Kumsomesha mke wako chuo

Kumsomesha mke wako chuo

Za kuambiwa changanya na zako...

Habari wadau, Naomba niwashirikishe katika hili.

Nina mke wangu ambaye kwa sasa tuna kama miaka takribani sita,wakati tunaingia mahusiano alikuwa yupo form six,alipomaliza tu A-level nikampa mimba bahati nzuri alipata nafasi akachaguliwa kwenda St John Dodoma na mkopo juu asilimia kama themanini hivi,kutokana na hali halisi aliyokuwa ya ujauzito kwake likawa tatizo tukaamua kuahirisha tena bila wazazi wake kujua.

Baada ya miaka miwili na miezi nane akiwa amejifungua na mtoto angalau mkubwa mimi nikaamua aende chuo atimize ndoto zake.Mpaka sasa anasoma chuo na ameingia mwaka wa pili.

Tatizo nililonalo ni kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakinibeza kuwa napoteza muda vyuoni kuna mambo mengi watakuchukulia na mwanamke atakuja kunigeuka nikabaki nisijue la kufanya.

Mwaka 2017 ndio anamaliza chuo.

Je, wewe mdau mstaarabu hembu nisaidie kwa hekima zako!

Kama atakua mvivu wa kupiga msuli ktk masomo hakuna jinsi lazima atafute maksi za chupi.ila kama mzuri kimasomo usiwe na wasiwasi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom