Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,012
- 5,571
Muhongo asema Sekta Binafsi "mguu sawa"
WAZIRI wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo ametaja vigezo vitakavyotumika kuwapata watendaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi ya Uganda.
Profesa Muhongo ameyasema hayo ikiwa ni siku moja tu baada ya kuwasili nchini akitokea Kampala, ambako alihudhuria kikao cha viongozi wa nchi wanachama wa jumuia ya Afrika Mashariki ambapo Rais Yoweri Museveni wa Uganda alitangaza uamuzi wa Serikali yake.
Rais Museveni aliitangaza njia ya Kabaale hadi Tanga nchini kuwa ndio sahihi kupitisha mafuta ghafi yake.
Baadhi ya vigezo vitavyotumika kuwapata Viongozi na Watendaji hao ni hizi kama vifuatavyo: Uadilifu, Uzalendo, Ubunifu na Utaalamu.
Aliendelea kusema kuwa vigezo vingine ni Uzoefu, Umakini, Ufanisi, Ushirikiano, Historia ya mafanikio kikazi na kasi ya utekelezaji wa majukumu yaliyotolewa.
"Tumedhamiria kupunguza muda (mid 2020) uliopangwa wa kukamilika kwa Bomba hili mapema zaidi," alisema Prof Muhongo.
Waziri alilakiwa kwa mbwembwe na bashasha na wananchi waliojitokeza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Profesa Muhongo ameitaka SEKTA BINAFSI kujiandaa kwa kazi za aina mbalimbali zitakazotangazwa karibuni.
Katika mchakato huo, Tanzania ilipata upinzani mkali sana kutoka kwa Serikali ya Kenya, ambao walitaka bomba hilo lipitie katika bandari ya Lamu yenye miundombinu hafifu.
Mbali na miundombinu hafifu na hatari ya uwezekano wa hujuma kutoka kwa magaidi wa al-shabab, ingechukua muda mrefu zaidi hadi mwaka 2022 kumaliza ujenzi wa bomba hilo.
Habari kutoka chanzo cha habari cha kuaminika kimemtaja Mwanasiasa maarufu, Makongoro Nyerere kuhusika katika ushawishi wa mradi huu.