Kumfuma mke akichat na mwanaume mwingine

Kumfuma mke akichat na mwanaume mwingine

Mkuukiukweli kila mwanamke utakaemuoa alikuwa na mtu wake, mimi wakati nakutana na mama mtoto 2010 aliniambia kila kitu nikakubaliana nae ila hakuniambia kama kuna jamaa wa kijijini kwao ambae alikuwa nae na bado wako nae, miaka ikasonga hadi mwaka jana ndo mambo yalianza kubadilika nikajifanya mjinga huku nikitafiti mdogo mdogo kiukweli MUNGU hamfichi mnafiki siku nikafuma kila kitu from whatsapp to facebook. Nikambana ki-askari akakubali na kuomba msamaha ila kiukweli mapenzi yalipungua kwa kiasi kikubwa, na miezi 8 mbele nikaona amani hairudi ndani kila siku ni ugomvi mie nikajiengua, nimemua tu aishi mwenyewe na kama ataamua kuolewa tena na huyo jamaa wa huko kwao its fine tulikuwa na mtoto mmoja na nimemuachia akae nae tu maana ukingángánia haya mambo unaweza kufa kwa pressure, its much better kila mtu akakaa pembeni ili tuone baada ya muda nani atakuwa muathirika. Still niko kwenye 30th ila ngoja nisogee kwenye 40 nitaoa tena kwa sasa hapana tena nawachukia sana hawa viumbe.Na inaumiza sana
Real sure bro...mimi mwenyewe nime decide hivyo but nataka nimuache peacefully
 
Ushauri gani huu? Ukute jamaa ana kisukari tayari, mambo ya kukuna keshakatazwa na daktari. Huoni unaomwongezea presha? hahahahaha.
No am physically an mentally fit bro so everything working perfect
 
Ni kweli lakini labda nikuulize mkuu kwa hiyo niendelee kumvumilia mtu huku akiendelea na mahusiano na mtu mwingine nje??
Ukimchunguza kuku huwezi kumla na kushauri usipekuwe simu ya mkeo asilimia kubwa ndoa unazoziona ni uvumilivu.
 
Kwanza kwa nini ukague sm ya mkeo? Huna imani naye au? Hivi, kuna mtu duniani anayemjali mwenziye au anamtaka mwenzie ajue kuwa ana cheat kweli? Faham kuwa kama kweli anajua kuwa kaolewa, hawezi kuacha meseji za kipuuzi ka hizo kwenye sm halaf aiache sm uione. Kaamua, na hii ni kutaka ku draw your attention kwake. Ameona umezidi kumdharau, na mtu pekee anajua unaweza ku mmind ni huyo ex wake. Hawana uhusiano wowote zaidi tu ya kuhurumiana. Amemweleza mapito yenu na jamaa aawa anamtiz tu usiogope. Mrudishie haki yake mkeo, sidhani hata ka una ham naye tena. Acha kumtesa mtoto wa watu naye kazaliwa kama weye
 
M
Habari jamani humu ndani,

Hivi mtu unakuwa na ugomvi kila siku na mkeo huku sababu za ugomvi hata hazieleweki,visilani tu kila kukicha hakuna jema utalomfanyia akaridhika yeye kila jambo umfanyialo kwake baya mwisho wa simu unazifuma text anazochati na mwanaume mwingine wa nje ambaye alikuwa mtu wake wa zamani ambaye kwa mujibu wa text hizo zinaonesha mahusiano wameyarudisha tena sasa wadau hivi huyu mtu/mke kuna ya kuendelea tena na ndoa hapo?

Ushauri tafadhali.
Mh!, mbona Kama unanisema Mimi Tu!, maana nimetafutwa weekend hii, ila kijiografia nipo mbali Na huyo x- wangu. Lakini sija-intend kujikumbushia enzi zileee!, kwa sababu nilikojiegesha kunatosha!. Pole!.
 
Wachaga tuna msemo mmoja unasema "ng'ombe aliyezoea kucheza zizini, haachi kucheza mpk umchinje asije akazaa kizazi kikarithi hiyo tabia" so mke hajitambui nn maana ya ndoa/kuolewa chukua maamuzi magumu
 
Yaaani wewe umenigusa kuliko maelezo. Na hili ndio tatizo kubwa, washauri kusikiliza upande mmoja na kutoa ushauri ili hali hawajui ya upande wa pili. Hapo ndio ukute mawifi na mama mkwe kama mie, anaapia na kuapia kuwa ukiendelea nae huyo nakulaani! There is no excuse to cheating lakini mara chache sana mtu ataamka tu na kumkumbuka x-wake
Halafu kama ukichunguza hapa jf stori nyingi mtu akileta anajifanya yeye yupo innocent sana wakati kumbe yeye ndio aliyeanzisha hilo tatizo. Kuna siku rafiki yangu mmoja alitaka nimpe ushauri juu ya tatizo lake na mpz wake nikamwambia mlete na huyu mwenza wako walipokuja. Huwezi kuamini nani aliyekuwa mkosa na kuanza kuomba samahani, Mara nyingi mimi huwambia watu kuweni na maongezi ya nini aongeze au nini apunguze kwenye uhusiano wao, japo mara moja kwa mwezi na wake/wapenzi wao huondoa hata khofu na ugomvi wa mara kwa mara.
 
Halafu kama ukichunguza hapa jf stori nyingi mtu akileta anajifanya yeye yupo innocent sana wakati kumbe yeye ndio aliyeanzisha hilo tatizo. Kuna siku rafiki yangu mmoja alitaka nimpe ushauri juu ya tatizo lake na mpz wake nikamwambia mlete na huyu mwenza wako walipokuja. Huwezi kuamini nani aliyekuwa mkosa na kuanza kuomba samahani, Mara nyingi mimi huwambia watu kuweni na maongezi ya nini aongeze au nini apunguze kwenye uhusiano wao, japo mara moja kwa mwezi na wake/wapenzi wao huondoa hata khofu na ugomvi wa mara kwa mara.
Tunataka kutoa vibanzi toka macho ya wenza wetu bila ya kutoa boriti kwenye macho yetu
 
Ni kweli lakini labda nikuulize mkuu kwa hiyo niendelee kumvumilia mtu huku akiendelea na mahusiano na mtu mwingine nje??
Usijidanganye huwezi kumtidhisha mwanamke Kwa kila kitu ,kama ka rudisha mawasiliano mana yake kuna vitu kwako hapati na huenda anajuta.mwanamke ni mtu mwenye msimamo lakini wakiyumba wana yumba kweli kweli so hapo kimbia
 
Ukiona manyoya ujue kaliwa huyo,,,Pole sana mkuu fukusa hiyo muke haraka sana
 
Fukuza huyo unasubiri nn??? Ila tambua mke ni wako na maamuzi yoyote utakayochukua juu yake yanatoka kwako asilimia100 maana faida zake na hasara zitakuhusu wewe binafsi
 
Back
Top Bottom