Kumsomesha mke wako chuo

Kumsomesha mke wako chuo

nandembako

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
655
Reaction score
528
Habari wadau, Naomba niwashirikishe katika hili.

Nina mke wangu ambaye kwa sasa tuna kama miaka takribani sita,wakati tunaingia mahusiano alikuwa yupo form six,alipomaliza tu A-level nikampa mimba bahati nzuri alipata nafasi akachaguliwa kwenda St John Dodoma na mkopo juu asilimia kama themanini hivi,kutokana na hali halisi aliyokuwa ya ujauzito kwake likawa tatizo tukaamua kuahirisha tena bila wazazi wake kujua.

Baada ya miaka miwili na miezi nane akiwa amejifungua na mtoto angalau mkubwa mimi nikaamua aende chuo atimize ndoto zake.Mpaka sasa anasoma chuo na ameingia mwaka wa pili.

Tatizo nililonalo ni kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakinibeza kuwa napoteza muda vyuoni kuna mambo mengi watakuchukulia na mwanamke atakuja kunigeuka nikabaki nisijue la kufanya.

Mwaka 2017 ndio anamaliza chuo.

Je, wewe mdau mstaarabu hembu nisaidie kwa hekima zako!
 
Hayo mawazo wa waoga tu!! Somesha mkeo kwa maendeleo ya familia yenu, kwani huyo ni "demu" wako?!
 
Kama unaisshi nae msomeshe tu. Isitoshe umeshamchukuliaa mda wa kutosha.
 
Hayo ni mawazo ya mwanaume asiyejiamini usiwape watu wakujaze na fikra za kijinga...msupport mkeo katika hilo suala la elimu na isitoshe wewe ndio sababu ya yeye hadi leo hii hajahitimu masomo ulimkatisha masomo
 
Kinachowaponza ni kusikiliza maneno ya watu.... hususan kusikiliza kutoka kwa walioshindwa.

Hebu ishi maisha yako kama wewe fanya malengo yako. Yanayotokea kwa mwingine haimaanishi kwako yatatokea.

Afterall kuna hasara gani kumsomesha mama wa mtoto wako? Mbona yeye kahatarisha maisha kwa kukuzalia wewe kutoa vijisenti tu unaona issue??
 
Kama n mkeo, uko sahihi kumsomesha especially kwa ajili ya future ya wanao!
 
Jidanganye,hao kenge huwa hawasomeshwi,unaharibu mizania,mizani ilikuwa imebalansi were unaongeza uzito upande wake,hao viumbe waliongea na shetani wa kwanza kabisa kati ya viumbe wote mungu alioumba,utakuja kulia,mwanamke mwanamke tu,awe binti,mkeo,kakuzalia,mzee. Tupa kule
 
Hahahahaaaa hawa viumbe ndo wa kwanza kuongea na shatani teh teh teeeeh umekulavitu vyako nn mkuu?
 
Huko chuo itabd uwe unaenda mara kwa mara ili asikupoteze akilini maana huko atakutana na vijana wa rika lake na lolote linaweza kutokea, unaweza kugongewa tu kwa muda akiwa anasoma ama ndo akafol hapo ndo itakuwa shida. Ila uwe na hisia chanya zaidi ya hzo hasi.. mpeleke ila mtembelee mara kwa mara.
 
Broo wory out, we somesha and if possible nipe namba yake niwenampa ushaur. Coz mi nipo hapa st john Dodoma mambo yataenda vizur
 
Habari wadau,naomab niwashirikishe katika hili....nina mke wangu ambae kwa sasa tuna kama miaka takribani sita,wakati tunaingia mahusiano alikuwa yupo form six,alipomaliza tu A-level nikampa mimba bahati nzuri alipata nafasi akachaguliwa kwenda st John dodoma na mkopo juu asilimia kama themanini hivi,kutokana na hali halisi aliyokuwa ya ujauzito kwake likawa tatizo...tukaamua kuahirisha tena bila wazazi wake kujua,baada ya miaka miwili na miez nane akiwa amejifungua na mtoto angalau mkubwa mimi nikaamua aende chuo atimize ndoto zake...mpaka sasa anasoma chuo na ameingia mwaka wa pili,tatizo nililonalo ni kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakinibeza kuwa napoteza muda vyuoni kuna mambo mengi watakuchukulia na mwanamke atakuja kunigeuka nikabaki nisijue la kufanya....mwaka 2017 ndio anamaliza chuo,JE WEWE MDAU MSTAARABU HEBU NICHANGIE HEKIMA ZAKO!

Ni mke baada ya taratibu zote kufatwa ikiwa ni kutoa maali kupata kibali cha wazazi na kama sio mean ni mchumba so kusomesha mke sawa ila mchumba!!!!!! Ongeza za kwako jk
 
hata kama ni ka dem kako kumbuka ni ww uliesababisha akakatiza masomo, kwa hiyo ankudai kwa kile alichofanya kwa ajili ya kulinda penzi lenu. Ukitendewa wema lipa wema mkuu ndio ubunaadam "wewe kakupa mtoto yeye mpatie kadigirii kake then ya mbele mwachie Mung.
 
Asante sana wadau....imenifurahisha sana,point za wanaosupport ni nyingi kuliko wanaonibeza.....nia ya kuuliza ni kwamba mimi kama binadamu napata wasi wasi,najiuliza mbona naona nachokifanya ni sahihi kwa maendeleo ya familia,hata kama atafanya ujinga lakini hataweza kumchukia mwanae ambae ni damu yake....asanten wadau
 
Ni wazo zuri tu kiongozi, ila wamama nao wanachoshaaaaaaa! Msomeshe tu ila usitegemee kwamba lazima upate +ve social return on investment!
 
Habari wadau,naomab niwashirikishe katika hili....nina mke wangu ambae kwa sasa tuna kama miaka takribani sita,wakati tunaingia mahusiano alikuwa yupo form six,alipomaliza tu A-level nikampa mimba bahati nzuri alipata nafasi akachaguliwa kwenda st John dodoma na mkopo juu asilimia kama themanini hivi,kutokana na hali halisi aliyokuwa ya ujauzito kwake likawa tatizo...tukaamua kuahirisha tena bila wazazi wake kujua,baada ya miaka miwili na miez nane akiwa amejifungua na mtoto angalau mkubwa mimi nikaamua aende chuo atimize ndoto zake...mpaka sasa anasoma chuo na ameingia mwaka wa pili,tatizo nililonalo ni kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakinibeza kuwa napoteza muda vyuoni kuna mambo mengi watakuchukulia na mwanamke atakuja kunigeuka nikabaki nisijue la kufanya....mwaka 2017 ndio anamaliza chuo,JE WEWE MDAU MSTAARABU HEBU NICHANGIE HEKIMA ZAKO!

Hata akikugeuka elimu yake ataitumia kumlea mwanao.
 
Mimi mke wangu nilimsomesha toka A-level hadi chuo baada ya kumpatia ujauzito akiwa kidato cha3. Sasa tunaishi wote. Acha woga, usiwasikilize watu.
 
Huko chuo itabd uwe unaenda mara kwa mara ili asikupoteze akilini maana huko atakutana na vijana wa rika lake na lolote linaweza kutokea, unaweza kugongewa tu kwa muda akiwa anasoma ama ndo akafol hapo ndo itakuwa shida. Ila uwe na hisia chanya zaidi ya hzo hasi.. mpeleke ila mtembelee mara kwa mara.

Kugongwa atagongwa tu hata mtaani. Vijana acheni mawazo hasi. Kuna jamaa namfahamu kamsomesha mkewe masters UK kwa hela yake mfukoni gharama zote, tuition fee peke yake GBP 16000, Na jamaa anasema hata akigeuka elimu hio itasaidia wanae,karudi sasa hivi wanaendelea na maisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom