Kumsamehe mtu ni lazima muwe marafiki tena?

Kumsamehe mtu ni lazima muwe marafiki tena?

Display Name

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2014
Posts
423
Reaction score
451
Wakuu habari za muda huu,

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada ambayo naomba niiwasilishe kwa mtindo wa swali kwani natamani sana kujua majibu ya hili.

Je, nikimsamehe mtu ni lazima tuwe marafiki tena?

Mfano kwa kupitia kisa hiki;

Mume amegombana na mkewe na ikafika hatua ya mume kumjeruhi mke wake kwa kutumia kisu na shoka na kesi ikaenda kwenye yombo vya Sheria hadi kufikia mume kufungwa jela.

Mume akaja kupata msamaha wa Rais na akarudi nyumbani ambapo alikuwa akiishi mwanzo na mkewe ila mke akaomba muda wa kujifikiria na kwenda kuishi kwa mmoja wa watoto wao ambapo kwa kusikiliza panaonekana ni eneo hilo hilo kwani wanaweza kuonana muda wote na kuweza kula pamoja

Kufanya hadidhi ndefu kuwa fupi ni kwamba mume aliona maisha ya pale nyumbani magumu tofauti na matarajio yake na mke ndio anaonekana kushindwa kabisa hivyo sasa hivi mke kaondoka kirudi kwao na mume anasema haelewi kwa nini mke kaondoka.

Mind you: Mume alipotoka jela kwa msamaha kabla ya kutia mguu pale nyumbani kulifanyika Tambiko (mambo ya kiasili) na pia inaonekana na mambo ya kikanisa yaliganyika pia (sielewi uhusiano hapa) ila yote haya ni kuandaa wahusika kuishi pamoja.

Sasa mimi nina maswali hapa:

> Mke amemsamehe mume wake au bado?

>Je, kumsamehe mtu ni lazima mrudishe mahusiano yenu au kila mtu anaweza kuishi maisha mengine huku umemsamehe aliyekukosea?

> Mume huyu anajua kuwa alikosea?

> Huyu mume anaonaonesha kujutui alichofanya?

>Je, unadhani hawa wote wanaweza kutoka hapa walipo na kuishi maisha ya furaha na amani wakiwa pamoja au kutokuwa pamoja?

> Ushauri wako ni upo kwao?


Tazama video ya kisa hiki

 
Msamaha unatoka moyoni sio mdomoni

Kwaiyo inategemeana na namna ambavyo moyo wa huyo muombwaji umeridhia vipi, na pia huyo muombaji ni kweli anajutia kosa au ni drama ambazo zimejidhihirisha usoni kwake kiasi cha kumfanya muombwaji agundue kua ana ektiwa?
 
Najaribu kuvaa viatu vya huyo mama (mke) lakini havinitoshi.
Huyo mke hajamsamehe mume, kwa mazingira ya kosa la mume hata me sikusamehi na ikitokea nikakusamehe basi ni ule msamaha wa kupeana salamu tu sio kuishi pamoja.
 
Kwa mujibu wa swali lako jibu ni kuwa sio lazima muwe marafiki tena, ni muhimu.

Kuhusu huo mfano wako; wanandoa ni zaidi ya marafiki. Haijalishi wamekoseana nini, hakukuwa na haja ya kutengana.

Inavyoonekana bado hawajasameheana.
 
Labda kuna kosa jipya, kumbuka mume hakuwepo muda mrefu. Labda karudi na vitabia na utaratibu mpya wa maisha (aliojifunza/zoea mazingira aliyokuwepo awali kabla ya msamaha), sasa vinamshinda mke.

Lolote linawezekana wakati ana adjust kuishi mazingira mapya tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anatakiwa amfuate mke nyumbani kwao huku akionyesha ametubu kweli kwa kulia......
Duh, yani mke kasababisha uende jela halafu uponee chupuchupu utoke umfate akusamehe kwa kulia???Hapo kuna kitu zaidi ya jela unakitafuta. Kama nimempiga kwa upuuzi aliosababisha yeye ni haki yake na scale ya kipigo inaendana na kosa hata ikizidi, sikulewa, sijamuonea ametibua nimemrekebisha weee hasikii,

nikamzibua akaumia, akiyapeleka haya mambo kwa mjumbe tu hapo ni kwa heri ya ndoa mara 100 anishaki kwa wazazi wake au wangu. sembuse kwa mwenyekiti-polisi-mahakamani-jela...halafu nirudi nikamuombe msamaha hata kama angekuwa na utajiri wa Dangote HAITOKEI.
 
Duh, yani mke kasababisha uende jela halafu uponee chupuchupu utoke umfate akusamehe kwa kulia???Hapo kuna kitu zaidi ya jela unakitafuta. Kama nimempiga kwa upuuzi aliosababisha yeye ni haki yake na scale ya kipigo inaendana na kosa hata ikizidi, sikulewa, sijamuonea ametibua nimemrekebisha weee hasikii, nikamzibua akaumia, akiyapeleka haya mambo kwa mjumbe tu hapo ni kwa heri ya ndoa mara 100 anishaki kwa wazazi wake au wangu. sembuse kwa mwenyekiti-polisi-mahakamani-jela...halafu nirudi nikamuombe msamaha hata kama angekuwa na utajiri wa Dangote HAITOKEI.
Tatizo mzee hana dira hata kula yake ni ya shida,pia tukumbuke aimaanishi kuwa na mke/mume ndio tunahatimiliki ya uhai wake.Kutoa uhai au kujaribu kutoa uhai wake ni kosa
 
Tatizo mzee hana dira hata kula yake ni ya shida,pia tukumbuke aimaanishi kuwa na mke/mume ndio tunahatimiliki ya uhai wake.Kutoa uhai au kujaribu kutoa uhai wake ni kosa
ni sawa bro, nakubaliana na wewe kabisa ni kosa ila chanzo kingekuwa kinahusika katika kutoa hukumu ingekuwa ni vizuri zaidi. Sometime wanazingua sana na huyu jamaa hadi kufikia hivyo inaonesha alichoka.
 
ni sawa bro, nakubaliana na wewe kabisa ni kosa ila chanzo kingekuwa kinahusika katika kutoa hukumu ingekuwa ni vizuri zaidi. Sometime wanazingua sana na huyu jamaa hadi kufikia hivyo inaonesha alichoka.
Katika hali ya kawaida hata ukimkuta mkeo anafanya mapenzi na ukashuhudia kwa macho yako,hutakiwi kuua wala kujerui,we nikuchukua hatua za kuachana naye tu.
 
sahihi kabisa na ndio uamuzi wa busara zaidi..ila hapo ni Mungu akusaidie tu.
Ndio maana wazee wetu wa zamani kabla ya kufika nyumbani,walikuwa wanakooa au kutuma mtoto kwanza ili kama kuna chochote kilichopo ndani kikimbie,asije akasababisha maafa.
 
Siyo lazma muendelee kuwa marafik

Sent using GunTrigger
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom