Kumshitaki Mbunge Lusinde kwa matusi aliyomwaga Arumeru

iwapo akina mama watakaa kimyakwa kudhLilishwa kiasi kile kuhusu mimba then sintowaelewa tena

ntaomba comments zagaijin, wos, rr
 
Slaa, Lema, Mbowe, kumfungulia Lusinde Kesi ya Madai kwa udhalilishaji?

Tarehe 26.03.2012 katika eneo la Ngaresero, Usa River, Arusha, Lusinde, Mbunge wa Mtera, alitoa hotuba iliyolenga kuwadhalilisha baadhi ya viongozi wa chadema kwa hulka zao binafsi, inayolenga kuwachafua na kuwadhalilisha utu wao binafsi, na kauli ambazo kwa tafsiri ya wazi hazikuwa na tija kisiasa

Mh Lusinde alinukuliwa akisema

Lema (mbunge wa Arusha) .." alipata bwana magereza, "aliliwa", bwe*e, tunajua alifanywa nini"

Dk Slaa "alishindwa upadre na alifukuzwa kwa kutia mimba wanakwaya", "anatembea kama anajinyea", "ana mimba yetu" " anatishia kujamba wakati anaharisha" "kama dk slaa anataka fujo basi ianzie kwa mke wake" , "yule ngumi moja tu naua"

Mbowe – "ana uchungu wa mimba" "tumeshampiga mimba"
nassari – "(w)amepigwa mimba"

Kutokana na kauli hizi Lusinde yuko kwenye hatari ya kufunguliwa kesi ya madai na kufilisiwa kabisa.

Mtazamo ~ kauli hizi zinalenga kudhalilisha utu wa mtu binafsi na hazina mshiko wowote katika kukosoa sera za upande wa pili. Inawezekana kukosoa sera za wapinzani wako bila kuchafua utu, familia yake, au heshima yake mbele ya jamii. Kwa kweli hata kama kuna uhuru wa maoni, hii imepita kiasi. Kweli unajaribu kum -convince mpiga kura akupigie kura kwa kwa hoja ya "kupiga wanasiasa wenzako mimba" ? Sidhani kama hizi ndio sera za CCM. Lakini pia Lusinde alitoa kauli kuwa yeye "ni kichaa wa kuzaliwa" kwa hiyo inawezekana kweli hana akili timamu na CCM imeamua kumtoa kafara kichaa wao kwenda kulipuka na kutoa kauli ambazo yeye mwenyewe hajui madhara yake. Lakini pia ukifuatilia michango ya Lusinde Bungeti utagundua kuwa ukweli uwezo wake wa akili unatia shaka.

Baada ya uchaguzi kuna umuhimu wa huyu mtu kuchukuliwa hatua za kisheria angalau tujue uhuru wa speech unaazia na kuishia wapi, ili na sis wengine tukitaka kuropoka humu JF tujue madhara yake....

Video link //bofya hapa kusikiliza hotuba yake... Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru - YouTube
 
Dr Slaa, Lema, Mbowe wote wako kwenye kundi la waheshimiwa, wanajitambua kuwa wanalo jukumu la kulinda uheshimiwa wao mbele ya wazee, vijana na watoto. Wana majukumu mazito na watu wanaona nini wanafanya.

Huyu kibaka Lucinde watuachie sisi wananchi tuhangaike naye. Waheshimiwa waendelee na kazi ya kusuka upya nchi hii inayoelekea kuzimu.
 
Nimemsikiliza Halima Mdee, ni kweli unaweza kusema kuwa kama ni mpira basi alikuwa akichezea kwenye chaki.

Kasema Katoboa sikio ila hajasema ni Shoga (hapa ukiwa mahakamani, inaweza kula kwako).

Kasema Wasira ni mbaya sana na sura kama Sokwe (hapa napo waweza kupata sana shida maana neno NI KAMA linaweza kumpa mtu ushindi na kukuacha wewe ukiwa huna cha kujitetea).

Ila maneno ya Lusinde kuwa:

1. Lema kapata bwana na ameliwa - Hakuna mtu alisema fulani wa CCM kaliwa.

2. Vinsent Nyerere ameliwa - Kama hapo juu.

3. Prof. Majimarefu kawachanja chale matakoni wana CDM (Itabidi Prof. athibitishe hili.)

4. Slaa alifukuzwa Upadre kwa kuwapa Mimba waimba kwaya (Nalo itabidi alifukuze).

5. Dr. Slaa anatembea kama kajinyea (hili ni kama la Halima Mdee, itakuwa ngumu kuthibitisha maana ni KAMA).

6. Wamewamba Mimba Chadema (hili itabidi athibitishe hasa wenye wake zao Chadema.)

Na mengine mengi ambayo unaona kuwa hakukuwa na haja ya kuyasema.

Kesi ya Mkapa na Vincent Nyerere lilikuwa ni OMBI/Swali kwa Mkapa (Jibu) kuwa atueleze Watanzania kifo cha Nyerere. Hakuna sehemu VN alisema Mkapa alimuuwa Nyerere. Unaweza ukabishana sana juu ya hili lakini ukweli unabaki kama kwa Halima Mdee kuwa Wanachezea kwenye mstari. Itakuwa ngumu kusema mpira ulitoka. Ila CCM wanajilipua wazima wazima na haswa huyu Lusinde kwenye hii video.

Anyway, nafurahi kuwa anajiita yeye ni KICHAA WA KUZALIWA.
 
Hivi Tendwa yuko wapi? mbona kimya? au hayo siyo matusi.

Kama sio matusi mimi ninaomba yageuziwa kwa RAIS JK Kikwete tuone kama kama Tendwa atakaa kimya! Kwenye Majina ya Lema, Dr. Slaa, Mbowe na Nassari tu-substitute tuweke jina la KIKWETE tuone kama itakubarika!
 
kumshitaki lusinde ni kumpa promo isiyokua ya lazima..huyu ni kuachana nae tu hajui alitendalo.!
 
Mpaka Leo hajaitwa na waliompeleka Arumeru akapate councelling? Mbona ametukana matusi ya nguoni? Nani atakaechagua chama cha watu wanaotoa matusi namba hiyo? Watoto, mke wake, familia ya Lusinde, Watanzania wote mtu huyu anatufaa? Ameaibisha familia na chama chake.
 
hilo ni lazima walifanye maana ukisikiliza hayo mashambulizi utapata taabu kama alijua mahali pale kuna watu wa aina mbalimbali, ambao nao pia walihitaji kusikia lugha ya staha kutokana kwamba wengine walikuwa na familia zao. lakini hata ccm tunahitaji tusikie nini watasema juu ya lusinde, wakikaa kimya basi kuna haja ya kujiuliza zaidi juu yao.
 
Ni kauli za kisiasa tu jamani, jadilini yalio na faida katika taifa lenu.

Kiongozi, Sina shaka hata kidogo Lucinde asingekuwa bungeni angekuwa kibaka. Na kuna tofauti kubwa sana kati ya kauli za wana siasa na kauli za vibaka. Kauli alizotoa Arumeru, zinamfunua kabisa ukondoo wake, na kama Mtera waliamini wamemchagua mheshimiwa sasa wakae wakijua wapata kibaka. Hawana mbunge.
 
JacksonMichael said:
Ni kauli za kisiasa tu jamani, jadilini yalio na faida katika taifa lenu
Kama ndo kauli zenu za kisiasa, no wonder ndo maana nchi ipo hapa!!!!

Mkuu unashangaa nini wakati kila kukicha wapinzani wanaropoka mambo ya ajabu! sijaona cha kuwafanya mbowe a wenzake wapanic kwa kuwa ndio siasa za TZ kuattack personal kuliko sera.
 
magamba wameishiwa sera wanakuja ma matusi sijui matusi yakiisha watakuja na nini tena
 
Kujibizana na mtu kama Lusinde ni kupoteza muda tu. Kama wanataka kumchukulia hatua ni niis bora zaidi kwa sababu huyu jamaa nadhani ana matatizo makubwa kwenye akili yake
 
Haya matusi apelekewe Tendwa aulizwe ana maoni gani juu ya haya matusi?
Na je wangetukana CUF, CHADEMA, TLP n.k dhidi ya CCM angechukua uamuzi gani?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
hilo ni lazima walifanye maana ukisikiliza hayo mashambulizi utapata taabu kama alijua mahali pale kuna watu wa aina mbalimbali, ambao nao pia walihitaji kusikia lugha ya staha kutokana kwamba wengine walikuwa na familia zao. lakini hata ccm tunahitaji tusikie nini watasema juu ya lusinde, wakikaa kimya basi kuna haja ya kujiuliza zaidi juu yao.

Jambo ambalo bado sijaelewa na ccm hawaonekani kutoa majibu ni kwa nini Lucinde aliona ni sahihi kuingiza wazazi ambao kwake ni kama babu kwenye siasa huko Arumeru? Anapata wapi ujasiri wa kumuongelea baba mzazi wa Mwl Nyerere Mzee Burito? Au baba mzazi wa Dr Slaa Mzee Peter? Kulikuwa na sababu zipi za kuwaingiza hawa babu kwenye siasa za Meru?
 
Angalia salary slip yako, anganilia PAYE asilimia kubwa inatumika kuwalipa watu kama LUSINDE. Ni aibu kwa jimbo kuongozwa na mhuni kama huyu.
 
Slaa, Lema, Mbowe, kumfungulia Lusinde Kesi ya Madai kwa udhalilishaji?

Tarehe 26.03.2012 katika eneo la Ngaresero, Usa River, Arusha, Lusinde, Mbunge wa Mtera, alitoa hotuba iliyolenga kuwadhalilisha baadhi ya viongozi wa chadema kwa hulka zao binafsi, inayolenga kuwachafua na kuwadhalilisha utu wao binafsi, na kauli ambazo kwa tafsiri ya wazi hazikuwa na tija kisiasa

Mh Lusinde alinukuliwa akisema

Lema (mbunge wa Arusha) .." alipata bwana magereza, "aliliwa", bwe*e, tunajua alifanywa nini"

Dk Slaa "alishindwa upadre na alifukuzwa kwa kutia mimba wanakwaya", "anatembea kama anajinyea", "ana mimba yetu" " anatishia kujamba wakati anaharisha" "kama dk slaa anataka fujo basi ianzie kwa mke wake" , "yule ngumi moja tu naua"

Mbowe – "ana uchungu wa mimba" "tumeshampiga mimba"
nassari – "(w)amepigwa mimba"

Kutokana na kauli hizi Lusinde yuko kwenye hatari ya kufunguliwa kesi ya madai na kufilisiwa kabisa.

Mtazamo ~ kauli hizi zinalenga kudhalilisha utu wa mtu binafsi na hazina mshiko wowote katika kukosoa sera za upande wa pili. Inawezekana kukosoa sera za wapinzani wako bila kuchafua utu, familia yake, au heshima yake mbele ya jamii. Kwa kweli hata kama kuna uhuru wa maoni, hii imepita kiasi. Kweli unajaribu kum -convince mpiga kura akupigie kura kwa kwa hoja ya "kupiga wanasiasa wenzako mimba" ? Sidhani kama hizi ndio sera za CCM. Lakini pia Lusinde alitoa kauli kuwa yeye "ni kichaa wa kuzaliwa" kwa hiyo inawezekana kweli hana akili timamu na CCM imeamua kumtoa kafara kichaa wao kwenda kulipuka na kutoa kauli ambazo yeye mwenyewe hajui madhara yake. Lakini pia ukifuatilia michango ya Lusinde Bungeti utagundua kuwa ukweli uwezo wake wa akili unatia shaka.

Baada ya uchaguzi kuna umuhimu wa huyu mtu kuchukuliwa hatua za kisheria angalau tujue uhuru wa speech unaazia na kuishia wapi, ili na sis wengine tukitaka kuropoka humu JF tujue madhara yake....

Video link //bofya hapa kusikiliza hotuba yake... Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru - YouTube

Binafsi naona apuuziwe tuu, kwasababu mtu mzima kama yule kutoa matusi ya namna ile kila mtu kamzalau
 
Back
Top Bottom