ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,543
Jana kupitia habari saa mbili usiku Utv kuna mwekezaji toka arabuni ameletwa huko Njombe na tayari yupo mbioni kutaka kuwekeza katika zao la Parachichi akihitaji apatiwe maelfu ya hekari.
Imeelezwa Tanzania ni kama nchi ya tatu au nne katika nchi zinazotoa parachichi bora kabisa duniani.hii ina maana soko la uhakika lipo.
Nimejiuliza tumeshindwa kujiongeza sisi kama nchi kupitia wizara za fedha/kilimo/Sua kuwa organize vijana tuliojazana mitaani kwa kukosa ajira kukatiwa vipande vya mashamba either kwa vikundi au mtu mmoja mmoja kuwezeshwa vianzio na baadae kurejesha yaani kuwe na mpango maalum wa kuzungusha mitaji.
Hawa vijana wangezalisha parachichi kwa wingi serikali ikatafuta masoko duniani hapo serikali ingepata pesa za kigeni,vijana wengi tungeweza kujipatia ajira ya kudumu na kujikimu na maisha.
Zoezi hili lingefanyika sehemu tofauti nchini kwa mazao tofauti kutegemea na hali ya hewa sememu husika
Hilo pia lingefanyika kwenye mabonde makubwa,upande wa uvuvi maziwani humo,kwenye ranchi za taifa upande wa ufugaji,asali,upande wa uwindaji pia kilimo cha mboga na matunda,migodini nk
Nina imani seikali kupitia wizara zake wangezingatia hili tatizo kubwa la ajira na umasikini lingeenda kupungua pakubwa
Tujitaahidi kuilinda ardhi na mali asili zetu zilinufaishe taifa na Watanzania,bado ninaamini ile kauli ya baba wa taifa kwamba ili tuendelee tunahitaji Watu na Ardhi.
Rasilimali zetu tuzitumie sisi wenyewe kwanza kabla ya kuita wageni kwa mambo ambayo hata sisi tunaweza kufanya.