Kumsamehe mtu ni lazima muwe marafiki tena?

Duh, yani mke kasababisha uende jela halafu uponee chupuchupu utoke umfate akusamehe kwa kulia???Hapo kuna kitu zaidi ya jela unakitafuta. Kama nimempiga kwa upuuzi aliosababisha yeye ni haki yake na scale ya kipigo inaendana na kosa hata ikizidi, sikulewa, sijamuonea ametibua nimemrekebisha weee hasikii, nikamzibua akaumia, akiyapeleka haya mambo kwa mjumbe tu hapo ni kwa heri ya ndoa mara 100 anishaki kwa wazazi wake au wangu. sembuse kwa mwenyekiti-polisi-mahakamani-jela...halafu nirudi nikamuombe msamaha hata kama angekuwa na utajiri wa Dangote HAITOKEI.
😳😳😳😳 makubwa haya
 
Wakuu habari za muda huu,

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada ambayo naomba niiwasilishe kwa mtindo wa swali kwani natamani sana kujua majibu ya hili.

Je, nikimsamehe mtu ni lazima tuwe marafiki tena?

Mfano kwa kupitia kisa hiki;

Mume amegombana na mkewe na ikafika hatua ya mume kumjeruhi mke wake kwa kutumia kisu na shoka na kesi ikaenda kwenye yombo vya Sheria hadi kufikia mume kufungwa jela.

Mume akaja kupata msamaha wa Rais na akarudi nyumbani ambapo alikuwa akiishi mwanzo na mkewe ila mke akaomba muda wa kujifikiria na kwenda kuishi kwa mmoja wa watoto wao ambapo kwa kusikiliza panaonekana ni eneo hilo hilo kwani wanaweza kuonana muda wote na kuweza kula pamoja

Kufanya hadidhi ndefu kuwa fupi ni kwamba mume aliona maisha ya pale nyumbani magumu tofauti na matarajio yake na mke ndio anaonekana kushindwa kabisa hivyo sasa hivi mke kaondoka kirudi kwao na mume anasema haelewi kwa nini mke kaondoka.

Mind you: Mume alipotoka jela kwa msamaha kabla ya kutia mguu pale nyumbani kulifanyika Tambiko (mambo ya kiasili) na pia inaonekana na mambo ya kikanisa yaliganyika pia (sielewi uhusiano hapa) ila yote haya ni kuandaa wahusika kuishi pamoja.

Sasa mimi nina maswali hapa:

> Mke amemsamehe mume wake au bado?

>Je, kumsamehe mtu ni lazima mrudishe mahusiano yenu au kila mtu anaweza kuishi maisha mengine huku umemsamehe aliyekukosea?

> Mume huyu anajua kuwa alikosea?

> Huyu mume anaonaonesha kujutui alichofanya?

>Je, unadhani hawa wote wanaweza kutoka hapa walipo na kuishi maisha ya furaha na amani wakiwa pamoja au kutokuwa pamoja?

> Ushauri wako ni upo kwao?

Tazama video ya kisa hiki

View attachment 1427393

Mimi bado nipo kwenye kuwaza mahusiano kati ya matambiko/Maombi na huyo mume kubadilika tabia. But anyways
Hata wangechinja wanyama wote duniani, tabia ya mtu ni kama ngozi tu, Hapo naona familia wanaona wamesha solve kila kitu wanataka maisha yarudi kama zamani, Mambo hayawezi kuwa same, Na aliyewaambia kuwa bado kuna mapenzi hapo nani? Hakuna mapenzi hapo unalalaje/kuishi na kushirikiana na mtu ambae alimanusura akutoe roho??

Mi nadhani Mke wala hajamsamehe mume wake na wala si lazima, wamuache mama wa watu roho yake iwe sawa tena, kila mtu aishi maisha yake kwa ss na si lazime iwe nyumba moja

Kumsamehe mtu haimaanishi mrudi kama zamani, huyo mme pia sidhani kama anajua alichofanya ni almost to mauaji, anafikiri some matambiko/Maombi will fix moyo wa mke wake alafu warudi kama zamani, woii Mpaka sasa nampongeza mwanamke kwa kuchukua uamuzi aliochukua, siku akipata chance ya kumkamata mke wake tena atamuua tu kabisa( Mwanaume si mzima yule anahitaji msaada zaidi)

The fact kuwa baba bado haelewi anajiuliza kwann mama kaondoka, hilo ndo tatizo kubwa linalonichanganya mpaka mda huu
 
Upo sahihi kabisaa mkuu, yaani huyu mume hapo anashangaa kwanini mke kaondoka, yaani anataka watu wamuelewe yeye au mke amuelewe yeye na sio yeye kuwaelewa wenzake.

Yaani kisha kafanya tambiko na kuombewa sijui (huu mchanganyiko haueleweki) anaona ni tiketi ya kila kitu kuwa sawa. Huyu baba wala hajielewi. Hata ningekuwa mimi isingekuwa rahisi kuendelea na maisha kama zamani. Ampe muda huyo mama wa watu na asipoweza kurudi kwake pia amuelewe. Huyu mume ni mbinafsi sana.
 
Somo la msamaha ni gumu sana ndio maana kwa wakristo kipindi cha Yesu wafuasi wake walikuwa wanamuuliza sana kuhusu msamaha na hata majibu aliyokuwa anayatoa bado yalionekana na utata mfano mtu akikukosea ukamsamehe na baadae akarudia unaweza kusamehe hata 7 mara 70.

Kwa kesi ya huyo mzee nadhani kila mtu aendelee na Maisha yake tu huwezi kuishi na mtu ambae alitaka kukutoa uhai ukawa comfortable. Unaweza ukasamehe ila si kuishi nae tena ni ngumu mno huwezi kupata Amani ya moyo
 
Mkuu watu wanasamehe na kuishi pamoja vizuri tu mkoani Mara mwanamke anapigwa hadi anakaribia kufa bado anaendelea kuishi na mumewe mpaka wanakufa.

Kama wana watoto wakubwa mpaka wanajitegemea kabisa afu mwanamke anarudi kwao kwa baba na mama yake hapo ni kiashiria tosha huyo mwanamke bado hayupo sawa na ni pasua kichwa.
 
Asamehe na ajitahidi asahau(ingawa hapo Kuna ugumu) .. inawezekana kuwa marafiki kwa ajili ya watoto.
 
Ni rahisi kusema "nimekusamehe" ila kutoa msamaha ni ngumu sana.
 
Wakuu habari za muda huu,

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada ambayo naomba niiwasilishe kwa mtindo wa swali kwani natamani sana kujua majibu ya hili.

Je, nikimsamehe mtu ni lazima tuwe marafiki tena?

Mfano kwa kupitia kisa hiki;

Mume amegombana na mkewe na ikafika hatua ya mume kumjeruhi mke wake kwa kutumia kisu na shoka na kesi ikaenda kwenye yombo vya Sheria hadi kufikia mume kufungwa jela.

Mume akaja kupata msamaha wa Rais na akarudi nyumbani ambapo alikuwa akiishi mwanzo na mkewe ila mke akaomba muda wa kujifikiria na kwenda kuishi kwa mmoja wa watoto wao ambapo kwa kusikiliza panaonekana ni eneo hilo hilo kwani wanaweza kuonana muda wote na kuweza kula pamoja

Kufanya hadidhi ndefu kuwa fupi ni kwamba mume aliona maisha ya pale nyumbani magumu tofauti na matarajio yake na mke ndio anaonekana kushindwa kabisa hivyo sasa hivi mke kaondoka kirudi kwao na mume anasema haelewi kwa nini mke kaondoka.

Mind you: Mume alipotoka jela kwa msamaha kabla ya kutia mguu pale nyumbani kulifanyika Tambiko (mambo ya kiasili) na pia inaonekana na mambo ya kikanisa yaliganyika pia (sielewi uhusiano hapa) ila yote haya ni kuandaa wahusika kuishi pamoja.

Sasa mimi nina maswali hapa:

> Mke amemsamehe mume wake au bado?

>Je, kumsamehe mtu ni lazima mrudishe mahusiano yenu au kila mtu anaweza kuishi maisha mengine huku umemsamehe aliyekukosea?

> Mume huyu anajua kuwa alikosea?

> Huyu mume anaonaonesha kujutui alichofanya?

>Je, unadhani hawa wote wanaweza kutoka hapa walipo na kuishi maisha ya furaha na amani wakiwa pamoja au kutokuwa pamoja?

> Ushauri wako ni upo kwao?

Tazama video ya kisa hiki

View attachment 1427393
Hapana niliambiwa na bibi usimwamini mtu mlie pigana naye hata kama ni ndugu.
 
Back
Top Bottom