Bukwabi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2013
- 3,352
- 1,155
"Mke wangu ametoroka na hajulikani alipo. Chanzo ni kwenda naye bar wanapopika chakula vizuri sana ili ajifunze kupika kwani akipika chakula sifurahii kabisa.
Kwani kinazidiwa na cha house maid "Hayo ni maneno ya rafiki yangu ambaye yuko kwenye sintofahamu na mke wake baada ya kumsifia mhudumu wa bar.
Baada ya kumaliza kula chakula kwenye bar moja ambayo inasifika kwa kupika chakula kizuri. Jamaa yangu huyo alimtoa 'out' mke ili akaone wanawake wenzake wanavyopika na ajifunze ili awe anmpikia vizuri.
Kitendo cha kumsifia mhudumu wa bar kilimuudhi sana mke wa jamaa kwani rafiki yangu huyo hajawahi kusema "asante kwa chakula" kilichopikwa na mke wake!.
Mke akaamua kuondoka na mpaka sasa hajulikani alipo. Rafiki yangu huyo anampenda sana mke wake ikizingatiwa kuwa ni kati ya wanawake waliojaaliwa kila idara kwenye uumbaji.
Je kwenda bar na mke ni balaa? Mke akiwa wa aina hii wewe unafanya nini?
Kwako mdau toa ushauri wako