Kumlinganisha Odinga na Lowassa si sawa, Naweka kumbukumbu sahihi

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,621
2,000
Kumekuwa na upotoshwaji wa baadhi ya watu kumlinganisha Lowassa na Odinga ambaye ni mwanasiasa mwandamizi nchini Kenya.

Raila Odinga ni mtoto wa mwanasiasa,mfanyabiashara na makamu wa kwanza wa Raisi Kenya Mzee Jaramongi Odinga wakati Edward Lowassa ni mtoto wa tarishi wa mahakama ya serikali ya kikoloni na baadaye Tanganyika kabla ya kustaafi mwaka 1975 aliyehamia Monduli toka Usariva,hakuwahi kuwa mfugaji.

Raila Odinga ni mwanasiasa wa upinzani kwani baada ya Kenya kuanzisha vyama vingi alijiondoa Kanu ambapo mwaka 1992 Babake aligombea uraisi huku yeye akishinda ubunge huko Siaya kwa tiketi ya upinzani.Edward Lowassa hajawahi kuwa mpinzani kwani alibaki CCM na amekuwa mbunge wa CCM na hataweza kushika nafasi yoyote ya kisiasa nje ya CCM.Alijiunga na upinzani kugombea uraisi tu,ni kama mchezaji wa ndondo.

Raila Odinga ni mwanasiasa mwenye hoja wakati Lowassa ni mwanamaigizo mwenye kutegemea mazingaombwe,unabii,ramli ili kuonyesha jamii anaushawishi,hutegemea pete na muelekeo wa nyota kama mvuto.

Kielimu Raila ni Mhandisi aliyepata shahada yake huko Ujerumani Lowassa anamiliki shahada ya sanaa za maigizo aliyopata UDSM kitengo cha "Fine and Performing Art" (FPA).

Raila Odinga ni Waziri Mkuu mstafu wa Kenya aliyetumikia nchi miaka mitano bila kashfa na kumaliza kwa heshima huku Lowassa ni waziri mkuu aliyekimbia kufukuzwa kazi na wabunge kwa wizi wa mchana.

Haya ni machache yanayowatofautisha Odinga na Lowassa ambayo kimsingi yanaweka msingi wenye lengo la kuondoa upotoshaji uliowekwa mitandaoni.
 
MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,265

Inawezekana hukuelewa context ya kuwafananisha RAO na EL! Labda wewe ulitaka wafanane mpaka vinasaba (DNA); Duh!!!
 
goodluck5

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
4,041
2,000
Mkuu sina hakika sana na taarifa yako.....binafsi mara baada uchaguzi mkuu mwaka jana akili imenirudi na imegoma tena kumkubali laigwanani ingawa kura yangu ya hasira aliipata kwa kuichukia kwangu ccm.
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,621
2,000
Kwa mantiki hiyo hakuna anayefanana na mwingine dunia hii!Kama unabisha mtaje halafu mimi nije na tofauti!
Nways naona lengo lako ni kumponda lowassa!Mbona hujatoa tofauti ya kuwa lowassa aliwahi kuwa waziri wa maji na kwa miaka mingi huku Raila hajawahi!
Hakuna nilipomoonda mtu.Nashukuru umeongeza hilo la waziri wa maji.
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,938
2,000
Nimeweka kwa mapana,hawa watu hata kisiasa hawafanani.
Kwanza ungeweka rejea hiyo ya kwafananisha Raila na Lowassa ili tuweze kuupata vizuri huo mlinganisho uliotoa. Ni sawa na kulinganisha Juliana Shonza na Wema Sepetu kwa vile walishiriki wote mchujo wa kura za maoni na kuanguka ila huyu Juliana Shonza vikatumika vigezo vingine akapata Ubunge wa VITU maalum. Vigezo vingine ni nini? Hakuna anayejua zaidi ya hao wanaume walio mpa ubunge na yeye mwenyewe.
 
MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,265
2,000
Nimeweka kwa mapana,hawa watu hata kisiasa hawafanani.
Kufanana sio lazima Uwe kama photocopy au identical twins; kwa mfano 1: wamekuwa wabunge wa muda mrefu sana wa majimbo yao; RAO (LANG'ATA NAIROBI) na EL (MONDULI ARUSHA) 2: wameshika wadhifa wa uwaziri Katika nchi zao 3: wamekuwa mawaziri wakuu katika nchi zao respectively na 4: Hakuna ubishi kwamba RAO na EL ndio wanasiasa wa siasa mbadala (upinzani ukipenda!) kabla na baada; wenye mguso mkubwa zaidi (de facto opposition leaders) katika nchi zao kuliko mwanasiasa mwingine yoyote Kenya na Tanzania respectively!
 
Lowassa si kiongozi wa upinzani bali ni mgombea uraisi tu yaani "mchezaji wa ndondo"....hakwenda upinzani sababu anataka bali kugombea uraisi RAO alienda upinzani wakati nchi imeingia kwenye vyama vingi hata kuacha ulaji kuunda upinzani uliokuwa mchanga.
 
Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,989
2,000
Lowassa si kiongozi wa upinzani bali ni mgombea uraisi tu yaani "mchezaji wa ndondo"....hakwenda upinzani sababu anataka bali kugombea uraisi RAO alienda upinzani wakati nchi imeingia kwenye vyama vingi hata kuacha ulaji kuunda upinzani uliokuwa mchanga.
Unaweza andika mambo gani wanafanana?
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,621
2,000
Kwanza ungeweka rejea hiyo ya kwafananisha Raila na Lowassa ili tuweze kuupata vizuri huo mlinganisho uliotoa. Ni sawa na kulinganisha Juliana Shonza na Wema Sepetu kwa vile walishiriki wote mchujo wa kura za maoni na kuanguka ila huyu Juliana Shonza vikatumika vigezo vingine akapata Ubunge wa VITU maalum. Vigezo vingine ni nini? Hakuna anayejua zaidi ya hao wanaume walio mpa ubunge na yeye mwenyewe.
Ni matumaini yangu ubongo wako umeshiba kwa chakula nilichoweka hapa jamvini.Karibu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom