Samahani, nikusahihishe ili nawe usiwe mpotoshaji. Hiyo digrii ya Fine and Performing Art (sic) haikuwepo mwaka 1974-77 Lowassa aliposoma digrii. Na kwa kuwa alisoma Education asingesomea FPA pekee, bali na kitu kingine kwa utaratibu wa major-minor. Digrii aliyopata Lowassa inaitwa Bachelor of Arts, ambayo pia walipata watu wengine waliosomea sayansi za jamii wakati huo, kama wachumi, wa sayansi za utawala, wanajiografia, wasosiogia, n.k. Kwa ujulisho, mchepuko mmojwapo wa masomo ya Lowassa unaoudhania ulikuwa na majina ya theatre arts. Mengi katika masomo hayo yanahusu ukuzaji wa vipaji vya kutenda na kusema mbele ya kadamnasi, ikiwa ni pamoja na uwasilishaji wa mada, uandaaji wa vipindi, utangazaji ktk runinga na uigizaji wa filamu - fani zinazoheshimika na kulipwa vizuri sana ktk ulimwengu wa kisasa. Pia, mapema kabisa, Lowassa alisoma na kutunukiwa digrii ya umahiri ya uchumi-maendeleo huko Bath, Uingereza.