Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,586
Mimi nimekuelewa, asie kuelewa ana yake mambo. Huwezi kupanda maharage ukavuna mahindi. Kazi ni dhamana, na dhamana ni huduma bora utakayo itoa kwa wananchi. No one will respect you if your don't respect your customers (in this case customers are wananchi).Ili mfanyakazi kwenye taasisi yeyote aweze kufanya vizuri sana "outstanding performance" anatakiwa awe na nidhamu ya hali ya juu, morali ya kazi, kujituma, ubunifu, elimu na ujuzi sahihi na kikubwa kupita vyote pengine ni dhamira njema. Kwa hiyo pamoja na juhudi za kujenga nidhamu ambazo kimsingi ni muhimu, ipo haja pia ya kuangalia ni kwa namna gani unaweza kujenga nidhamu na wakati huo huo hayo mengine nayo yakajengeka na kuimarika ili kuwa na matokeo bora.