na kurudisha nyuma maendeleo na mambo muhimu kama michango!!! Nisamehewe ila sipendi na huwa sichangi, nachanga kwa vitu important na watu important, tena kile nilichonacho sio kile watakacho. Nways cjui maana, ngoja wenyeji waje!
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mkuu ulivyotaja tu bagamoyo kilichonijia akilini ni mambo mawili kuhusu hiyo kadi ya mchango uliyopewa;

  1. Kumtoa mtoto yaweza kuwa kwamba aliyekupa kadi mke wake au mwanamke alijifungua mtoto siku kadhaa zilizopita hivyo huyo mtoto baada ya kuzaliwa then anahitajika kufanyiwa kasherehe ambapo sasa atakuwa anaweza kuchanganyika na other members of the community. Sijui ni watu wa itikadi gani lakini kama ni waislam hiyo kitu huitwa siku 40 baada ya mtoto kuzaliwa ambapo huendana na kisomo ( maulidi) watu hula na kunywa na kufurahi na ndipo hata huyo mtoto hunyolewa zile nywele wanazoita za utotoni yaani alizozaliwa nazo.

  2. Huenda huyo aliyekupa kadi ana binti yake aliyevunja ungo na kwa mila zao huwekwa ndani kwa muda fulani akifundishwa mambo yanayoendana na majukumu ya mwanamke then baada ya huo muda hufanyika sherehe ya kumtoa huyo binti. Hii mara nyingi huendana na sherehe ya ngoma zaidi sijawahi kuona maulid ikifanyika zaidi ya watu kula, kunywa na kucheza.....Nina uhakika moja kati ya haya mawili linahisika hapo!
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,175
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Thanks mkuu ngoja nisubiria wengine kama wana maana zaidi ya hii, lakini mpaka hapa sijaona kama natakiwa kuchangia hasa katika kipindi hiki kigumu
   
 5. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,175
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Tatizo dada yangu ni definition ya vitu important ni vipi hivyo? ndiyo maana hata hili swala wamenisisitiza kwamba nitoe mchango ili kufanikisha "swala hili muhimu"
   
 6. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kutoa ni moyo na si utajiri. Kumbuka huyo ni jirani yako, leo kwake, kesho kwako!
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Mkuu haya mambo ukiyaangalia kwa undani utagundua ni kamtindo kamezoeleka ndani ya jamii kuchangiana kwa yale mambo ambayo yanahusisha jamii husika. lakini kiukweli hayana tija hata kidogo. Niliwahi wakati fulani kusababisha manung'uniko na mtafaruku kwenye familia yetu. Tulikuwa na mtoto wa sister wetu amepata admission CBE kusoma Advanced Diploma (Self sponsorship) at the same time tulikuwa na mtoto wa baba yetu mkubwa anataka kuoa. Utakuta yote yalikuwa yanatutegemea cc kuchangia mambo yote. Nikatoa wazo baada ya kuona hali kwa mambo yote mawili hayaendi. Kwa nini tusielekeze nguvu kumchangia huyu mwanafunzi aende chuo then huyu anayetaka kuoa achukue tu mke wake kwa a very simple sherehe...Weeeeeeh!!!!! Yalitoka maneno hapo acha tu sitaki kukumbuka hiyo siku...Kwa hiyo ili ku-maintain mahusiano na ujirani mwema we changia tu ulichonacho....
   
 8. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,775
  Likes Received: 8,039
  Trophy Points: 280
  Mambo ya makabwela wa Buguruni hayo. Huko masaka na chuo kikuu nakoishi mtaalam hakuna mambo ya kumtoa mtoto wala kumuingiza.

  Baada ya hilo, kaa tayari kwani muda si mrefu utaambiwa mchango mwingine wa mtoto kuingizwa suna.

  Hapo kigodoro lazima kiwepo
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,175
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Inauma sana kufanya kitu kinafiki any way nitafanya hivyo kinafiki lakini huwa sifurahishwi na vimichango vya aina hii
   
 10. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,175
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Tatizo siyo kutoa ishu unatoa kwasababu gani? unajua watu wamezoea kuchangisha imefikia mahala watu wana changisha hata Birthdays au graduations
   
 11. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  I bet mumber 1 suits to your question...by the way kuna haja sana ya kujitathmini na hizi mila zinazokomba kila

  senti tunayosevu...manake michango mingi ya sisi makabwela ni ya starehe za muda mfupi zisizo na tija..lolest!
   
Loading...