Profesa Wajackoya: Raila Odinga alikuwa na CHADEMA akalega lega amerudi tena

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,011
Nchi na mataifa mbalimbali sasa wanaendeleza hamasa ya kuungana na chama chenye malengo ya kuongoza nchi kwa misingi ya amani, umoja, na upendo, na maendeleo pia na kuimarisha diplomasia. Hii ni kutokana na itikadi na misingi mizuri ya kuanzishwa kwake.

Prof Wajackoya, nguli wa sheria na mwanasiasa maarufu nchini Kenya, akitoa salamu zake kwenye mkutano mkubwa uliokusanyika kumpokea Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Godbless Lema, aliyewasili nchini mchana wa leo kupitia Uwanja wa Ndege wa KIA. Wajackoya anasema ametumwa na Mh Raila Odinga kuomba radhi kwa kuwa hapo nyuma alikuwa mshirika wa Chadema lakini akalega kidogo. Lakini sasa amerudisha uhusiano na chama hicho makini.

Itakumbukwa kuwa kwenye siasa za Tanzania miaka michache iliyopita, Raila Odinga alikuwa rafiki wa karibu sana wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kufikia kiwango cha kutembeleana mpaka nyumbani. Pia iliwahi kusemwa kwamba mmoja wa watoto wa Dr John Pombe Magufuli (R.I.P) alikuwa anasomea Kenya akiishi kwenye familia ya Raila.
 
Shida ni mmoja akishapata madaraka anaona chama rafiki ni maadui na ataanza kushirikiana na vyama tawala vya nchi jirani
 
Shida ni mmoja akishapata madaraka anaona chama rafiki ni maadui na ataanza kushirikiana na vyama tawala vya nchi jirani
Lakini analazimika kufanya hivyo maana anadumisha urafiki wa Kitaifa na sio wake binafsi? Au sio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom